Uchaguzi 2020 Hadhi ya Lissu ni sawa na wagombea ubunge, tusimlinganishe na Rais Magufuli

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Kuna baadhi ya kikundi wanalazimisha kwa kufanya propaganda kuwa Tundu Lissu ni sawa na Raisi Magufuli, wanaenda mbali kwa kutaka ''mdahalo'', sijui nini na nini. Tuweke taarifa sawa, Tundu Lissu sifa zake ni hizi;
  1. Anagombea urais kutafuta ruzuku ya chadema ili angalau baada ya uchaguzi aweze kupata chochote
  2. Anaogombea urais ili kuwaridhisha wafadhili wake; mfano mzuri hata hadhira na mambo anayozungumza yanahusu wakenya na wazungu.
  3. Tundu Lissu anaamini miundombinu, hospitali,shule nk ni maendeleo ya vitu sio watu; sasa hapa kufanya naye mjadala wenye akili watakushangaa. Ni sawa na kumkimbiza kichaa.
Kwa hoja hizo tatu itoshe kusema inashangaza kuona baadhi ya watu wanaoamini kuwa Tundu Lissu anamaanisha analolofanya kiasi cha kumlinganisha na Rais John Magufuli ambaye ametekeleza kwa kufanya mambo makubwa kwenye ujenzi wa nchi. Magufuli anapaswa kufanya yafuatayo;
  1. Anapaswa kwa makini kutulia na kuona ni jinsi gani atatimiza manifesto (ilani) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), ikumbukwe mambo mengi ametekeleza kuzidi matarajio (2015-2020) na sio kujadili mdahalo wa kujadili kuwa miundombinu ni maendeleo ya watu au vitu?
  2. Huyu ni mtu anayetumia akili kufikiri namna ya kuwaletea wananchi kwa kutumia rasilimali zilizopo na sio kufurahisha watu wa nje.
Aah itoshe kusema, Raisi Magufuli hahitaji kujieleza, yeye keshatenda. Ni jukumu la Lissu kuwaambia watanzani Je Barrick/Accacia wameshinda kesi MIGA?

Wasalaam.
 
Media zina wengi wa kutangaza..sio yeye peke yake maana halipii airtime.

Na wale waliokatisha ghafla. Mkuu jiulize kwa nini pamojana madai ya kunyoosha nchi miaka minne wananchi hawana kabisa hamu na CCM, hapa ndio swali la msingi. Ukijiuliza hili swali litasaidia kwenye masuala ya sera na vipaumbele kama Taifa. Huwezi kutumia matrilioni kununua ndege zaidi ya 10 wakati hali ya maisha ya watumishi haiboreshwi kimaslahi. Sasa tunakopa tu kila siku hito stigler mpaka leo, hata nyumbani huwezi kukazania kununua sofa zuri halafu mnashindia mihogo hata protein hampati ili tu akija mgeni aone unaishi pazuri. Mtapata utapia mlo afya izorote mpate na magonjwa mwisho mfe.

Na amini ndugu uchaguzi ukiwa huru na haki kutatokea mshangao mkubwa sana
 
Hamtakaa msahau kosa mlilofanya kwakumzuia mbwa kubweka ndani ya miaka mitano wakati ndo tabia yake mkisingizoa kuwa bado ni mchana. Sasa usiku umefika kaamua kubweka kwa lazima mmeanza kuona ni kelele na zinawakera ili hali mlikubaliana naye usiku awe anabweka.
 
Na wale waliokatisha ghafla. Mkuu jiulize kwa nini pamojana madai ya kunyoosha nchi miaka minne wananchi hawana kabisa hamu na CCM, hapa ndio swali la msingi. Ukijiuliza hili swali litasaidia kwenye masuala ya sera na vipaumbele kama Taifa. Huwezi kutumia matrilioni kununua ndege zaidi ya 10 wakati hali ya maisha ya watumishi haiboreshwi kimaslahi. Sasa tubakopa tu kila siku hito stigler mpaka leo, hata nyumbani huwezi kukazania kununua sofa zuri halafu mnashndi mihogo hata protein hampati ili tu akija mgeni aone unaishi pazuri. Mnatapata utapia mlo afya izorote mpate na magonjwa mwisho mfe.
Na amini ndugu uchaguzi ukiwa huru na haki kutatokea mshangao mkubwa sana
Kwanza tuna sheria ya maudhui..ukitaka kujua kauli anazotumia tundulisu tafuta interviews zake anazofanya na media za nje na hasa kenya. Kwa vyombo makini vya habari ni ngumu kufanya nae coverages. Hata kwenye hardtalk yule jamaa alikuwa anapingana nae sana.

Pili maisha bora ya watanzania hayapo kwenye kula tu..na hakuna mtanzania aliyelalamika njaa. Mahitaji ya watanzania ni umeme, huduma za maji, huduma za afya na miundombinu. Ukiwaboreshea hapo tayari umerahisisha njia za utafutaji riziki.
 
Mkuu nadhani mdahalo ungekuwa poa sana,ili tuone hiyo mechi Kati ya Real Madrid na Lipuli inavyopigwa and in the end tuconclude who is utopolo and who is not
 
Magu hana viwango vya marais usimfananishe na marais wanaoeleweka, yeye viwango vyake ni vya kina iddi Amin, Bokassa, Mabutu nk. Marais wa aina hiyo hawana uwezo wa midahalo maana hawana jipya wala uwezo wa ushawishi, zaidi ya kutegemea vyombo vya dola na kuongoza kwa kujaza watu hofu, na kutengeneza mapenzi bandia.
 
Magu hana viwango vya marais usimfananishe na marais wanaoeleweka, yeye viwango vyake ni vya kina iddi Amin, Bokassa, Mabutu nk. Marais wa aina hiyo hawana uwezo wa midahalo maana hawana jipya wala uwezo wa ushawishi, zaidi ya kutegemea vyombo vya dola na kuongoza kwa kujaza watu hofu, na kutengeneza mapenzi na bandia.
Mkuu mbona umempendelea sana,Hivi mtu anayehangaika na masoko na stend,mtu anayedhani kuweka taa za barabarani Dodoma nayo ni achievement,hata ukimpa cheo cha mwenyekiti wa Kijiji still unakuwa umekidhalilisha cheo hicho
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom