Hadithi ya Kongamano la Iringa

Hadithi ya Kongamano la Iringa

aisee ni taamu sana...naisubir inayofuata
 
KONGAMANO LA IRINGA-4



Naomba niendelee na simulizi hii tam na yakusisimua, sehemu iliyopita tulimuona Ray akiwa bado amezimia. huku Cheni akimpeleka Vai Kwenye kongamano la CHALUFAKITA. Hata hivyo Vai anazidiwa na usingizi na kusinzia ukumbini, akiwa amesinzia anaota ndoto ya ajabu sana.
Vai anaendelea kusimulia.....
Nilishtuliwa na kijana mmoja ambae hata jina sikumfahamu nikajikuta napiga kelele kuwa sio mimi...!yule kijana akaniuliza "sio wewe kivipi? " nikamwambia samahani nilikuwa naota tu, basi akaniambia kuna mtu anakuita hapo nje, mmmh...! hofu ikazidi kuniingia moyoni mwangu, nikajiuliza ni nani huyo na anataka nini? Ilinibidi niende tu nilipofika huko nje nikakutana na baba mtu mzima, akajitambulisha kwa Jina kwa jina la Mzee Chipula. Mzee Chipula akanisalimu; habari yako Dada? Je Unanikumbuka?" Nikamwambia hapana, akasema Mimi nishawahi kukuona Dar maeneo flani hivi" au sio wewe?"Mimi nikamuangalia tu nikanikaona kama ananichanganya akili yangu. Akaendelea kusema tangu umekuja unaonekana huna raha kabisa, pia nahisi unamatatizo kwani kitu gani kimekusibu mrembo kamawewe?" Hapo nikajiuliza sijui nimwambie yaliyonisibu au nisimwambie? lakini nikajisemea moyoni endapo nitamwambia na baadae nikakuta mume wangu amefariki yaani yeye ndie atakuwa wa kwanza kunipeleka polisi. Nikamjibu hapana sijiskii vizuri kabisa, "akaniuliza kwani umefikia wapi?" Nikamwambia hoteli moja hivi iko mjini, akasema "kama hutojali kongamano likiisha tuondoke wote nikapafahamu ulipofikia. Mmmh....!moyo ukanipasuka paaaa nikajiuliza huyu ni mpelelezi au? Mbona anamaswali mengi kiasi hiki? Nikamkunjia sura Nikamwambia samahani naomba uniache nenda ukaendelee na mambo yako, sitaki kufatiliwa maisha yangu. nilimjibu kwa jazba sana mpaka akaogopa.
Niliiingia ndani kwenye kongamano na baada ya muda kidogo ukawa ni muda wa mpumziko kwa ajili ya chai. Chai ilikuwa nzuri sana yenye vitafunwa vingi lakini kwangu niliiona chungu kama kwinini, kwani kila nilipomfikiria mume wangu Ray kamba alizofungwa na mateso aliyoyapata sababu ya kupigania mke wake, roho Iliniuma sanaaa hata chain haikupita, nikajikuta nadondosha machozi mbele ya watu wote.
Mara ghafla akaja mtu akanipa leso ya kujifutia, nilipomuangalia usoni alikuwa mzee chipula, nikazidi kukasirika zaidi nikamuuliza hivi wewe zee zima unajibaraguza nini kwangu, unataka kitu gani hasa? Ujana wako umekula na Nani hadi uzee ule na Mimi? Nikakichukuwa kile kitambaa nikakitupa chini.

Baada ya chai watu walirudi ukumbini na kuendelea na Ratiba ambapo mada mbalimbali ziliwasilishwa, mimi nikamuomba muongozaji anitoe katika ratiba ya kuwasilisha mada kwani mada niliiandaa lakini sijiskii vizuri kabisa, wakati naongea hayo na kiongozi yule mzee likuwa pembeni akadakia na kusema " Mimi nitaiwasilisha hio mada badala yako," Moyoni nilichukia lakini ikanibidi nimuachie tu aiwasilishe kwa sababu imeshapangwa kwenye ratiba.
Mada ziliendelea kuwasilishwa, lakini mimi nilikuwa sielewi kitu, niliwaza sana mambo mengi kichwani, niliwaza hatma ya mume wangu, je?yu hai au amekufa? Nikawaza hatma ya ndoa yangu kuwa je hata akifanikiwa kupona atanisamehe kweli au atanilipizia kisasi? Hayo na mengine mengi yalikuwa yakiniumiza kichwa sana hata nisijue nini cha kufanya.

Mara chakula cha mchana kilikuwa tayari na watu wote tukahitajika kupanga foleni, nilijivuta taraatibu na kutoka nje, Watu wengi sana walikuwa wakifurahiasiku hio na kuanza kupiga picha mbalimbali na walimu wao, pamoja na marafiki zao, Mimi nilikaa pembeni nikiwatazama tu ikafika kipindi watu waliokuwa wanapiga picha za ukumbusho nikawa naona kama wanapiga picha za marehemu mume wangu katika hatua ya mwisho ya kuuaga mwili wake, pia nilipoangalia foleni ya watu waliojipanga kwa ajili ya kupata chakula nikawaona kama watu waliojipanga mstari kwa ajili ya kwenda kuuaga mwili wa marehemu mume wangu. Ama kweli majuto ni mjukuu nilijilaumu sana kwa kitendo nilichokifanya, nikajikuta namchukia sana Cheni nikaona kama ni ibilisi aliekuja kuharibu ndoa yangu.

Baadae nikajipa moyo konde nikasema hili ni jaribu kutoka kwa mwenyezi mungu na ninahakika nitalishinda tu. Japokuwa sikuweza kula chakula lakini nikajikaza nikaingia ukumbini nikiwa na ujasiri mkubwa sana. Mada ziliendelea kuwasilishwa mpaka ilipofika saa moja usiku, nikaondoka kwenye kongamano nikaenda hadi geti kuu la kuingilia chuo kikuu cha Iringa, nikampigia Cheni simu aje anichukue lakini nilipompigia simu yake ikawa haipatikani, nikajaribu tena na tena lakini simu ikawa haipatikani kabisa. Na kwa wakati huo kulikuwa hakuna daladala hata moja kutokana na wanafunzi Wa chuo hicho kuwa likizo.
Wakati nikiendelea kutafakari nini cha kufanya, ghafla nikakuta mtu ananishika begani, nilipogeuka alikuwa ni mzee Chipula, akaanza kuongea kwa madaha huku akitingisha funguo zake za gari " mmmh...! Malkia wa ulimwengu unafanya nini hapa muda huu, wewe sio binti wa kusubiri daladala bwana njoo nikusindikize unapoenda" mwanzoni nilikataaa lakini nilipoona imeafika saa mbili usiku ilinibidi nikubali kishingo upande, nikapanda ndani ya gari nikakaa siti ya nyuma.
Gari lilipoondoka mzee chipula akaanza tena maongezi, akaseama... " binti, kumbuka akufaae kwa dhiki ndie rafiki naomba niwe rafiki yako mrembo, mimi sina nia ya kukuchezea bali nataka nikusaidie".
Niliona kama ametonesha kidonda ambacho ni kibichi kabisa moyoni mwangu, nikamjibu kwa kauli Moja tu kama hutaki kunipeleka naomba nishushe. Mzee Chipula akona anyamaze kimya.
Aliendesha Gari kwa kasi mpaka tukaingia mjini, tulipofika karibu na ile hoteli nikamwambia niache hapohapo tafadhali, akaniacha kisha akanipa kadi yake yenye namba za simu akaniambia nikiwa na shida yoyote nimtafute, nikaipokea ile kadi nikaondoka.
Hofu ya kuingia hotelini ilizidi kutanda tena katika moyo wangu huku nikitarajia kukuta mambo mawili, Ray akiwa mzima au amekufa. Wakati naingia hotelini kwa kunyata ghafla nikashtuliwa na sauti ya Dada mhudumu ikiita, " Dada, we Dada funguo yenu hii hapa, mwenzako amesema ametoka kidogo ila atarudi muda sio mrefu."
Nilifurahi sana kusikia maneno hayo nikainyakua ile funguo haraka, huku nikijisemea moyoni kuwa naenda kumtorosha mume wangu Ray haraka sana, nikasema nitapanda hata malori ya kwenda Dar ili tutoroke na mume wangu.
Nikafungua mlango haraka haraka nikaingia ndani. LOOH.......! SIAMINI NILICHOKIKUTA[emoji134]
JE NINI KITAENDELEA....?
USIKOSE TOLEO LIJALO....



ENDELEA..............




KONGAMANO LA IRINGA-5

Naomba nindelee na simulizi hii tam na ya kusisimua, sehemu iliyopita tulimuona Vai akirudi kutoka kwenye kongamano na kukuta Cheni ametoka. hivyo akaamua aingie ndani haraka ili akamkomboe na kumtorosha mume wake mpenzi Ray.
Vai anaendelea kusimulia....!
Nilifungua mlango kwa haraka sana huku nikiwa na Furaha kubwa ya kumkomboa mume wangu.
Nilipofungua tu siamini nilichokikuta nilikuta matone ya damu yakiwa yameganda juu ya simenti, na Ray akiwa hayupo chumbani. Nilipojaribu kupekuwa pekuwa nikaona hata lile shuka lililokuwa limemfungia mdomo Ray lilikuwa linamatone ya damu. Nilijikuta naangua kilio kikubwa, Nililia sana nikiwa na hisi kuwa lazima Cheni atakuwa amemuua mume wangu Ray. Nililia kwa uchungu sana huku nikitafakari mambo mengi na jambo la kwanza nililokuwa nikitafakari ni kwamba Nitawaambia nini ndugu zake Ray? Je polisi wakijua nitakuwa katika mazingira gani? nikajiuliza pia kwanini Cheni ameamua kumuuwa mume wangu? Na je kama hakumuua atakuwa amepeleka wapi? Kwa kweli nilijilaumu sana kwa kitendo nilichokifanya.
Muda wa Masaa matatu yote nilikuwa nalia na kutafakari nifanye nini. Baadae nikapata wazo la kutoroka nirudi Dar haraka sana wakati huo ilikuwa ni saa tano usiku, baada ya kutafakari nikapata wazo nimpigie Mzee Chipula aje anichukue pale aliponiacha. Nikachukua simu ili nimpigie, nipochukua tu nikasikia hodi...hodiiii...!, moyo ukanipasuka paaaa! Nilifungua mlango na kuangalia nje kumbe alikuwa ni Cheni, akaingia ndani huku akiwa anahema sana. Nilikasirika nilipomuona, maana nilimuona kama muuaji mkubwa na pengine hata mimi anaweza akaniuwa.
Akaniambia " kaniwekee maji ya kuoga wewe mwanamke, mke gani huna hata upendo na mume wako?
Nikamsonya nyoooooo....! Baradhuli mkubwa wewe, nawezaje nikawa na mume jambazi katili kiasi hicho? Kwanza Ray umempeleka wapi? Akanijibu kwa ukali "Ulikomuacha Ray wakati unakuja huku ndiko nilikomrudisha, halafu kuanzia sasa hivi sihitaji swali jingine lolote lile la kipuuzi, kwanza wewe na mume wako mmenitia gharama nisizozitarajia".
Hasira zilizidi kunipanda nikatamani nimvamie nimpige, lakini sikuwa na uwezo huo hata kidogo.
Cheni aliingia bafuni akaoga kisha akapanda kitandani, akanivuta juu ya kifua chake, akaniambia, " Vai nadhani unajua fika jinsi gani ulivyouteka moyo wangu, nakupenda sana vai, nakushauri tuondoke Tanzania twende Nchi nyoyote unayoipenda tukaanze maisha yetu mapya kwani maji yakishamwagika hayazoleki, huwezi kurudiana na mume wako tena."
Nilimuangalia tu bila ya kumjibu kitu maana mpaka mda huo sikujua kama Ray amekufa au yupo hai.
Cheni alinibembeleza sana nishiriki nae tendo la ndoa lakini Mimi nilikataa katakata kwa kuwa nilitokea kumchukia sana, akaniambia wewe si unajifanya jeuri? Nitaiona jeuri yako leo, baada ya muda alinikamata kwa nguvu na kuniingilia kimwili, nilichukia sana kitendo hicho lakini nilipopiga kelele alinitishia akaniambi "weeee nitakunchangua ubongo sasahivi, unataka hela yangu niliolipia hoteli iende bure? mimi sio fala kama huyo mwenzio mume bwege."
Asubuhi kulipokucha nilijiandaa kwenda kwenye kongamano baada ya hapo alinipakiza kwenye gari lake na kunipa vitisho kuwa nisije nikathubutu kumwambia mtu yoyote kilichotokea na nikithubutu kumwambia basi atanishtaki Polisi kuwa nimemuuwa mume wangu.
Aliponifikisha Chuo Kikuu cha Iringa nikamwambia wewe si ulipania kongamano sana mbona huendi hata ukumbini, akaniambia haoni raha ya kwenda kufurahia huko kutokana na hayo matatizo yaliyotokea.hivyo akageuza gari na kurudi.
Ratiba ya kongamano ikaendelea kama kawaida na ikatanguliwa na utenzi na baadae mkuu wa wilaya kugawa vyeti, nilipokea cheti changu huku nikiwa sina raha hata kidogo.
Baada ya kumaliza kabisa shughuli zote za kongamano, Ilifatia ziara ya kwenda kuangalia makumbusho ya mkwawa wa Uhehe, historia yake yote na maisha alioishi mpaka kujiuwa. haikuishia hapo tukaenda mpaka bonde la Ismila. Huko niliona kidogo mawazo yakapungu maana tulipanda kwenye magari ambapo watu wengi walikuwa wanapiga story,wengine walikuwa wanachekesha sana na kunifanya nifurahi na kupoteza mawazo.
Baadae tulirudi mjini mimi nikaja kuchukuliwa na Cheni. Usiku huo nilijaribu kuwa mpole ili aniambie kama mume wngu yupo hai au la, yeye akanikaripia na kuniambia hataki maswali ya kijinga. Tulilala wote lakini mimi nikawa naomba mungu subuhi kuchwe Ili nirudi dar.
Asubuhi kulipokucha nikajiandaa na yeye akajiandaa kwa safari ya kurudi dar, Cheni alinisisitiza nifikie kwake, akadai nitaenda kupata tabu sana huko nitakakokwenda, mimi nilikataa katakata kwenda kwake, Yeye akanijibu kwa jibu kwa kejeli " mmmh....!mkataa pema pabaya panamuita". Mimi sikumjibu.
Tulipoanza kuingia Jiji la dar wasiwasi ukazidi kuniingia nikajiuliza niende kwangu au niende kwetu? Na nikienda kwangu Je nitamkuta Ray au Ameshauwawa?
Na je Nikimkuta hai atanifanya kitu gani?
Cheni alinishusha barabarani karibu na kwangu akaniambia lazima utanitafuta"
Mimi sikujali maneno yake nikashika njia ya kwenda nyumbani kwangu, nilipokaribia kufika mvua kubwa sana ilinyesha na radi kali ilianza kupiga, nilizidi kupata hofu na kuhisi kama mauzauza, lakini nikapiga moyo konde, nikaendelea kusogelea geti la nyumba yangu nikapiga hodi sana lakini sikuitikiwa, nikasukuma geti, kuangalia huku na huko hata mlinzi hakuwepo. Niliingia woga zaidi na mvua ilizidi kunitotesha, nikaingia ndani bila hata hodi,
LOOH NILIISHIWA NGUVU KWA NIYOYAKUTA.
JE NINI KITAENDELEA....?
 
Back
Top Bottom