Hadithi mpya ya kusisimuwa uchawi wa mama mkwe

Hadithi mpya ya kusisimuwa uchawi wa mama mkwe

HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE-5

"UNAJUA mume wangu kichwa ambacho kimeniuma asubuhi kilikuwa cha ajabu sana. Nilikuwa nahisi kama kuna mtu ana nyundo ananigonga kichwani, nikajikuta nikilia," nilimdanganya.

"Pole sana, unajua wakati mwingine uwe unajikaza kulialia namna ile kama mwenzako ana presha anaweza kuanguka, ukampoteza."
"Pole sana, sikuwa na nia ya kukushitua ni maumivu tu ya mwili yalinifanya niwe vile."

Kimya kilipita huku wote tukiwa kitandani na baada ya dakika kama kumi na tano hivi nilimsikia mume wangu akikoroma.
Niliinuka kitandani hadi kwenye mlango na kuhakikisha kuwa umefungwa kwa ufunguo. Nilifanya hivyo ili kudhibiti wale waliokuja jana usiku bila taarifa.

Mimi nilichelewa sana kupata usingizi kutokana na kuwaza hili na lile kuhusiana na tabia mbaya ya uchawi ya mama mkwe.
Hata hivyo, usingizi hauna adabu, nilijishitukia nikiwa nimelala fofofo na baada ya hapo sikujua kilichoendelea hadi saa tisa usiku niliposhituka baada ya kuona mtu kanishika kichwani.

Nilipofumbua macho nilimuona mama mkwe akiwa chumbani kwetu akiwa mbele yangu. Nilitamani kupiga yowe lakini nilishindwa. Ni kwamba mwili ulikuwa unataka kufanya hivyo lakini nikawa sina nguvu hata ile ya kujitikisa.

Nilipigwa na butwaa na kujiuliza maswali mengi bila majibu. Huyu mama kaingiaje? Mbona mlango nilikuwa nimefunga kwa funguo?'
Yeye alikuwa akiniangalia huku akiwa ameweka kidole kimoja mdomoni ishara ya kuniambia kuwa nisiseme kitu nibaki nimetulia. Lakini haraka sana nilifumba mambo na akawa ananipigapiga kofi kwenye mashavu yangu ili kuthibitisha kama nimelala kweli usingizi au nilikuwa macho.

Niliamua kujifanya nimelala usingizi ili nione alichotaka kufanya. Alipanda kitandani na akawa anatutambuka mmoja baada ya mwingine. Kati ya mimi na mume wangu, alitutenganisha kwa kuweka nafasi katikati yetu kwa kuwa kitanda chetu kilikuwa kipana sana cha sita kwa sita.

Baadaye alipuliza tunguri yake na mara nje nikasikia upepo mkali ukivuma lakini ukaishia juu ya mabati ya nyumba yetu. Nilikosa amani kabisa. Nilifumba macho kwa nguvu sana kwa sababu mama mkwe alikuwa anashuka kitandani kupitia kichwani kwetu.

Nilimsikia akiimba nyimbo ambazo sikujua maana yake kwa sababu hazikuwa nyimbo za Kiswahili nadhani zilikuwa ni za kijini au kichawi. Kwa kuwa chumbani kulikuwa na mwanga hafifu kutokana na ukweli kwamba nilikuwa nimezima hata ile taa ya mwanga mdogo, sikujua kuwa mama mkwe alikuja chumbani mwetu akiwa na kijimfuko.

Nilikiona hicho kijimfuko baada ya yeye kuchuka chini na kukiinua na akawa anachakuachakua ndani. Alitoa kitu kirefu kama mkia wa taa, sikujua anataka kuufanyia nini na mwanga wa taa za nje ulinisaidia kuona kila alichokuwa akikifanya.
Nilihisi kuwa inawezekana ule siyo mkia wa taa bali ni kamba na hakuna ajabu kama ataamua kuitumia kuninyonga nayo.

Nilikuwa na hofu hiyo kwa sababu aliahidi mchana mara mbili kuwa kama mambo yake ya uchawi nitamjulisha mume wangu ambaye ndiye mwanaye, ataniua na mwili wangu kuufanya nyama ambayo ataila!

Mbaya zaidi ni kwamba sikuwa na uwezo wa kupiga yowe au kutumia nguvu ili asinifunge shingoni na kitu kile kama mkia wa taa. Hata hivyo, tofauti na mawazo yangu, aliinua ule mkia na kunitandika nao makalioni pwaa. Dakika hiyohiyo nikawa nakosa nguvu hata ya kufumbua macho.
Niliyalazimisha kuona nikafanikiwa japokuwa yalikuwa yamefunguka kidogo sana kutokana na kichapo cha mkia ule.

Je, huo ndiyo mwisho wa mama Ajigale? Fuatilia simulizi hii ya kusisimua Kesho.....
 
sawa mkuu sitabiri tena
Kafunguwe Thread yako kisha Utabiri uchaguzi unao kuja nani atakuwa mshindi kati ya Chama cha CCM na vyama vya Upinzani usitabiri hadithi ninayoweka mimi ni upuuzi mtupu unaofanya wewe .Kama wewe ni Dr wa kutabiri katabiri Uchaguzi unaokuja Dr wa ukweli kwa kufuta Utabiri wako nimekusamehe.
 
HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE-6

Niliyalazimisha macho kuona na nikafanikiwa japokuwa yalikuwa yamefunguka kidogo sana kutokana na kichapo cha mkia ule. Niliamini kuwa ule mkia ulikuwa na nguvu ya kumdhoofisha mtu.
Hata hivyo, mume wangu yeye hakumchapa hali iliyonipa wasiwasi zaidi na kujiuliza kwamba au kuna jambo la ziada juu ya bakora niliyochapwa?

Alichukua unga fulani ambao sikujua ni wa nini na kumnyunyizia mume wangu sehemu zake nyeti kisha kuvua bukta yake ambayo alikuwa akiitumia kulalia.
Aliniinua mimi na kuniweka chini ya kapeti mlemle kwenye chumba chetu cha kulala.
Je, nini kiliendelea?

SONGA NAYO HAPA.


Nilikuwa natamani kupiga yowe lakini mdomo ulikuwa haufunguki na nilikuwa najaribu kujiinua pia nikawa nashindwa kufanya hivyo.
Baada ya sekunde kama kumi hivi nilimuona mama mkwe akipuliza vitu, sikujua ni vitu gani lakini nilihisi alikuwa akifanya vile ili kutufanya mimi na mume wangu tuzidi kupoteza fahamu kwa sababu yeye alikuwa amefunika pua kwa kitambaa cheusi.
Hata hivyo, baada ya dakika mbili mama mkwe alikaa kitandani akawa anasema maneno ambayo sikuyaelewa maana yake kwa sababu hayakuwa ya Kiswahili wala lugha yao.

Nilishitukia chumba kinakuwa na mwanga kama vile amewasha taa ya umeme. Akili yangu ilikuwa sawasawa tatizo lilikuwa nguvu za kuzungumza nilikuwa sina.
Baada ya mwanga kuwepo mle chumbani nilishuhudia mlango ukifunguka na kundi la wachawi wakaingia chumbani, wote walikuwa wamevaa kaniki (nguo nyeusi).

Sikuweza kuwahesabu kutokana na woga. Lakini mara baada ya kuingia ndani ya chumba chetu walianza kucheza ngoma ya kichawi huku wakiimba polepole sana.

Walimbeba mume wangu na kumshusha kwenye kitanda, akavaa bukta yake wakatoka naye nje akiwa hajitambui.
Sikujua huko nje walikwenda kumfanya nini lakini walichukua muda mrefu kurudi. Wakati wachawi hao wanaondoka, mbele yao alikuwa ni mkwe wangu aliyekuwa na usinga (mkia wa mnyama nyumbu au twiga na kukaushwa).
Alikuwa akiupunga mkia huo huku wachawi wenzake wakipiga manyanga ( kifaa kilichotiwa kokoto au mbegu ambacho hutumika kama ala ya muziki kwa kuwa kinatoa sauti).

Kwa kuwa nilikuwa nimefumba macho na kuangalia kwa chati sana, nilijaribu kuyafungua lakini nikagundua kuwa mle ndani alikuwepo mchawi mmoja aliyeachwa amekaa kitandani.
Nilihisi kuwa yule alikaa kunilinda mimi ili kuhakikisha kuwa siamki na kukuta mume wangu hayupo kitandani kwetu.

Lakini mchawi yule siyo kwamba aliacha anakula raha tu, hapana kuna manuizo alikuwa akiyafanya huku akifukiza uvumba kwenye chombo alichokuja nacho.
Ajabu ni kuwa chombo kile alikiweka juu ya kitanda chetu, shuka zilikuwa haziungui lakini moshi ulikuwa ukifuka chumba kizima.

Nilielewa kuwa alikuwa anakifukiza kwa ajili ya mimi niliyekuwepo kwa sababu wakati anafanya hivyo alikuwa akilitaja jina langu mara kwa mara kwamba nisizinduke.
"Moshi eneo ndani ya chumba hiki na mfanye Mei au mama Ajigale asizinduke," alikuwa akisema hivyo na kukifunika chombo kile kwa kiganja kisha anapofunua moshi mwingi kutoka na kujaza chumba.

Alikuwa akiinama mara kwa mara na kunikagua kuona kama nilikuwa nina uwezo wa kufumbua macho au la, kila aliponiita nilifumba macho.

Kuna wakati alichukua mkono wake mmoja na mwingine akashika sura yangu kisha kufungua jicho langu moja, nami nilijilegeza.
"Duh jicho jeupeee kama aliyekufa," alisema polepole nami sikumuuliza alikuwa na maana gani.
Baadaye alichukua mafuta ambayo sijui ni ya nini na kunipaka kwenye paji la uso huku akisema maneno ambayo sikuyaelewa maana yake.

Alijaribu kuinua mguu mmoja akauachia ukapiga juu ya zulia na akafanya hivyo kwa mguu wa pili. Nilijifanya sijui chochote kwani nilijua kama angegundua nilikuwa namuona angewaambia wenzake kisha ningeuawa na kuliwa chama yangu kama mama mkwe alivyonitishia zaidi ya mara mbili nikiwa na akili timamu.
Mchawi yule baadaye aliamua kujilaza kitandani kwetu huku akiendelea kuimba wimbo wake wa kichawichawi lakini akaacha kufukiza ule moshi.

Je, kilifuatia nini? Usikose Kesho.....Usikonde tu....
 
HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE-7

LIPOISHIA
Baada ya dakika kama kumi hivi mimi nikiwa bado chini nimelala kwenye kapeti, mchawi yule nilimsikia akikoroma.
Nilishangaa sana mchawi kuja kwenye chumba cha watu na kuanza kukoroma kama vile alikuwa kwake. Mawazo yangu yakaenda kwa mume wangu kwamba amepelekwa wapi?
SONGA NAYO


Nilijaribu kuinuka pale nilipokuwa nimelazwa, nikashindwa. Na yule mchawi aliyeachwa anilinde akawa anaendelea kukoroma juu ya kitanda chetu.]
Dakika kumi baadaye nilisikia kishindo nje ya nyumba. Nilijua kuwa lile kundi la wachawi walioondoka na mama mkwe wangu lilikuwa linarudi.
Moyo ulinienda mbio mithili ya mtu aliyemaliza kukimbia mbio fupi za mita mia moja. Niliona mlango wa chumba chetu ukifunguliwa.
Niliminya macho kujifanya nimelala fofofo.

Lakini niliyaachia kidogo ili kuona kama mume wangu amerudishwa au amekwenda kuliwa nyama na wachawi wale.
Nilifarijika baada ya kuona kundi lile la watu hao wabaya wakiwa wamembeba kama walivyokuwa wameondoka naye.
Walipomfikisha kitandani walishangaa kukuta mwenzao waliyemuacha akikoroma.
"Huyu mjinga kweli kweli. Tulimuacha amlinde mke wa baba Ajigale yeye akaamua kulala," alisema mama mkwe wangu.
"Muamshe. Muamshe kwa kumchapa na mkia wa taa," aliamuru mtu ambaye sikumjua kwa jina.
Mchawi mwingine alichukua mkia wa taa na kumchapa yule mchawi aliyekuwa akikoroma kwenye kitanda chetu. Hakushituka na wote mle ndani wakashituka.
"Huyu inawezekana alikuwa akimfukizia moshi huyu mke wa baba Ajigale ili asizinduke na matokeo yake naye fukizo limemkolea." "Ni kweli kabisa. Lete ugoro," alisema yule kiongozi wa wachawi.
Nilisikia kifuniko kikifunguliwa na baadaye alinusishwa yule mchawi aliyekuwa akikoroma.
"Chaa, chaa, chaa," alipiga chafya.

Baadaye aliketi kitandani na kuulizwa kulikoni alilala kitandani wakati aliachiwa kazi ya kunilinda!
"Huyu mama Ajigale alitaka kuzinduka. Nikaamua kuchukua dawa ya mafusho nikawa namfukizia moshi. Nilisahahu kujifunga kitambaa chenye dawa ya kuzuia mimi kuleweshwa, nikalewa.
Ndivyo ilivyokuwa," alijitetea.
"Lakini huyu mama Ajigale hakujua lolote?"
"Hakujua, nilipoona anajitingisha tu, nikamuwahi na mafusho."
"Umefanya kazi nzuri," alisifiwa.

Baadaye walimtoa pale kitandani na kumlaza mume wangu. Baada ya hapo walininyanyua pale chini ya zulia jekundu chumbani kwetu na kunilaza kando ya mume wangu.
Sikuthubutu kuonesha kuwa najitambua badala yake nilijitahidi kujilegeza kana kwamba nilipoteza fahamu kabisa.
"Isije ikawa ule moshi wa mafusho ulizidi. Tunaweza kumuacha akapata fahamu kesho saa tisa mchana, tutakuwa tumefanya kitu kibaya sana," mmoja wa wachawi alishauri.
Yule mkubwa wao akasema ni vema na mimi ninusishwe ugoro na kazi hiyo akapewa mama mkwe wangu kwa kuwa analala nyumba hiyo hiyo tofauti ni vyumba tu.
Walikubaliana. Kilifunguliwa kichupa chenye ugoro na kupewa mama mkwe.
"Sisi tunatoka. Utamnusisha mkweo baadaye na akianza kupiga chafya tu, toka atazinduka kivyake vyake," alisema yule mtu ambaye mimi namuita ni kiongozi wa wachawi.
"Sawa," akaitikia mama mkwe.
Giza nene lilitanda na baadaye mwanga ukaja kwa mbali na nikamuona mama mkwe akininusisha ule ugoro. Nilitamani nikatae lakini nguvu zilikuwa zimeniishia kabisa nikawa nashindwa kunyanyua mkono ili kupokea ule ugoro.
Alininusisha nikaanza kupiga chafya, haraka sana mama mkwe akakimbia kuelekea chumbani kwake.
Nilijaribu kuinua mkono, ukainuka, nikajaribu kuketi pale kitandani, nikafanikiwa. Niligeuza shingo kumuangalia mume wangu na hasa nilimuangalia kifuani kama bado alipumua au walimleta pale akiwa maiti.
Niligundua kuwa bado anapumua kwa sababu kifua chake kilikuwa kikitanuka na kushuka alipokuwa anavuta hewa.
"Baba Ajigale, baba Ajigale," nilimuita lakini hakuitika.
Niliwaza kwamba nimuendee mama mkwe nikamshurutishe aje amzindue?

Je, atapata fahamu au mpaka waje wale wachawi? Fuatilia kesho tena.....
 
Lengo yakuleta hii hadithi hapa jamvini ni nini? Yani hapa tumeanza kuandikiana hadithi kweli? Nikama tupo shule ya msingi au secondary. Mtumie Shigongo aiweke kwenye magazeti ya udaku.
 
Lengo yakuleta hii hadithi hapa jamvini ni nini? Yani hapa tumeanza kuandikiana hadithi kweli? Nikama tupo shule ya msingi au secondary. Mtumie Shigongo aiweke kwenye magazeti ya udaku.

Wenzako tuna enjoy we kama unakereka usisome
 
Mbona ya kusisimua ya zaman hujamaliza umeanza mpya jaman mzizi mkavu malizia basi ile ya andendekisye
 
MziziMkavu
, basi kesho iwe kesho kweli sio uingie mitini.
Kwa sisi wazee inatukumbusha yale ya Ganzel na gazeti la Taifa!
 
Lengo yakuleta hii hadithi hapa jamvini ni nini? Yani hapa tumeanza kuandikiana hadithi kweli? Nikama tupo shule ya msingi au secondary. Mtumie Shigongo aiweke kwenye magazeti ya udaku.
Mteja mzuri ni yule anaejuwa kipi hakitaki na akaacha kununuwa lakini hawi na mgogoro na wanachonunua wenzake!
 
Mbalu, hadithi pelekeni kwa magazeti ya udaku kwa shigongo. Hapa letini mambo ya watu wazima. Naona sasa jamvi lina vamiwa tu.
 
Hadithi, nikitu an realistic kabisa, leteni issues tujenge taifa, tupo nyuma kimaendeleo, hatuhitaji hadithi tena, twa hita objective ideas bwana.
 
Hadithi, nikitu an realistic kabisa, leteni issues tujenge taifa, tupo nyuma kimaendeleo, hatuhitaji hadithi tena, twa hita objective ideas bwana.

Sema wewe ni mvivu kusoma hadithi au sio hoby yako ingekuwa cd ya bongo muv hpo kcheko tu
hujui km watu wanapata mkate wa kila siku kwa ajili ya utunzi wa hadithi
huoni mtu ana jiajiri mwenyewe kwa kutumia kipaji chake tusiwabeze kihivyo hz ndyo sanaa zenyewe na ndyo ajira zenyewe


Jamii isiyo tumia sanaa daima ita ishi ktk Mawazo yaliyo dumaa
 
Mng'ongo, naona hunielewi nawe, kuna sehemu au mahala ya kila kitu. Ndio maana kuna magazeti yenye habari nzito nzito, watu ambao ni wavivu kufikiri hawanunui hao magazeti, kwa sababu yanalenga watu wenye upeo mkubwa, walisha so hadithi huko nyuma, na sasa ni wakati mambo mazito. Mtu mwe uwezo mdogo naye yapoagazeti yake kama ya shigongo hapo ndipo unapopata wavivu. Huwezi kuimiza kichwa vile kwasababu ni habari nyepesinyepesi. Na watanzania wengi na hadithi zao, wajenga tabia ya uongo uongo, na hawachukuli mambo mazito serious, wamezoea hadithi njo. Kwahio kuna social network zingine naona zina ingiliwa kama hapa jf. Lengo la hapa nikupea, kuchanganua, kuelimishana na kunga hoja ambazo zina mtazamo wakitaifa. Let's review our contents.
 
Sina muda na bongo moves, am looking at real issues za jamii na taifa kwa ujumla. Watu sehemu fulani wanakosa maji, huduma muhimu, waleta hadithi tena. Shule hovyo sehemu nyingi za nchi, leta hio mada. Vyuo vinatoa elimu duni, leta hoja tuwaambie wabadilike. Sio hadithi tena.
 
HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE-8

ILIPOISHIA
Mara tu baada ya kumnusisha alipiga chafya mara tano au sita. Nilishukuru kwa kitendo kile maana nilikuwa nimeanza kuchanganyikiwa.
"Baba Ajigale, baba Ajigale, baba Ajigale," nilimuita, lakini hakuweza kuitikia.
Niliwaza kwamba nimuendee mama mkwe nikamshurutishe aje amzindue?
Songa nayo


Nilipata akili haraka sana kwamba nikifanya hivyo mama mkwe atagundua kuwa nilikuwa naona kila kitu ambacho walikuwa wakikifanya na wachawi wenzake.
Akili ikaniambia nizidi kumnusisha ugoro uliokuwa juu ya godoro japokuwa ulikuwa ‘kiduchu' lakini nilijitahidi kuokoteza.
Baada ya kazi hiyo nilimnusisha tena akapiga chafya na kufumbua macho. Nilimuita, "Baba Ajigale." Akawa ananitazama bila kusema chochote.
Nilifungua mlango na kwenda jikoni kwenye friji, nilichukua soda na kurudi chumbani kwetu, wakati narudi mama mkwe naye akawa karibu kabisa na mlango wa chumba chetu.
Alikunja vidole vya mkono wake na kuachia kimoja akawa ananipa ishara kuwa nifunge mdomo wangu.
Nami sikumchelewesha nikamuambia kwa kunong'ona kuwa nimemnusisha ugoro nitamuambia kuwa umenipa wewe. Nikazama chumbani.
Nilipoingia chumbani, nilimuinua na kumketisha mume wangu kisha nikaanza kumnywesha ile soda.
Alikunywa kana kwamba alikuwa ametembea kwenye jua kali sana na alikuwa na kiu. Nilichukua shuka na kumfutafuta pua ambayo ilikuwa na chembechembe za ugoro. Alipiga chafya tena.
"Najisikia mchovu sana, kwani nilikuwa nafanya nini mpaka ukaamua kuninywesha soda?" aliuliza.
"Nimekuona unakosa nguvu, kila nikikuita huitiki , nikahisi kuwa inawezekana una sukari kidogo mwilini," nilimdanganya.
"Sawa, lakini mbona kuna harufu ya ugoro puani kwangu, kulikoni."
Kabla sijajibu swali hilo moyo ulipiga paa kwa sababu niliona nikimtajia sababu na aliyeleta ugoro kuwa ni mama yake na wachawi wenzake itakuwa balaa.
Nilifikiri sana, lakini sikupata jibu la haraka.
"Mbona hunijibu, imekuwaje kuna ugoro na kwa nini nimenusishwa?"
Nilijua kuwa mama mkwe kutokana na tabia yake ya ‘kubana' nyuma ya mlango wetu alikuwa anasikiliza mazungumzo yetu, hivyo nilipaza sauti ili asikie kule alipo:
"Ugoro nilikwenda kumuomba mama mkwe ambaye alinipa nikunusishe, alisema mtu akikosa nguvu akinusa ugoro anapiga chafya, kitendo ambacho kinachangamsha mapafu na kuyafanya yafanye kazi sawasawa, hivyo mtu kupata nguvu,"nilisema huku nikionesha kutokuwa na wasiwasi na maelezo yangu.
"Hebu nenda kaniletee maziwa yangu kwenye friji, au umekunywa?"
"Hapana, bado yapo."
"Hebu nenda kaniletee."
"Sawa."
Ile nafungua mlango tu, nikakutana na mama mkwe akiwa pembeni ya mlango. Akanong'ona, "Gonga."Alisema neno hilo huku akitoa tabasamu pana lililomuonesha mapengo yake ya meno ya mbele.
Nilitamani nicheke na hasira zote zilinitoka kutokana na mama mkwe huyo kunipa mkono wake na kunitaka nigonge kufurahishwa na nilivyomdanganya mume wangu.
Nilikwenda kwenye friji na kuchukua maziwa fresh yaliyokuwa yamekuwa baridi sana. Nilidhani ameondoka pale karibu na mlango wa chumbani kwetu.
Ajabu ni kwamba bado alikuwa amesimama palepale huku akitabasamu utafikiri alikuwa juha.

***
Kulikuwa kumepambazuka na majogoo yalikuwa yanawika kuashiria kuwa jua lipo mbioni kuchomoza. Niliinuka na kwenda bafuni kujisaidia na nilipotoka huko nilikwenda moja kwa moja kwenye meza ya chakula kumuandalia kifungua kinywa mume wangu kabla hajaenda kazini.
Naye alikwenda kuoga na akaingia chumbani kwetu. Mama mkwe hakuwa ameamka bila shaka kutokana na kazi nyingi za kichawi za usiku alizokuwa amezifanya.
Mume wangu alifika mezani na kukuta chai ipo tayari pamoja na mayai ya kuchemsha mawili na kipande cha mkate mweusi ambao anapenda kula.


Itaendelea Kesho..............
 
Mzizi endelea basi, huyu mama mkwe nae mbona atamfanya mkamwana wake awe mchawi kama yeye.
 
Back
Top Bottom