KOSA LANGU NI LIPI? Sehemu ya 12
ILIPOISHIA
Hee leo umepotea njia Joyce alicheka kidogo
na kusema Lina na wewe hata salamu Lina
akamjibu Mwenzangu nimeshangaa kukuona.
hatujaonana siku nyingi au ndiyo shemeji
anakuficha Baadaye alimkaribisha ndani na
kumpatia kinywaji, na waliendelea
kuzungumza Eeh rafiki yangu, niambie za
huko kwako vipi shemeji mzima Alisema
Lina.Joyce alinyamaza kimya kidogo na kujibu
Mzima lakini huko si kwema sana, nina tatizo
kidogo. JE NINI KITAENDELEA
USIKOSE ....SURA YA.....12.......
INAPOENDELEA
Tatizo gani tena wewe mwanamke una mume
anakupenda. kila kitu unapata sasa una
matatizo gani Alisema Lina huku akiguna
kidogo. Joyce alimjibu Tatizo ni kupata
ujauzito,hapa nilipo sijui nifanyeje natamani
kweli kupata mtoto na Fredy jana alipofika tu
baada ya kutoka kazini amelizungumzia hilo na
kusema anataka mtoto Lina alimsikiliza kwa
umakini na kusema Sasa hapo kuna tatizo
gani, ni kwenda tu Hospitali. mkaangalie kama
kuna tatizo. Mshauri mume wako ili muende
kwa wataalamu watawasaidia, mbona kuna
watu wanakaa hata miaka kumi ndiyo wanakuja
kupata mtoto Joyce akamjibu lakini kweli
rafiki nitafanya hivyo. Waliendelea
kuzungumza baadaye Joyce aliondoka na
kurudi nyumbani.
Huko nyumbani siku zilivyozidi kwenda Fredy
aliendelea na nia ya kutaka kupata mtoto.
Ndipo Joyce alipoamua kumuambia kuhusu
kwenda Hospitalini. Siku hiyo Joyce alifika
nyumbani na kufanya kazi zake za nyumbani
kama kawaida kisha aliketi sebuleni akimsubiri
Fredy ili amshauri kuhusu kwenda hospitalini.
Akiwa pale sebuleni moyoni mwake aliwaza
akisema Eeeh Mungu naomba unisaidie
nipate mtoto, hivi inawezekana labda kizazi
changu kiliharibika nilipokuwa natoa mimba,
kipindi nipo kwa Maliki sijui nitafanyaje kama
mimi ndiye mwenye tatizo na Fredy hafahamu
kama mimi nilishawahi kutoa mimba naogopa
sana kumpoteza Fredy.
Akiwa anaendela kuwaza alishtuka Fredy yupo
karibu yake. Fredy alimshangaa na kusema
Vipi mke wangu mbona una mawazo sana
yaani mimi hadi naingia ndani hunioni
unawaza nini? Joyce aliamua kutabasamu
kisha kusema Samahani mume wangu
nilikuwa nimepitiwa kidogo ila pia nilikuwa
nawaza kuhusu wazo la kupata mtoto Kabla
hajamaliza kuzungumza Fredy akasema Vipi
kuna dalili ya ujauzito mke wangu
Joyce akasema Hapana nilikuwa napendekeza
tuende Hospitalini kuangalia kama kuna tatizo
naamini watatusaidia Fredy alicheka kidogo na
kusema Unajua mke wangu nilijua ipo siku
utaniambia hivyo, mimi sina tatizo na kwanza
nilipoona tumekaa muda mrefu bila ya kupata
mtoto. Niliwahi kumuomba Daktari aniangalie
kama nina uwezo wa kumpa mimba
mwanamke. Na majibu ninayo kwamba sina
tatizo. Kwahiyo wa kwenda Hospitali ni wewe
na si mimi
Joyce alishangaa na kusema Lakini Fredy,
haujanitendea haki mume wangu. Kwanini
hukunishirikisha Fredy alinyamaza kimya
kidogo na kusema Naomba unisamehe mke
wangu, kwani niliogopa nikahisi isije ikawa
mimi ni tatizo. nilitamani kujua mapema
samahani kwa hilo Joyce aliinama chini kidogo
kisha akamwangalia mume wake na kumuahidi
ataenda kuangalia nini tatizo. Ilipita kama wiki
moja tokea Joyce na Fredy wazungumze juu ya
kupata mtoto mambo yalizidi kuwa mabaya
kwa upande wa Joyce kwani hata ndugu wa
Fredy walianza kuhoji kuhusu mtoto.
Siku moja Mama yake mzazi na Fredy alienda
kuwajulia hali Joyce na Fredy. Siku hiyo
alimkuta Joyce kwani Fredy alikuwa hayupo
kwa wakati huo."Habari za hapa Joyce, binti
yangu naona unazidi kupendeza" Alisema
Mama Fredy. Joyce alijibu huku akionyenya
tabasamu pana "Asante mama jamani
nimefurahi umekuja kutusabahi, nikuletee
kinywaji gani Mama yangu" Mama Fredy
akamjibu "Hapana Joyce usiniletee chochote
embu keti kwenye sofa kwanza tuzungumze".
Joyce alijisogeza huku akisema "Lakini mama
si ningekuletea angalau hata soda" Mama
Fredy akasema "Hapana Joyce hizo soda
nakunywa kila siku, mimi kilichonileta hapa
nataka kujua hivi unawaza nini kuhusu kupata
mtoto jamani" Joyce alinyamaza kimya kidogo
bila kujibu chochote kana kwamba kuna kitu
anatafakari "Hivi si nazungumza na wewe Joyce
inamaana hunisikii" Alihoji Mama Fredy
"Hapana Mama, Mimi na mume wangu
tumeshalizungumzia suala hilo la kupata
mtoto.Kwani muda bado upo Mama mtoto
atakuja tu" Alisema Joyce huku akimtizama
mkwe wake, ambaye hakuridhika na majibu ya
Joyce "Muda upo! muda gani huo? Wakati
ndiyo huu, natamani sana kumuona mjukuu
wangu, au wewe binti ni mgumba?" Aliuliza
mama Fredy.
Joyce alionekana kukosa amani na kusema
"Jamani Mama kupata mtoto ni mipango ya
Mungu. Naamini Mungu atatusaidia tu...."Kabla
hajamalizia kuzungumza Mama Fredy
alimkatisha na kusema "Sikiliza nikuambie
binti mimi naona hapa kuna tatizo. Sasa kama
mwanangu ameoa mwanamke mgumba,
itabidi atafute mwanamke mwingine ili azae
naye. siwezi kukubali mwanangu asiwe na
mtoto wakati wanawake wapo wengi" Joyce
alimsikiliza Mama Fredy kwa umakini na
kusema "Lakini mama mbona unafika huko"
Alilalama Joyce Mama Fredy akamjibu kwa
sauti iliyojaa jazba "Huko wapi?Ahera au, tena
sikiliza nikuambie fanya ufanyalo mimi nahitaji
mjukuu. alaah! Hivi unafikiri hili jambo ni dogo
eeh, mimi naondoka lakini tuliyoyazungumza
hapa ukae nayo kichwani na uyafanyie kazi"
Aliongea huku akiondoka na kumuacha Joyce
akiwa ameketi pale sebuleni. JE NINI
KITAENDELEA USIKOSE SEHEMU YA ......13.....