Habinder Sethi aomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabiri ya Uhujumu Uchumi

Puto halijafanyiwa usafi mda mrefu sana itakuwa limechafuka sana. Shikamoo JPM. Hao ilikuwa hawaguswi na mtumishi wa serikali ukiwagusa unaharibikiwa.
 
Hawajashinikizwa, unaomba mwenyewe msamaha na kukiri alafu unarudisha pesa! Kama huwezi kukiri na kurudisha pesa, basi kesi inaendelea na wapo ambao hawajakiri makosa na wanaendelea na kesi kama kawaida!
 
Hivi hizo hela huwa zinarudi kweli au maneno tuu kuonyesha ushujaa wa kushinda kila kitu
 
Mbona lile tumbo la puto halipo tena? Au ndio mazoezi hayo? Mzee atakuwa amefaidika sana kutoa hilo tumbo bila upasuaji, pamoja na hasara ya pesa atakzorudisha ila atakuwa na faida ya kiafya.
Dah kweli aiseh! Aliingia na shepu ya pipa anatoka amenyooka kama muwa!
 
Mwenye akili timamu lazima akubali hata kama hakufanya kosa. Hakuna namana mahakamani hakuna haki ukikataa ndo kwanza unaongeza hasira kwa Mtukufu utafia jela!
Nasubiri kusikia wote 2 wamerudisha zile bil 309!!
 
Mwenye akili timamu lazima akubali hata kama hakufanya kosa. Hakuna namana mahakamani hakuna haki ukikataa ndo kwanza unaongeza hasira kwa Mtukufu utafia jela!
Nasubiri kusikia wote 2 wamerudisha zile bil 309!!
Rugemalila yeye bado amekomaa
 
Kafanya la maana Sana akitutajia aliowagawia rushwa na kutupatia vielelezo wamwachie maramoja, tkkr mtumieni huyu Kama shahidi namba moja.
Pesa irudi. Isijekuwa kuna mchezo umebuniwa na wakubwa kupiga pesa.
 
Ingelikuwa ni vyema hao waliotuhumiwa, masharti ya kukiri iwe ni pamoja na kuchoma ramani nzima ya vita...

Waeleze ni namna gani walikuwa wakihujumu uchumi, na wamekuwa wakishirikiana na kina nani...
Wakiweka masharti hayo yataumbua wengi sana waliopo sarikalini hivi sasa.

Yaani itakuwa ni aibu.

Viongozi wengi wamepatikana kifisadi, kwa hiyo wengi wataumbuka.

Lakini kama tumeamua kujenga Tz mpya, tungefanya kama walivyofanya S.Africa ya Mandela baada ya utawala wa ubaguzi wa rangi, iliundwa kamati ya maridhiano.

Waliotubu bila kujali walifanya kosa gani la kibaguzi, walisamehewa, na waliodinda wakaadhibiwa.

Kwa hiyo na sisi kama unavyoshauri mkuu, wangetajana angalau raia tukaambulia kuwatambua ikatosha.
 
Seth na Rugemalira ndio walikuwa walengwa wakubwa wa msamaha huu.
"wengine wamekonda kweli"
Alisikika akijisemea Rais mmoja huko Afrika mashariki.
Na siyo utani, kwa picha hiyo Seth na huyo mwenzake Ruge wamekonda na kuzeeka sana, tofauti na picha walivyoingia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…