Hadithi: Kizuizi

Hadithi: Kizuizi

Laana hiyo....mtu utalalaje na baba yako bwana..??

Yani ni laana kabisa na ndo maana anakumbwa na matatizo kila kukicha na ataendelea kugawa kwa jose b bila hiyana.Jose B yeye anajilia utamu kiurahisi ila mwisho wake naona hautakuwa mzuri
 
haya tena yule mzee wa storii hatare anarindima jukwaani nani wakumwekea kizuizii....nakereka sana na tabia za kipuuzi za Lameck ni bora James angemuondoa na huyu faraa
 
Wadau inabidi mchango upitishwe ili mzambwa atoe series ya hii kitu, ni uhalisia wa maisha yetu! Hapo record ya vitabu na film itunzwe! Ni wazo tu.
 
HADITHI: KIZUIZI

SEHEMU YA KUMI NA TISA

Siku iliyofuata mapema sana. James anayekaribia kuchanganyikiwa alikwea ndege. Katika sarari nzima aliyawaza maneno yaliyoachwa na mtekaji katika nyumba yake.
“TUTAONA NANI MJANJA.”

**UTATA mpya....maneno yaliyoachwa katika tafrani yanamuhusu EMMY na JAMES naye anadhani aliwahi kuambiwa......ni nani hasa muhusika.

***EMMY anazidiwa ukubwa na matatizo.....anaiokoa ndoa yake kwa gharama za kuuacha mwili wake utumike hovyo.....JOSE B naye anatafutwa jijini Mwanza ilhali yupo Dar es salaam.

***KIZUIZI kimesambaa sasa na ni muda wa kulipuka...KIZUIZI kitaondoka iwapo tu UKWELI utafunguliwa kutoka katika minyororo....
PESA na MAPENZI vinauchelewesha UKWELI huu......

ENDELEA.......


Majira ya saa tano asubuhi, taksi ilipiga honi lakini haikupishwa, umati ulikuwa mkubwa ukimsikiliza Gloria. Fahamu zilikuwa zimemrudia. Vyombo vya dola vilikuwa makini kunukuu kila neno lililosemwa na Grolia.

“Walikuwa wamejifunika usoni, sikumtambua hata mmoja. Lakini kuna mmoja alikuwa ni mwanamke. Walimpiga sana Grace kisha wakaondoka naye. Nilipojaribu kuleta vurugu walinipiga kisha wakanifunga kamba.” Alijieleza huku akibubujikwa na machozi.

Alikuwa anaelezea mkasa uliotokea usiku uliopita.

James aliamua kushuka katika ile taksi baada ya kuona uwezekano wa kupishwa haupo. Hima hima akaliendea kundi lililokuwa limemzunguka Gloria, pupa zikamponza akaanza kusukuma watu wasiofahamu uhusika wake katika tukio lile.

Papara zikamtokea puani, kwanza akatukanwa matusi ya nguoni. Kisha akadhalilishwa kwa kukutana na vibao vikali kutoka kwa polisi waliovaa kiraia.

Kabla hajajitetea zaidi ndipo akaokolewa na mkewe aliyekuwa hajitambui kuwa amevaa kanga moja inayomfanya awe mfano wa kituko flani.

Umati ukasambaratishwa baada ya Gloria na familia yake kuhitajika kituoni kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Emmy alikana vikali kuwa na ubaya wowote na mtu. Na hakuewa na la kusema juu ya maneno yaliyoandikwa katika kile kikaratasi. Maneno yake ya kukana kuhusu kujua lolote juu ya maandishi yale yalimfanya amfikirie Lameck kama muhusika. Akataka kumtaja lakini akapatwa na hofu juu ya usalama wa ndoa yake. Aliamini kuwa kwa kumtaja tu mwanaume huyo mjeshi, lazima angechukuliwa kituoni kwa ajili ya kutoa maelezo yake juu ya tuhuma hizo.

Emmy akaamua kukaa kimya.

James naye aliruka maili mia juu ya kuwa na kisasi na jamii yoyote ile. Na aliruka zaidi juu ya yale maneno akakiri kuwa ilikuwa mara ya kwanza kuyasikia.

Wakati akijibu haya alikuwa na wasiwasi mkubwa sana juu ya mwanamke wa miaka kadhaa nyuma. Alikitazama kidole chake cha shahada kwa makini, akaiona alama ikimdhihaki. Alama ya pete ambayo kamwe isingeweza kutoka kutokana na jinsi ilivyotolewa kwa kulazimisha.

Akahisi huenda kuna mzimu unafanya kisasi badala ya Mariam.

Imani yake ikameguka kiasi fulani na kuamini katika ulimwengu huo wa giza.

Kama ni mizimu nimekwisha? James katika dimbwi la mawazo alijikuta akinong’ona, sauti ikatoka. Ilikuwa bahati kuwa afande mmoja alikuwa anaongea katika simu kwa sauti ya juu. Hakuna aliyeisikia kauli hii.
Mahojiano yakamalizika. Dola ikaingia kazini kufuatilia ni wapi Grace amepelekwa.

Sala za James na Emmy zilikuwa zikihangaika kumfikia Mungu wanayemuamini juu ya uzima wa Grace.
Hakuna aliyekuwa tayari kupokea taarifa juu ya umauti wa mtoto huyu asiyekuwa na hatia.

Emmy akiwa na James pamoja na Grolia na wauguzi kadhaa walioandama pamoja kwa ajili ya kumfikisha Grolia hospitali kwa ajili ya vipimo zaidi, ilisikika sauti kwa mbali ikiita.

“Emmy.....James....” James akasikia, Emmy hakuwa amesikia.

“Bamdogo yulee.” James akasema, Emmy akasikia akageuka.

Mapigo ya moyo yakabadili mwendo wake baada ya kumuona Lameck akija hima. Hofu ikatanda. Akaamini siku ya kuumbuka imefika.

Alitamani kukimbia, lakini akajizuia asije akazua hata yasiyokuwepo. Akajikaza.

James hakutilia maanani kumtazama Emmy usoni. Fursa hiyo ilimtosha Emmy kujilazimisha kurejea katika hali ya kawaida.

Lameck akafika. Akawasalimia wote wawili.

Emmy akajibu bila kumtazama Lameck usoni. James akamchangamkia mwanajeshi yule ambaye pia ni kijana mwenzake.

Kisha akamuelezea kwa kifupi juu ya mkasa uliotokea. Lameck akasikitika sana, Emmy akanung’unika moyoni kwani aliamini ni yeye ambaye amemteka ama amemuua Grace.

Cha ajabu anajifanya kusikitika mbele yake.

Emmy akakumbwa na hasira za ajabu akawa anatetemeka. Ile siri aliyoificha ikawa inamtesa. Kidogo aufungue mdomo wake na kumtuhumu Lameck lakini akasita baada ya kukumbuka kuwa James atapata walakini wa tuhuma hizi na akiamua kuchunguza basi ndoa inavunjika.

Emmy akajizuia kwa kuichukua simu yake na kujikita katika kubofya ilimradi tu asitazamane na Lameck.

“Emmy...we Emmy” James aliita baada ya Emmy kuonekana amejikita na mambo mengine mbali kabisa na mazungumzo hayo.

“Bee...samahani..nilikuwa aaah...”

“Ba’mdogo anakuuliza ...” James alizungumza huku akiwa amekereka. James alisifika kwa kuwaheshimu ndugu wa mwanamke na hakupenda Emmy awakosee heshima hata kidogo.

Lameck alikuwa ndugu yake na Emmy. Baba mdogo.

“Eti Emmy...wewe umerejea nyumbani ilikuwa saa ngapi? Na hukuona alama za tairi za gari ama....”

“Sijaona chochote na sikumbuki nilirudi saa ngapi.” Alijibu kwa jeuri, James na Lameck wakatazamana kwa mshangao. James akapandwa na jazba lakini Lameck akawa wa kwanza kumtetea Emmy kuwa amevurugwa na tukio hilo. James akamuelewa.

Safari ya kuelekea hospitali.

****

James alitangulizana na mgonjwa hadi ndani huku nyuma akiwaacha Lameck na mwanaye Emmy ambaye ni mjamzito.

Hakuna aliyemsemesha mwenzake. Emmy alikuwa ameuvuta mdomo kwa hasira.

“Hivi Emmy unadhani haya mambo ukileta hasira zako za jana yataisha kwa usalama. Wewe kuwa mtulivu tuzungumze tujue tunayamaliza vipi. Ona sasa unataka mume wako ajue mapema kuwa nina tofauti na wewe...”

Lameck alizungumza huku akitazama mbele kama vile hazungumzi na Emmy ambaye yupo pembeni yake.
Emmy hakujibu kitu, Lameck akaendelea, “Sikia kwa sasa nakusihi uwe mtulivu wakati tunatafuta hatma ya Grace....lakini Emmy au kuna mtu ulikwazana naye nd’o analipiza kisasi...” hapa Emmy akageuka na kumtazama Lameck.

Sasa hasira zikakosa subira. Akarusha kiganja katika shavu la Lameck.

Kati ya vitu ambavyo wanajeshi hufuzwa katika kambi zao ni kutomwamini adui yako na pia kumtilia mashaka mwenzako kwa asilimia kadhaa. Lameck akafanikiwa kukwepa kile kibao.

Emmy akapepesuka, Lameck akawahi kumdaka.

Mshangao ukamkumba Lameck, hakuamini kama Emmy anaweza kufanya kitendo kile cha kumwaibisha.
Emmy baada ya kusimama imara alianza kulia kana kwamba amefiwa. Emmy hakuwa na ujanja wa kuzikabili hasira zake zaidi ya kuangua kilio. Ikawa kazi ya Lameck kumbembeleza.

James alipotoka katika huduma iliyompeleka alimkuta Emmy akiwa amenyamaza tayari.

Safari ya kurejea nyumbani.

Polisi wakiwa wanaendelea na upelelezi wao juu ya utekaji huu wa kushtukiza.

Chumbani hapakuwa na la kuongeleka. James kama baba mwenya nyumba alilazimika kujikita katika tukio hili zaidi ya mkewe ilimradi tu aitafute ile furaha ambayo tayari ilikuwa imetoweka kwa mkewe.

James aliamini kwa asilimia zote kuwa ni yeye alikuwa chanzo cha haya yote yanayotokea kuanzia kifo cha baba yake, mdogo wake, na mama mkwe na sasa binamu yake mkewe alikuwa ametekwa bila sababu kuwekwa wazi.

James aliumiza kichwa na kujihisi kuwa anadhalilishwa kwa kiasi kikubwa na huyo adui yake ambaye hadi wakati huo alikuwa hajajiweka wazi. Alikuwa anashambulia kimya kimya.

Inamaana atakuwa ni Mariam? James alijiuliza tena kwa mara nyingine.

“Mariam amefanyaje?” Emmy aliuliza.

James akajishtukia kuwa alizungumza badala ya kuwaza.

Hakujibu lolote. Emmy naye hakuuliza tena.

Walikuwa wameelekezeana migongo.

Usiku ukapita. Grace akiwa hajapatikana.

****

Taarifa za vifo vya Keto na Kakele vilimshangaza sana msichana huyu ambaye aliamini kuwa katika orodha hiyo ndipo atakapoupata ukweli kabla ya kumkabili Kindo.

Wasiwasi ukatanda baada ya kuambiwa kuwa vifo vyao vilitokea katika juma moja lakini siku tofauti.
Kakele akiuwawa kwa risasi na Keto akichomwa visu katika mwili wake.

Katika kufuatilia zaidi tarehe za matukio hayo, akapata jambo jingine jipya kuwa vifo hivyo vilitokea kabla Kindo hajafunga ndoa.

KIZUIZI. Ina maana Keto na Kakele walidhurumiwa na Kindo ama. Alijiuliza yule mwanamke ambaye alijihisi ni mfu anayeishi kutokana na majanga aliyopitia, lakini yu hai sasa na yupo jijini Dar es salaam.

Wazo la kumvaa Kindo moja kwa moja akaliona kama ni la hatari sana na pia litalifanya zoezi lake kuwa gumu sana.

Akaamua kuanzia mbali ilimradi tu amnyanyase Kindo mpaka hatua ya mwisho.

“Atanitambua mimi ni nani, na pia atajulikana nani mjanja kati ya mjeruhi na mjeruhiwa.” Aliapa mwanamke huyu ambaye alikuwa na majeraha kadhaa mwilini mwake.

Usiku wa siku hiyo akiwa na vijana wake kadhaa ambao alisafii nao kutoka mbali aliingia katika kupigania ukweli uliofichika.

Siku kadhaa za kuwa katika jiji la Dar es salaam tayari alikuwa amepeleleza mambo kadhaa na alikuwa amepafahamu nyumbani kwa Kindo na mengine mawili matatu.

Usiku wa siku hiyo hakufanya makosa.

Akaivamia nyumba ya Kindo ambaye anajiita James.

Akamteka Grace.

Sasa amezua kizungumkuti, Emmy anahisi ni Lameck amemteka Grace.

James bado hajawa na uhakika ni nani amemteka Grace na hataki kuamini kabisa kama Mariam anaweza kufanya hivyo.


**********

***MARIAM ana kisasi gani kwa Kindo ambaye anajulikana kama James......
**Keto na Kakele nao wanahusika vipi katika vita hii....
**Lameck licha ya kushuhudia tatizo lililomkabili Emmy bado anakumbushia juu ya mtoto ambaye bado hajazaliwa.....

ITAENDELEA.....
 
Sam wa Ukweli ***** Sam wa Pili
James ***** Kindo
 
Back
Top Bottom