Kizuizi -20
Atanitambua mimi ni nani, na pia atajulikana nani mjanja kati ya mjeruhi na mjeruhiwa. Aliapa mwanamke huyu ambaye alikuwa na majeraha kadhaa mwilini mwake.Usiku wa siku hiyo akiwa na vijana wake kadhaa ambao alisafii nao kutoka mbali aliingia katika kupigania ukweli uliofichika.Siku kadhaa za kuwa katika jiji la Dar es salaam tayari alikuwa amepeleleza mambo kadhaa na alikuwa amepafahamu nyumbani kwa Kindo na mengine mawili matatu.Usiku wa siku hiyo hakufanya makosa.Akaivamia nyumba ya Kindo ambaye anajiita James.Akamteka Grace.Sasa amezua kizungumkuti, Emmy anahisi ni Lameck amemteka Grace.James bado hajawa na uhakika ni nani amemteka Grace na hataki kuamini kabisa kama Mariam anaweza kufanya hivyo.
Upelelezi haukuwa na lolote jipya. Mkono wa dola ulitapatapa huku na huku bila mafanikio. Bado Grace hakupatikana.James akajiona kuwa yeye ni ----- mkubwa. Anamuhisi mtu fulani kuwa yawezekana anaweza kuwa anahusika na utekeji huu lakini anapuuzia na kukaa kimya akiwangoja polisi wasioisha kusema neno lao la siku zote upelelezi unaendelea.James akatamani kumshirikisha Emmy juu ya hisia zake. Lakini akahofia maswali kadhaa kutoka kwa Emmy juu ya huyo Mariam.Akiniuliza tulikuwa na mahusiano gani na kwanini aandike kuwa tutaona nani mjanja nitajibu nini? Maswali haya ambayo majibu yake ni magumu sana yakazua kizuizi kwa James kuthubutu kufanya jambo lile.Emmy naye alikuwa na tatizo kama la James. Alijua kitu lakini alihofia maswali kutoka kwa mumewe ambaye alimuamini kwa asilimia mia kuwa alikuwa yu mtakatifu pasi na hatia.Wote wakawa wanawaziana mazuri lakini wakikumbwa na kizingiti cha kuuachia ukweli huru.Sintofahamu ikawazunguka.Emmy akiwa katika kuwaza juu ya Grace, mara akamkumbuka Lameck na kauli yake kuwa ile mimba ilikuwa halali yake.Tumbo likaanza kutetemeka, akaanza kuhisi huenda kuna ukweli fulani katika maneno ya Lameck. Emmy akamfikiria Lameck kuwa si mtoto mdogo azalishe ghafla tu mada ile bila kuwa na hisia fulani.Mahesabu ya mimba yake kuingia yakamvuruga kabisa.Akafumba macho yake kabla ya kukatishwa na hodi getini, alipofungua macho yake akakutana na yule mwanaume aliyekuwa anamuwaza kichwani.Lameck!!Tumbo la kuhara likamkamata, akanyanyuka na kutimua mbio kuelekea ndani chumbani, safari ikaishia chooni.Hakuna kilichotoka. Ilikuwa hofu tu.Huko maliwatoni, Emmy akawaza kuwa hatimaye Lameck ameamua kumkomesha kwa namna nyingine.Pigo la mwisho lenye hatari kupita yote.Lameck ameamua kumshirikisha James siri nzito.Emmy..... James aliita.Emmy akauchuna kana kwamba hasikii lolote.Bado alikuwa maliwatoni bila lolote la kufanya.Nguo zake zilikuwa nusu zimevulika na nusu bado zikiutawala mwili wake. Alikuwa anajiuliza aitike ama aendelee kuuchuna.Shem.... sauti ya Gloria ikaita kutokea mlangoni.Emmy akazidi kuchanganyikiwa.Emmy akapandisha nguo zake na kutoka nje.-Kuna nini? akauliza.Simu yako ilikuwa inaita....naona imekatika....hii inaita tena... Gloria kwa nidhamu akamkabidhi Emmy simu.Mlango ukafungwa akaitazama namba inayompigia.Mshtuko. Alikuwa ni Jose B waukweli ama Sam wapili.Simu ilikuwa imepigwa mara tatu bila kupokelewa.Jose matamaa . akaingiwa na tamaa na wivu kutokana na simu yake kuacha kupokelewa. Akatuma ujumbe.Nakuja nyumbani kwako. Ujumbe huu Emmy aliusoma baada ya kuwa amekata simu badala ya kupokea.Emmy akajikuta anapiga yowe, yowe ambalo halikusikiwa nje ya chumba hicho.Akapagawa na ujumbe ule. Mume wake alikuwa nyumbani na baba yake mdogo pia alikuwa nyumbani.Aibu ya karne!!Emmy akaingia maliwatoni akajisafisha uso wake kwa maji na sabuni.Mara akanogewa akaamua kuoga kabisa. Akajifungia maliwatoni.Hakuweza kuisikia simu ilivyoendelea kuita.Alitumia dakika kumi na tano bafuni.Aliporejea akakutana na simu saba zisizojibiwa.Akatamani kumtumia Jose B ujumbe lakini akajikuta akisahau na kuendelea kuvaa upesi upesi.Kosa kubwa!!Wakati akihangaika, Jose Matamaa alikuwa ametaharuki katika teksi aliyokodi imfikishe nyumbani kwa Emmy, Jose kijana mdogo kabisa asiyejua uchungu anaoupata mwanaume akiibiwa mke wake ama kijana mwingine yeyote anayempenda na kumthamini mpenzi wake anapogundua kuwa anasalitiwa. Alikuwa anafurahia kummiliki Emmy. Ilifikia wakati akawa anatamani kuwa mume wa Emmy ambaye ni mke wa mtu tayari.Kwa jinsi ambavyo Emmy alijirahisisha kuuachia mwili wake ndivyo Jose alivyopata nafasi ya kumtawala zaidi.Sasa bila kujali ni kwa kiasi gani anahatarisha ndoa ya Emmy alikuwa anaelekea nyumbani kwake.Emmy alitoka nje upesi akamuaga James kuwa anaonana na mtu kwa dakika kadhaa nje. Usoni alikuwa ametaharuki, James naye hakuwa na amani moyoni kwani ile hali ya kuona simu ya Emmy ikionyesha jina la Sam wapili. Akamkumbuka Jose B na jina hili lilikuwa na namba ya simu ya Jose.Alitamani kutoka pamoja na Emmy lakini ile tabia yake ya kutopenda kuwadharau ndugu wa mwanamke ikamtafuna akamheshimu Lameck na kuendelea kubaki akimsikiliza huku Emmy akitokomea nje ya geti upesi.Jose B hakuwa na utani hata kidogo. Hata yeye hakujielewa ni nini anafanya. Hakujisikia kumuogopa James, alifanya kile ambacho moyo wake ulimtuma kufanya. Sasa alikuwa jirani kabisa na nyumba ya Emmy. Penzi alilopewa na Emmy likamvuruga akili yake na kuwa kama mwendawazimu.Umri wake wa miaka ishirini na ushee uliruhusu kabisa kuwa katika hali hii. Hali ya kuwa mtumwa katika jambo jipya katika maisha.Emmy alikuwa wa kwanza kumuona Jose B akiwa amejiweka mbali kidogo na geti akiwa ameuegemea mti mkubwa wa mwembe usiokuwa na matunda.Emmy akatembea kwa mwendo kasi, akawa anatembea nusu na nusu anakimbia akiwa amelikamata gauni lake vyema.Sam......nini hiki unanitaka...eehJose B akageuka, alikuwa amenuna. Akamtazama Emmy kwa jicho kali.Unataka kunifanya mtoto mdogo sivyo? akahoji kwa jeuri.Emmy akashusha pumzi zake.Sikia Sam...nakuomba tusizungumze kwa sasa kesho nakuja nyumbani kwako tutakaa muda mrefu tu....niamini tafadhali, James yupo hapo na bamdogo, wanatoka sasa hivi Sam, nitaelewekaje mie pliiz nakuomba Sam nakuomba sana. Sauti yenye kitetemeshi cha hofu ilimkumba Emmy wakati anasihi. Hofu ilikuwa imetawala.Jose B akakumbwa na sintofahamu baada ya sauti ile kupenya katika masikio yake, akajikuta akitabasamu.Jose B alipenda sana kunyenyekewa.Akamkubalia Emmy. Wakaachana bila kuagana.James hakuwa anaelewa lolote lililosemwa na Lameck juu ya kupotea kwa watoto, alikuwa anawaza juu ya Jose B ambaye ana wasiwasi ndiye Sam wa ukweli.Ana hila gani na mkewe wa ndoa tena ambaye ana mimba tayari? Alijiuliza.Hakupata majibu.Akajisikia mchomo wa wivu ukimuandama, akaanza kupata suluba ya aina yake, akafumba macho na kumuona ----- mmoja waliyekutana jijini Mwanza, akamuuzia Kizuzizi kwa shilingi milioni sita, akapewa utangulizi wa shilingi milioni mbili akatoweka. Leo hii anaigusa ndoa yake.James akahisi kuwa Emmy anaweza kuwa ana mahusiano ya siri na Jose B ambaye kwa sasa anajiita Sam.Kwa hiyo huyu ----- amefikia hatua anamfuata mke wangu hapa hapa nyumbani kwangu? Haiwezekani hata kidogo wanichezee shere hawa. Hivi wananijua vizuri kweli?James alihamaki.Lameck aliigundua hali ya utulivu jinsi ilivyopotea katika uso wa James. Akaona asiendelee kuongea sana akamtazama na kumsikitikia kwa mengi.Likiwemo la kulea mimba ambayo si yake na sasa ana wasiwasi na mkewe baada ya kupigiwa simu kisha akatoka nje.Lameck akaamua kuaga na kuondoka zake.Kitendo cha Lameck kuaga kikampa James nafasi ya kipekee kujaribu kuuliza juu ya mtu aliyekuja nyumbani na kisha Emmy kutoka nje.James aliingia chumbani na kumkuta mkewe akiwa amejilaza kitandani, hakuwa na furaha hata kidogo, na kitendo cha mtu kuingia pale chumbani kikampagawisha.Akataharuki waziwazi.Emmy...ni nani alikuja pale nje ukamkimbilia mbiombio.Nani? Mimi? aliuliza swali la kipumbavu Emmy kwa hofu.Kwani humu ndani tupo wangapi? James alijaribu kuzuia jazba yake.Hapana ni rafiki yangu...nani huyu mzoa taka alikuwa anadai.....naniii Emmy alitia huruma, hakuwa na cha kujibu mbele ya mumewe.-James akakunja ngumi yake imara ili aweze kuikabili hasira yake. Akafanikiwa kwa kiasi kidogo.Mlipeana namba lini na huyu mtupa uchafu? James kwa sauti ya chini aliuliza, bado alikuwa amesimama na Emmy alikuwa ameketi.Hajanipigia simu wala.Kwa hiyo alikuita kupitia dirisha la chumbani sivyo? mwanaume akazidi kukoroma. Sasa alikuwa anatetemeka midomo.Haikuwahi kutokea hata siku moja katgika kipindi cha mahusiano yao.Emmy akakosa cha kujibu.James akaitwaa simu ya Emmy pasipo binti huyu kutarajia. Akapekuapekua sehemu ya namba zilizoingia, akakutana na majina kadhaa ya kike. Hapakuwa na jina la Sam wa pili.Akajaribu kulitafuta jina lile. Hakuna kitu.Kijasho chembamba kikamtoka.Akataka kuliendea kabati ili arejee na ile namba ya Jose B aiingize katika simu ya Emmy akahofia kuzua utata baadaye, alimjuaje Sam wa pili.Kama Emmy na Sam wana mahusiano lazima atamshirikisha na hapa ndipo mkanda utakapoharibika.na uhakika hujapigiwa simu na mwanaume wakati nipo na baba yako?Haki ya Mungu tena mume wangu. Akaapa.James akashikwa na hasira kali akakumbuka kuwa wanawake ni sumu kali, sumu isiyostahili kuguswa hovyo. Hasira zikampanda, ameua kwa ajili yake na sasa hana imani kwa ajili yake.Mkono ukawa mwepesi ukalishambulia shavu la Emmy.Kipigo kitakatgifu cha kwanza katika ndoa kikafuata.James akamwadhibu Emmy kwa kujaribu kumficha.Ugomvi wa kwanza ukazua kipigo.Emmy alidhani anapigwa kwa sababu za wivu pekee hakujua kama kuna lolote ambalo James anamuwazia kuwa huenda analifahamu.Wakati anapokea kipigo alijisifu kimya kimya kwa machale yaliyomcheza kwa kuifutilia mbali namba ya Sam wa pili, na pia meseji zake zote, hajui ni mizimu gani ilimtuma lakini alijikuta tu akitekeleza hisia.Emmy alijisifu kwa kuamini kuwa laiti kama James angeipata namba ya Sam angeweza kumpigia na mwisho wa siku angeujua ukweli juu ya mahusiano yake ya kimapenzi na baba mdogo. Jambo ambalo lingepelekea siri tatanishi ya mimba aliyonayo kuchukua nafasi ya kuwa wazi.Ilikuwa bora kupigwa kuliko siri hiyo kuvuja.Emmy hakujua kama mumewe naye kuna siri zake ametunziwa na Sam wa pili ambaye ni Jose B waukweli.Laiti angejua.......***EMMY anaitetea siri yake isifichuke kwa gharama yoyote......***JAMES anahisi Jose B anatembea na mkewe..hajui wameambiana nini.......***LAMECK naye kimya kimya anapigania damu anayoamini ni yak wake...**MWANAMKE aliyemteka Grace naye..........ITAENDELEA