Hadi Fredwah kasepa RFA

Hadi Fredwah kasepa RFA

Kuna mzee nampenda sana pale anayetangaza habari za kimataifa STAT TV Samadu Hassan, ananikosha sana huyu mtu
 
eeba nae,sasa inakuwaje tena manake yule ndiye kinara wa RFA
sasa kuna yule mkongo zuberi ndiye wanamtumia kwa kila kitu
hawezi kukataa kwa sababu akifukuzwa inabidi arudi kwao kongo
Zuberi Msabaha sio Mkongo we kachori, yeye asili yake ni Kigoma lakini shule ya singi amesoma Mwanza pale Mabatini, kabla hajamaliza darasa la saba aliondoka na kwenda kusoma Kongo. Hiyo ndiyo habari ninayoijua juu yake.
 
baada ya usikia NSSF inaendelea kutolewa nadhani akaona avute kwa ku resign hahahhahahaha
 
Jamaa anajua kuvutia watu na majonjo yake,kama kipindi cha vodacom asubuhi ipo sijui kama huyo mwingine ataweza kumfikia jamaa
 
2tazikumbuka sana sindano 5 za moto.. Afu na vichekesho cz jamaa ndo alikua m2 wa kwnza kuintroduce vichekesho kabla ya masage za kufowadiana
 
Jamaa inasemekana hakulipwa mshahara wa miezi mi4,kaondoka yeye na mke wake Rahabu fred zaid ya wiki mbili zilizopita

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
kuna uzi ulishapita umu ukieleza kuwa mishahara wanakopwa afu wanalipwa kwa mafungu mafungu....haina ubishi hata mi ningesepa...sijua kama mke wake, rahab fred au rahab fungo kasepa naye au lah
 
Duuh! Mzee wa VIROBA, kahama! Haya Diallo na li CCM lako limekuganda!:rockon:
 
Mwaka jana July nilitembelea na nilimkuta Fredwaa akiwa ktk kipindi asubuhi, na akanirusha hewani kimtindo.
Am sure tatizo pia linaanzia kwa HR wao Raphael Shiratu, yasemekana hafai kwenye post hiyo.

RFA imezalisha watangazaji wengi sana kwa mfano Mkamiti Juma Kibayesi (VOA-Swahili), Godwin Gondwe, Isaac Gamba, Paul James Sweya (Clouds), Baruan Muhuza, Hamisi Dambaya (Mlimani radio n TV), Gabriel Zacaharia, Roy Maganga,Alex Ngusa (Metro fm), Joan Itanisa, Kid bwoy, Anselim Ngaiza, etc.
Na sasa inawapika vijana wengi wakiongozwa na akina Yahya Mohamed, Gabriel Yotum a.k.a computer, Tom Chilala, mzee Samadu Hassan, Mukhsin Mambo, Paul Mabuga etc.

My take: Chairman Diallo amka na UBADILIKE
 
Kiuzushi nikwamba pale kunamtikisiko washekeli......Siunajua Chaguzi zachama tawala!Fungu linahamia kwenye kampeni,naukikosa kama alivyokosa ubunge mzee wao ukajidai unawachana live wanawatuma TRA wakuue kabisa!!Nasikia hilo ndio janga lililotokea kabla yakuukwaa Uyekiti!!Ngoja tuone matokeo yauenyekiti sasa!
 
Back
Top Bottom