Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,104
- 34,921
HADITHI YA KUSISIMUWA UCHAWI WA MAMA MKWE
HAIKUWA rahisi kwa mume wangu kuamini kuwa mama yake ni mchawi tena ana uchawi wa kutisha. Ni mwanamke ambaye alikuwa akiwanga usiku kila chumba katika nyumba yetu iliyokuwa Metropol jijini Arusha.Nilikuwa naogopa kumuambia mume wangu kuhusu uchawi wa mama mkwe na tabia yake ya kutusotea usiku tukiwa tumelala.
Siku moja alikuja chumbani kwangu na kunishusha chini akidhani kuwa amenipumbaza kwa dawa zake alizomwaga lakini nilikuwa na akili timamu. Nilichukia sana baada ya kuona anataka kumfanyia kitu mbaya mume wangu ambaye ni mwanaye wa kumzaa.
Baada ya kunishusha juu ya kitanda na kunilaza kwenye zulia chumbani kwetu, mama mkwe alianza kumtambuka mume wangu akiwa kitandani, kisha kumvua bukta yake. Nilijisemea, Nijifanye nimezinduka?
Kutokana na kumuangalia mama mkwe wangu alivyokuwa akimfanyia mume wangu, moyo wangu ulikuwa ukidunda kama vile nimetoka kufanya pushap hamsini dakika chache.
Japoku kulikuwa na giza lakini mwanga wa taa za ulinzi, zilizokuwa zikiwaka nje, ziliniwezesha nione kila kitu alichokifanya mama mkwe dhidi ya mume wangu.
Je, mama huyo ni nani na anafanya nini? Msimualiaji pia ni nani na ametoka wapi? Pata majibu hayo itaendelea.