Hadithi: Mfalme Kima ambumunda shetani mfupa mweupe

Hadithi: Mfalme Kima ambumunda shetani mfupa mweupe

Elijah

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2012
Posts
1,663
Reaction score
424
Mfalme Kima,aliyepewa mamlaka ya kuivuruga kasri ya peponi,pamoja na Nguruwe na sufii Sah,walimlinda Hisuan TSah,kwenye safari yao ya kwenda kusaka vitabu vya Kibudha,Kima aliongoza njia na wengine walimfuata wakivuka mito na mabonde kuelekea magharibi.

Ghafla kulitanda magenge marefu yaliyokita mbele yao na ukungu mzito ulijaa ukionesha hali mbaya,Kima alisema,''Jamani Jihadharini,nadhani kuna mashetani hapa''.

Hsuan Tsang alipoyasikia hayo hakuweza hata kukaa vizuri juu ya farasi,Kima alimpa moyo kwa kumwambia,''Bwana Usiogope,madhari upo pamoja nami,basi shetani yoyote atakethubutu kuja,nitamuua'',Hsuan Tsang alisema kuwa ni dhambi kuua.

Wakati huo,wingu jeusi lilipita mbinguni,na kwa kuwa na shaka,Kima aliruka kulifuatilia,na mara likapotea mlimani.

Aliporudi Kima,Nguruwe alimnyumbulishia mdomo na kusema,''Kaka,mara una shaka juu ya wingu,mara juu ya ukungu,una wasiwasi sana wewe'',halafu akalipapasa tumbo lake na kusema, tusonge mbele tutakatufe chakula.

Kima bado alikuwa na wasiwasi na aliwaambia wenzake,''huu ni mlima mtupu,na hakuna alama yoyote ya kuwapo binadaamu hapa kwa maili kadhaa,bora nikaangalie njia na nikawatafutieni matunda ya kuzuia njaa''

Aliposema hayo,alitoa fimbo yake iliyo na njumu ya dhahabu,Pruuuuuuh!!! akachora duara kubwa kuwazunguka akina Hsuan Tsang,aliwaambia tena na tena,kaeni ndani ya duara hii,msimsalimie yoyote na wala msile chochote.

Alipoondoka Kima tu,wingu lile jeusi lilipita tena,aliyekuwamo humo alikuwa ni shetani Mbwa mwitu,Mkaazi wa mlima huu,ambaye alitumwa kufanya doria.
 
pono,

Duh ... Umetoa wapi hii, mkuu? Unanikumbusha vitabu nilivyokuwa nasoma wakati huo nipo darasa la pili, kama sikosei ilikuwa ni mwaka 1985 .....!!!
 
kuna misimiati humo hatari ngoja nikipumzika ndio ntaisoma vizur
 
Afadhali nimepata hii adisi.........itaniweka busy.......kuliko siasa hizi.......
Eheee........endelea.........
Ikawaje walipofika kuichafua kasri ya mbinguni.......?.....
 
Afadhali nimepata hii adisi.........itaniweka busy.......kuliko siasa hizi.......
Eheee........endelea.........
Ikawaje walipofika kuichafua kasri ya mbinguni.......?.....

Duuh! NAMI NIMEIPENDA SANA.

Nasikitika sijawahi kuisoma.
 
Duh ... Umetoa wapi hii, mkuu? Unanikumbusha vitabu nilivyokuwa nasoma wakati huo nipo darasa la pili, kama sikosei ilikuwa ni mwaka 1985 .....!!!

Daah! Vinapatikana siku hizi kaka?

Natamani nikisome.
 
photo.jpg
 
Hii tamthiliya ilioneshwa sana ITV kipindi cha watoto siku za jpili miaka ya 1998 na kuendelea ni ndefu sana na inafurahisha sana. THE JOURNEY TO THE WEST ina vituko sana hasa huyo Monkey ni balaa
 
Shiva a.k.a Master alikuwa mduwanzi kama zezeta, mara abakwe na wasichana, kupigana hajui yaani yupo tu kama zombie
 
Kitabu chake ndo kitamu hasa,kiko katika muundo wa catoon,ile fimbo wa mfalme kima ilikuwa noma,
 
Hicho kitabu kilitengenezewa tamthiliya ya brother monkey ilikuwa inarushwa na itv siku ya jmos ktk kipindi cha watoto show
 
Humo mlimani,kulikuwepo shetani mkubwa aitwaye shetani mfupa mweupe,aliyetokana na mrundikano wa mifupa myeupe,aliposikia habari iliyoletwa na shetani mbwa mwitu,mashetani wrote walifurahi Sana,kila mmoja aligombea kwenda kuwakamata akina hsuang tsanga.
Shetani simba, aliongoza msafara wa mashetani wadogo kutoka,wakati huo shetani mfupa mweupe alicheka kwa kukebehi,akasema,'mnajua kwamba hsuang tsang Ana mfuasi aitwaye kima?"
Alipotajwa kima,mashetani wrote walipiga weupe kwa woga,shetani mfupa mweupe alisema,msiwe na hofu,Mimi Nina njia za kupambana naye.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom