Hadithi: Mikataba ya kishetani

Hadithi: Mikataba ya kishetani

11

Hali ya hewa nyepesi, iliyoambatana na jua angalau likichomoza upande wa mashariki, iliashiria siku nyingine tulivu yenye neema machoni mwa Joram. Lakini hakuwa hivyo moyoni mwake.

Japo ni kweli kuwa alilala kwa amani na kuamka bila ya kusikia taarifa yoyote dhidi yake kupitia vyombo vya habari au watu wake katika vyombo vya usalama bado alikuwa na hakika kabisa kuwa utulivu huo ulikuwa wa bandia. Hivyo, hakukubali hali hiyo imlaghai.

Alikuwa amelala kwa saa tatu tu, kichwa chake alikiona kizito, kikimshawishi kuendelea kulala. Hakuafikiana nacho. Alikuwa na mengi ya kufanya. Alioga chapchap, akavaa chapchap. Bastola yake aliichomeka katika soksi ya kulia kwenye mguu wake, kisu kushoto; vifaa vyake vingine nyeti alivifungia katika begi lake kabla hajafunga mlango wake na kuondoka na funguo.

Alitembea taratibu hadi alipoifikia baa moja chakavu, yenye jina maarufu, Lango la jiji, ambamo aliingia na kuagiza supu ya ng’ombe, aliketi kiti cha kona moja iliyokuwa tupu, akatoa simu yake na kuanza mawasiliano. Alianza kwa kupiga namba ya yule mtumishi wa hoteli ya Holiday Inn. Hakujua Chaku alitarajia nini toka kwake, lakini kama mpelelezi aliamini kuwa Chaku alikuwa na hisia fulani kwake. Simu ilikuwa imefungwa. Aliipiga mara tatu bila mafanikio. Akaitazama saa yake. Muda ulikuwa umemruhusu kupitia hotelini hapo kabla ya kuendelea na mikakati yake mingine.

Alikula supu na chapati mbili, akaishushia kwa chupa ya Coca Cola. Dakika chache baadaye alikuwa ndani ya teksi akielekea mjini. Muda mwingi akiwa ameifunika sura yake kwa kofia pana, miwani ya jua usoni, aliamini si dereva wala watu aliokuwa nao baa hiyo wangeweza kumtambua kwa urahisi. Alishuka mtaa mmoja kabla ya kuifika hoteli. Akatembea kwa mguu hadi hotelini ambako alifikia mapokezi na kumuulizia Tenga Mfaume.

Wavulana wawili na msichana mmoja walikuwa mapokezi hapo wakishughulikia wageni wanaoingia na wanaotoka. Yule msichana alishtuka mara jina la Mfaume lilipotajwa. Hata hivyo, mshtuko huo ulidumu katika uso wake kwa nusu dakika tu, nusu ya pili alikwisha jikarabati na kuzama katika shughuli zake kana kwamba hakuwa amemsikia Joram. Lakini haikuwa kabla ya Joram kuusoma mshtuko huo. Akamshuku kuwepo kwa jambo kati yake na Mfaume.

“Kwani wewe ni nani kwake?” mvulana mmoja alimuuliza Joram.

Kati ya vitu ambavyo Joram Kiango alikuwa amefanya usiku huo ni pamoja na kutengeneza nyaraka na vitambulisho vya bandia. Alitoa kimojawapo cha vitambulisho hivyo na kumwonyesha mtu wa mapokezi, “Naitwa Paul Mahiri, Inspekta msaidizi wa jeshi la polisi. Tuna shida ndogo tu ya kuzungumza na bwana Mfaume.”

Wote pale mapokezi walionyesha kushtuka. “Hajaonekana toka jana mchana. Aliondoka bila kuaga na simu yake imefungwa,” msemaji wa kwanza alieleza.

“Anaishi wapi? Joram aliuliza.

“Hakuna mwenye uhakika, mara anasema anaishi Osterbay, mara amejenga Tegeta. Ni mtu wa kupenda mzaha.”

Joram alilitafakari hilo kwa muda. Kisha aliomba kuzungumza na yule msichana ambaye sasa alikuwa akiyafuatilia mahojiano hayo kwa makini zaidi. “Tafadhali tuzungumze faragha kwa dakika tano tu dada yangu.”

Msichana huyo alisita. Hata hivyo, mmoja wa watumishi wenzake alimwashiria kukubali. Akamwongoza Joram katika chumba cha baa ambacho isipokuwa kwa mtu mmoja aliyekuwa akifuta meza na viti, kilikua kitupu.

“Unaitwa nani binti?” Joram alihoji pindi wakiketi.

“Mariam”

“Mariam nani?”

“Mariam Maftaha”

“Unaishi wapi?”

“Temeke.”

Joram alicheka kimoyomoyo. Haya hayakuwa maswali yake, yalikuwa maswali ya kipolisi, yeye hakupata kuwa polisi. Aliyatumia ili kumtia Imani msichana huyo kuwa anazungumza na polisi. Hata hivyo, Joram alihisi yakimchosha haraka mwenyeji wake kama yalivyomkinaisha yeye mwenyewe. Akabadili mwelekeo.

“Dada Mariam, nina mashaka Mfaume ni mchumba wako,” alimwambia.

“Mariam alicheka kabla hajajibu, “Sio kweli, nimeolewa huu mwaka wa tatu.”

“Alaa! Mbona mapema?”

“Dunia hii ya maradhi na vifo visivotabirika, ukiolewa mapema unamshukuru Mungu.”

Joram aliafikiana naye. “Na Mfaume ameoa?” aliuliza.

“Hakuna mwenye uhakika. Mara aseme ana mke wa kiarabu, mara mchumba wa kihindi. Ni mtu mcheshi wakati wote.”

“Unadhani kwanini ametoweka? Ameiba au kuibiwa na mke wa mtu?”

Joram alitegemea kauli hiyo ingemchekesha Mariam, kinyume chake ilimfanya abadilike sura kabla ya kusema taratibu, “Ametoweka kimiujiza.”

“Kwa vipi?” ilikuwa zamu ya Joram kushangaa. Mariam alimkazia Joram macho kama anayepima uadilifu wake. Kwa namna ya mtu aliyeridhika na alichokiona, alisema taratibu, “Liwalo na liwe, natumaini utanilinda.”

“Nitakulinda, jisikie huru kuniambia chochote kitakachotuwezesha kukutana naye. Tunahitaji sana msaada wako,” Joram alimhimiza. Mariam alisita kidogo tu, kabla hajasema, “Mimi ni mtu wa mwisho kumtia machoni. Nahisi kuwa nimehusika na kutoweka kwake.”

“Kwa vipi?”

Muda mfupi baadaye Joram alikuwa na hadithi kamili. Toka Mfaume alivyokuwa akimfuatilia mgeni mmoja wa kike ambaye pia toka jana hajaonekana, toka alivyoomba kadi ya akiba ya chumba hicho, alivyokwenda chumbani humo na kutosikika tena. Joram alisisimkwa na damu. Baada ya kuhoji mawili matatu juu ya msichana huyo alimshawishi hadi akachukua kadi nyingine ya akiba na kufuatana na Joram chumbani humo. Waligonga mara tatu kabla ya kujiaminisha kuwa chumba hakikuwa na mtu. Wakafungua na kuingia ndani.

Chumba kilikuwa kitupu na kimya, isipokuwa kwa kiyoyozi ukutani. Kitanda kilitandikwa vyema, kana kwamba hakikupata kutumiwa siku nzima ya jana. Joram alitazama hapa na pale. Hakujua anachokitafuta lakini hisia zilimfanya ajisikie amani katika chumba hicho. Alifunua mito, aliinua godoro na kuchungulia chini ya viti na kitanda. Hakupata kitu chochote kilichomvutia. Alifungua kasha la takataka, miswaki iliyotumika na kitana kilichonukia harufu ya mafuta ya nywele za kike vilikuwa humo. Akavirejesha na kuvirudishia mfuniko. Akaliendea jokofu kubwa chumbani humo na kulifungua.

Pamoja na ushujaa wake, pamoja na kukutana na mambo mengi ya kutisha, hilo Joram hakuwa amelitegemea. Alishtuka na kuduwaa kwa muda kabla hajakumbuka kufunga mlango wa jokofu ili Mariam asiweze kuona. Alikuwa amechelewa sana. Mariam aliona vizuri sana mwili wa Mfaume ukiwa umeketishwa ndani ya jokofu hilo, kichwa chake kikiwa kimeangukia upande katika hali ya kuvunjika shingo.

Ukelele wa hofu ulimtoka Mariam, huku akigeuka kutaka kukimbia. Joram alimwahi kwa kumshika na kumziba mdomo. Kwa sauti ndogo alimnong’oneza, “Jikaze. Halafu sahau kuwa unazungumza na Inspekta msaidizi wa polisi. Umenielewa?”

Mariam alikubali kwa kichwa.

“Haya, sasa nieleze kwa kituo bila haraka, alivyokuwa mpangaji huyu; mwenendo wake, kauli zake na kila unachokumbuka. Nieleze pia hisia zako juu yake, sawa?”

***

Dkt. Twalib Khalfan alichoshwa kitambo na maswali ya wapelelezi wa jeshi la polisi na wale waliojiita usalama wa Taifa. Aidha, alichoshwa zaidi na maswali ya waandishi wa habari ambao walianza kumiminika kwake kwa makundi kana kwamba tafrija, kati yao wakiwemo wale ambao hawakupata kuuliza swali la maana zaidi ya yaleyale ambayo amekwishayajibu zaidi ya mara mia moja na yamekwisha ulizwa mara kadhaa. Na waliporudi katika vyumba vya habari, walichoandika walifahamu wao na wahariri wao. Wako walioandika kichwa cha habari pekee na kujaza chumvi isiyolika katika habari zao za kuokoteza. Wako ambao wao wenyewe hawakujua kama ni waandishi wa habari kwa jinsi walivyoamua kutunga habari juu ya habari na kuzichapisha bila uoga. Mradi mkasa uliompata wao waliuchukulia kama ngekewa, au mradi wa kujipatia vijisenti kwa matumizi yao. “Au ndio wanaitwa makanjaja hawa?” Khalfan alipata kujiuliza mara kadhaa.

Kwaajili ya kuepuka kero hizo alikuwa amebadili namba zake zote za simu na kuwapa walinzi wake amri ya kutomruhusu mtu yeyote yule kuingia katika nyumba yake bila kauli yake, amri ambayo Joram Kiango aliikuta ikitekelezwa kwa umakini mkubwa. Hata hivyo, ilimchukua dakika mbili kumshawishi mlinzi huyo kumuunganisha na tajiri wake na tatu kumlainisha tajiri huyo hata akamruhusu aingie. Sasa waliketi kwenye makochi, Joram akinywa kahawa, Khalfan akinywa chai kwa mayai.

“Naijua nchi yetu… nayajua mambo haya. Polisi katika jitihada zao kumpata mhalifu hufikia hatua ya mhanga kujiona kama mtuhumiwa kwa maswali yao mengi. Waandishi wa habari vivyo hivyo. Wengi wao, kwaajili ya njaa zao wamepoteza hekima na utu wa kujua kuwa wanazungumza na mfiwa ambaye anahitaji faraja badala ya kero.”

Khalfan aliafikiana naye kwa kutikisa kichwa. Jina la Joram Kiango halikuwa geni masikioni na machoni mwake. Alisoma mengi na kusikia mengi juu yake. Ni hayo yaliyofanya akubali kukutana naye pale alipojitambulisha kwa mlinzi na kwake, ili kukidhi shahuku yake ya kuonana. Khalfan aliamini kile alichopata kusoma juu ya wajihi wa mtu huyu. Alikuwa mtu wa kawaida, ingawa alivuta macho kwa urefu wake, ukakamavu wake na sura tulivu iliyojaa hekima. Sauti yake pia ilikuwa ya kawaida. Ilimtofautisha vilivyo na kile ambacho alikitarajia cha kukutana na binadamu wa ajabu, binadamu wa ziada, ambaye hata kuzungumza naye ilikuwa kazi mpya.

“Picha zinazotolewa magazetini zinafanana sana na wewe. Tatizo ni ile miujiza. Si binadamu wa kawaida anayeweza kuhatarisha maisha yake kama unavyofanya wewe na akapona kimiujiza kama wewe unayeishi, ungeishi kabla ya kuzaliwa yesu kristu, bila shaka jina lako lingeingia katika orodha ya miungu kama akina Zeus wa Wagiriki au Susanoo wa Wajapan.”

Joram alikatiza kwa kicheko.

“Usiamini kila kinachoandikwa juu yangu,” alimweleza baada ya kicheko hicho. ‘Mie ni binadamu wa kawaida sana. Suala lakujitoa mhanga liko ndani ya damu ya kila mmoja wetu. Tatizo ni viwango katka msukumo wa kuafikiana na wito huo. Watu kama Kenyatta, Mandela, Nkurumah na wengineo walikuwa na hulka hiyo. Bila ya wao kuwa na msukumo ule wa kujitoa mhanga pengine historia ya Afrika ingekuwa ya kusikitisha zaidi. Bila akina Martin Luther King kujitoa mhanga Mmarekani Mweusi wa leo asingekuwa huyu wa leo.

“Una haki ya kuingia katika orodha yao.” Khalfan alisisitiza.

“Sidhani. Naamini kila mmoja wetu ana haki na wajibu huo. Na kila mmoja anafanya hivyo katika nafasi yake. Tatizo ni kiwango na msukumo, pamoja na hulka za binadamu. Siku zote kuna wajenzi na wabomoaji, watafutaji na walaji. Ndivyo tulivyoumbwa.”

Walizungumza mengi. Bila ya Khalfan kutegemea walijikuta wakizungumza mambo ambayo hawakutarajia kuyazungumza. Undani wa mapenzi baina yake na Cleopatra, kasoro ndogo ya mapenzi yao kwa kutokujali watoto, muda wa kuwa pamoja ulivyokuwa mdogo kutokana na kazi nyingi za marehemu na safari za mara kwa mara baina yao na kadhalika. Walizungumzia familia zao, shule zao na marafiki zao.

Joram hakutumia kalamu wala karatasi kunukuu maongezi yao. Lakini aliutumia ubongo wake kunukuu kila kauli aliyoichukulia kuwa muhimu. Alikuwa tayari amesoma mengi juu ya maisha yao. Alichokuwa akikitafuta hasa ni orodha ya marafiki wa karibu wa marehemu, kwa matarajio kuwa mmoja wao angekuwa na lolote la kumsaidia katika kupata majibu ya fumbo la kifo cha rafiki watatu wa karibu zaidi. Joram Kiango hakuweza kujizuia alitoa kalamu na lile daftari dogo la hayati Afande Chaku na kunukuu majina naanuani zao.

“Hawapo hapa msibani?” Joram alihoji.

“Hawajatokea. Sielewi kwanini, maana hata simu zao sijazipokea.” Khalfan alijibu akiwa katika hali ya mshangao.

“Ningeomba msaada wa kunipatia namba zao za simu kama hutojali.” Joram alisema huku akitoa daftari la hayati Afande Chaku.

Dkt. Twalib Khalfan, aliitikia kwa kutikisa kichwa na kumpatia Joram namba hizo ambazo alizinukuu.

“Sina simu kwa sasa,” Joram alimwambia Khalfan.

“Nadhani si vibaya ukinipa namba yako pia, kwa hadhari tu, ili nikiwa na jambo jipya niweze kuwasiliana nawe.” Alisema akiinuka.

Khalfan hakuwa na hiana. Alimpa moja ya namba yake ya simu ambayo ni watu wachache sana walihifahamu.

“Shukrani tena kwa msaada wako.”

“Sioni kama nimekusaidia chochote.” Khalfan alimjibu. “Ni wewe ninayestahili kukushukuru kwa kunitoa upweke.”

Waliagana kwa tabasamu lililodhihirisha mwanzo wa urafiki na kuaminiana.
 
iko powa,but why have you changed your avatar?
 
nawaahidi nitaanza kuileta mimi kuanzia Kesho.. Nameless hata kama hatatokea nitaifanya hii kazi katika kiwango kizuri kabisa
 
Mmh Ibra, mwenzio hiyo ni strategy ya kuvitangaza vitabu vya Marehemu baba ake, na ofcourse ni njia nzuri kwani me nimeshanunua vinne kupitia hizi nyuzi....sasa sijui atakuruhusu??? maana hata me natamani umsaidie...kitabu hiki sina.
 
mimi nimenunua vitano mpaka sasa.. Hiki mikataba ya kishetani alishawahi kuniruhusu nikishushe humu sema muda wangu ndio ulikuwa mdogo kwangu
 
Back
Top Bottom