umbwa mzee
Member
- Sep 16, 2016
- 11
- 2
TAMU NA CHUNGU YA KONGAMANO LA IRINGA.
Naitwa Vailet, wengi hupenda kuniita vai, Ni mkazi wa Dar es laam, ilala msimbazi center, huko ndiko ninakoishi na mume wangu mpenzi anaeitwa Ray, ambae tumeona miaka mitau iliyopita, mume wangu anafanya kazi ofisi za TRA Dar.
Katika maisha yetu tulikuwa tukiishi kwa furaha siku zote, mume wangu alinipenda sana na mimi pia nilimpenda Sanaaa, alikuwa akinijali na kunithamini sana,
Tangu tumeoana sikuwahi kumsaliti mume wangu hata Siku moja na yeye hakuwahi kunisaliti nikajua.
Mimi ni mhadhiri wa chuo kikuu cha dar es salaam. Ambapo nafundisha fasihi.pia ni mwanachama wa chalufakita.
wakati kongamano la chalufakita likiwa linatangazwa kwenye makundi ya what's up, kuwa litafanyika Iringa, yaani nilifurahi sana nikamshirikisha mume wangu, nikamwambia kongamano la chalufakita litaenda kufanyika iringa lazima twende wote. Mume wangu aliniangalia tu bila ya kunijibu chochote, kitu ambacho sio cha kawaida kabisa, kwani tulikuwa na tabia ya kwenda wo wote kwenye sherehe yoyote ile, hata ikiwa nje ya mkoa. Baadae akanijibu..." nitaangalia ratiba za kazi".
Ulipofika mwezi mmoja kabla nikamuuliza tena mume wangu kuhusu safari ya kwenda kwenye kongamano la chalufakita iringa, ndipo mume wangu akaniambia, " nakupenda sana malikia wangu, natamani tuwepo wote siku hio ya kongamano, lakini nisamehe sana, sitaweza kuhudhuria kongamano hilo kutokana na majukumu ya kikazi yalivyonibana, lakini wewe nakuruhusu uende, ila nakuusia usiache mbachao kwa msala upitao, ukajichunge sana huko uendakona pia fahamu ya kuwa sio kila king'aacho ni dhahabu, nakuomba sana mke wangu kamwe usijeukavunja heshima ya ndoa yangu ambayo tumeiweka ndani ya miaka mitatu sasa".
Aliongea kwa hisia kali sanaa mpaka nikapata wasiwasi.
Lakini nikamuitikia, nimekuelewa mume wangu kamwe siwezi kukusaliti.Siku zilizidi kwenda tukawa tunaishi maisha ya Furaha sana na mume wangu.
Zikiwa zimebaki wiki tatu kabla ya kongamano,
Siku moja nilipokuwa kazini akaja secretary akaniambia madam kuna barua yako, nikamuuliza inatoka wapi? Akaseama utasoma mwenyewe.
Ndipo nikapokea barua ambayo sikujua nani kaituma. Moyo ulinipasuka sana, lakini nikaifungua muda huohuo, kumbe barua hii alikuwa ameandika mpenzi wangu wa zamani ambaye nilikuwa naye kabla ya kuolewa na alijulikana kwa jina la Cheni.
Cheni alikuwa mpenzi wangu wa zamani kabla sijaolewa, na tulikuwa tunafanya nae kazi chuo kikuu cha dar es salaam yeye akifundisha isimu na mimi nikifundisha fasihi. Cheni alinipenda sana na tuliwekeana ahadi kedekede, ikiwemo ahadi ya kuja kuoana, lakini ahadi hio ilivunjika baada ya yeye kwenda kujiendeleza kimasomo nchini Uingereza. Hata hivyo baada ya kumaliza masomo yake alifanikiwa kupata kazi hukohuko na kukataa kurudi Tanzania kabisa.
Roho iliniuma sana kwa kumpoteza mpenzi wangu huyu ambae nilimpenda kwa dhati, kibaya zaidi hata simu zake zilikuwa hazipatikani. Nilimvumilia sana Mpenzi wangu cheni kwa muda wa miaka miwili lakini hakurudi wala sikuwa na mawasiliano naye yoyoyete, ndipo nikaamua kuolewa na kijana huyu aitwae Ray, ambae ndio mume wangu wa sasa. miaka mitano sasa imepita tangu tupotezane na mpenzi wangu cheni, ndipo nikapata barua hii iliokuwa imeandikwa hivi;
Kwako Mpenzi Vai,
Mimi ni mpenzi wako zamani wa cheni,
Natumaini umzima wa afya, nilishawahi kuja dar mwaka jana nikaambiwa kuwa demu wangu keshaolewa, nilihuzunika sana, nikakosa Furaha kabisa. Jiji la dar nikaliona kama jehanamu, nilikuwa kama kinda la ndege lililotelekezwa na mama yake, kwani nilikuwa mpweke sana, ukizingatia nilishajiwekea malengo ya kuja kukuoa. Bali mihangaiko ya maisha ndio iliyoniweka mbali na wewe malkia wangu, baada ya kukukosa ndipo nikaamua kurudi zangu Uingereza. Ambako kwa sasa nimebadilisha fani nafanya kazi katika kampuni binafsi.
kikubwa kilichonipelekea nikuandikie barua hii ni kwamba nimepata habari kuwa Kutakuwa na Kongamano la Chama cha Lunga na fasihi ya kiswahili ambalo litafanyika chuo kikui cha Iringa mwezi August, Hivyo Mimi kama mdau Wa Kiswahili nitahudhuria kongamano hilo kwa kuwa mwezi huo nitakuwa Tanzania, hivyo nakuomba Fanya uwezavyo tukutane katika kongamano hilo ili nikueleze kilichonipelekea kupoteza mawasiliano na binti mrembo kama wewe.
Ukipata barua hii naomba unijulishe kwa namba zangu za simu zilizopo hapo chini.
Wako akupendae,
. Cheni.
Nilipatwa na mshangao baada ya kusoma ile barua, ghafla nikajiuliza maswali huyu mtu anajua kuwa nimeolewa, sasa he mume wangu akijua itakuwaje? Na mume wangu akiiona hii barua je? Maswali yote hayo sikuyapatia majibu nikabaki kwenye dembwi la mawazo tele.
Niliporudi nyumbani mume wangu alinipokea kwa shamrashamra sanaa, akaniambia nimerudi mapema na nimekuandalia chakula mpenzi, nikamwambia sawa, lakini nikawa nababaika sana hasa alipotaka kunipokea mkoba. Nikamwambia hapana usinipokee. Hata wakati tunakula nilikuwa nababaika sanaa mpaka mume wangu akawa na wasiwasi na mimi. Akaniuliza "uko sawa mke wangu? Najua unawaza safari ya iringa tu, nitakugharamia kila kitu sipendi upate shida hata kidogo, nataka uwe na Furaha sana siku hiyo, wewe ndio mwanamke wa maisha yangu."
Alisema hivyo huku akinyanyuka na kunikumbatia, nikajikuta natabasamu na kuanza kusahau mawazo ya Cheni.
Baada ya kula nikaingia bafuni kuoga, nilipotoka tu nikachukuwa mkoba wangu ili niifiche barua ile nilioandikiwa na mpenzi wangu Cheni, lakini sikuiona. Nilimwaga vitu vyote kitandani lakini sikuiona, nikamuita mume wangu nikamuuliza, akasema hajawahi kusachi mkoba wangu hata siku Moja, na hana tabia hio, akaniuliza hio barua imetoka wapi? Mimi sikumjibu, niloendelea kutafuta mpaka nikachoka, sikuwa na raha hata kidogo, niliwaza sana nimeiacha wapi hio barua, nikampigia simu mtu aende ofisini kwangu akaitizame lakini akaniambia hakuiona. Kijasho chembamba kikawa kinanitiririka nisijue nini chakufanya. Siku hio nililala mzungu wa nne na mume wangu, huku kichwa kikiniuma sana.
Mume wangu hakufurahishwa na hali hio akanifokea sana, akasema, "wewe mwanamke hio barua imetoka wapi? Naomba usinifanye Fala mimi , nieleze ukweli.
Nikamdanganya imetoka kwa rafiki yangu wa kike, haikuwa rahisi kuniamini lakini aliniamini kiasi.
JE NINI KITAENDELEA?