Si kosa lako, nimeshakusamehe
Ahsante sana ndugu sitarudia tena rugha hiyo mkuu.
Si kosa lako, nimeshakusamehe
HADITHI
YA KUSISIMUWA UCHAWI
WA
MAMA MKWE-25
[FONT=Century
Gothic]ILIPOISHIA
Kwa upande wa tulipoketi akina mama mengi yalizungumzwa, wengine
wakiwa na hamu ya kuona maiti ya mama mkwe kwa kuamini kuwa atakuwa
siye.[/FONT]
Wewe wachawi unawajua? Huyo kajibadili tu, mwenyewe atakuwa katoweka na
utasikia yupo sehemu fulani, alisikika akisema mama mmoja ambaye
sikuwa namjua kabisa.
Si umesikia yaliyotokea huko polisi? aliuliza mama mwingine aliyekuwa
amejitanda ushungi.
Sijasikia,
Hujasikia kuwa yule
mwanaume aliyenasa ile nyumba ya jirani polisi hawakumkuta mahabusu
asubuhi?
Acha wewe!Inasemekena alifungiwa lokapu lakini asubuhi wakakuta
hakuna mtu. Waliangalia mlango wao wa chuma, ulikuwa umefungwa na nondo
kwenye madirisha zilikuwa nzimaaa.
Duh, ikawaje?
Ikawaje? Unauliza sharubu
kwa Osama, polisi wote waliokuwa zamu usiku wamewekwa ndani.
Hee! Kwa nini?Eti wakubwa wao wanadhani wamemtorosha.
Hawana akili hao wakubwa. Wamtoroshe kisha wapoteze kazi,
kisa?
Hayo unajua wewe.
Hawajiulizi kwa nini alikutwa ndani kwenye nyumba ya watu wakati hakuna
mlango wala dirisha lililobomolewa?
Unajua wakubwa serikalini
wanajifanya hawaamini uchawi lakini wao ndiyo waumini wa uchawi
kwelikweli, kila siku wanakwenda kwa waganga wa kienyeji kutafuta
kupandishwa vyeo.
Una uhakika?
Husomi magazeti au
kusikiliza vyombo vya habari? Siyo baadhi ya vigogo tu, hata viongozi wa
makampuni makubwa, baadhi yao hawakosi kwa waganga hao.
Sasa huyo mchawi wanaweza kumpata kweli?
Itakuwa kazi kubwa. Baada ya kutoka rumande atakuwa amehama mji huyo,
lakini serikali ina mikono mirefu, wanaweza kumtia
mbaroni.
Lakini huyu ni kiboko. Hiyo
dawa wakiipata majambazi tutakwisha wote. Maana wanaweza kuingia benki
wakazoa fedha zote wakakimbia nazo.
Kweli, lakini nilisikia mtu mmoja akisimulia kwamba masharti yao ni
magumu wakiingia ndani ya nyumba kimiujiza.
Hukuambiwa masharti hayo
ili nasi tuelewe?
Niliambiwa kwamba wanapoingia kwenye nyumba, sharti lao ni kwamba, kwa
kuwa wanaingia kupitia ukutani, si ruhusa kutoka ndani hata na sindano,
ndiyo maana hawaibi benki.
Kwa sharti hilo hata mimi
naamini kuwa ndiyo maana wachawi hawaibi benki.
Mazungumzo ya wanawake wale yalikatizwa na tangazo la MC aliyesema
kwamba mwili wa marehemu mama mkwe umeshafika pale
nyumbani.
Wanaume walibeba jeneza
lenye mwili na kuliweka ndani. Kusema kweli waombolezaji walikuwa
wachache. Walimlaani mama mkwe kutokana na mpango wake wa kutaka kumroga
mume wangu yaani mwanaye.
Hakukuwa na ucheleweshaji,
marehemu alipelekwa makaburini na alizikwa na watu wachache sana, wengi
walichukizwa kwa tabia yake ya uchawi.
Mwisho.
Nakushukuru wasomaji wangu kwa kufuatilia simulizi hii
asanteni.
Hiko vizuri sana lkn ilivyoisha sijaelewaasante ila sizani kama imeisha kwa sababu najua hajafa na anaweza kuwa anakutokea na mambo mengine utujuze basi