Habinder Sethi aomba msamaha na kukiri makosa yanayomkabiri ya Uhujumu Uchumi

Mkataba na IPTL ulishaisha toka 2017 na Mitambo yao ilishazimwa siku hiyo hiyo.
Watu wanachanganya kati ya mkataba wa iptl/tanesco na leseni ya kuzalisha umeme inayotolewa na ewura. Mkataba unaisha 2023, serikali ilichofanya ni kusitisha ku-renew hiyo leseni ya ewura mnamo 2017 iptl walipoiomba... Singa akajiamini akaja kushughulikia itolewe akiamini system bado ni ileile, ndo wakamdaka hadi leo na sio kua alikuja ku-renew mkataba kama inavyosemwa na watu humu ndani
 
Hilo ndilo la msingi mkuu,nchi hii ya ajabu sana sheria imetupwa kulee,Unakamatwa kuwa umefanya kosa unawekwa mahabusu miaka 3 upelelezi haukamiliki kisha unaambiwa ukili kosa na ukubali kulipa.Hiyo ni zaidi ya mahakama.
100%kwa hoja hii ninakubaliana nawe,why police wanakamata suspects kabla ya kuwa link na kosa kwanza?sasa nani talipa muda wao uliopotea,kodi zetu zilizotumika kuwaweka mahabusu kwa muda wote huu?ukweli hapa polisi hawakuwa na kesi dhidi ya watuhumiwa hawa,ni political games zilizokuwa zinachezwa hapa,tukumbuke suspect ni innocent until proved quilty by court of law,na kwetu sisi utawala,mahakama,bunge vyote hivi vipo pale magogoni.
 
We huoni apo ana kushinikiza (indirect) kesi inaendelea upelelezi hauja kamilika mwaka wa ngapi huu? nauliza
Hawajashinikizwa, unaomba mwenyewe msamaha na kukiri alafu unarudisha pesa! Kama huwezi kukiri na kurudisha pesa, basi kesi inaendelea na wapo ambao hawajakiri makosa na wanaendelea na kesi kama kawaida!
 
Hili neno linaniudhi sana ila basi tu, halafu mnataka kulazimisha mpaka liingie kwenye kamusi ya kiswahili fasaha, sijui huko shule mlienda kujifunza ujinga?
Mkuu mbona hilo nenp lipo kwenye kamusi ya kiswahili au mwenzetu umesoma uingereza
 
MBONA NASIKIA RUGE AMEANDIKA BARUA LKN IMEKUWA TOFAUTI NA SETH
YEYE RUGE AMETAKA NA WOTE WALIOCHUKUA PESA WATAJWE
 
Hana ubavu wa kugoma na yeye kishaandika barua mkuu. Wakili wa serikali kakiri kupokea barua ya hao magwiji na mastering wa hii movie
Mie mwenyewe leo nimesikia kwenye magazeti redioni nikashangaa! hahaha. Si alifikia hata kumzuia mama Tibaijuka asirudishe kwa kumhurumia yeye...
 
Miue mwenyewe leo nimesikia kwenye magazeti redioni nikashangaa! hahaha. Si alifikia hata kumzuia mama Tibaijuka asirudishe kwa kumhurumia yeye...
Ndugu yangu ukiwa neutral jitahidi kusikiliza vyombo vya habari neutral umiendekeza waandishi wa habari wa kileo kwenye mitandao utadhani kuwa kuna mapinduzi ama machafuko ya nchi. Huko twitter huyu Rugemalila kavishwa cheo cha ukamanda sababu tu mtu alisema kawakatalia serikali.
 
Kafanya la maana Sana akitutajia aliowagawia rushwa na kutupatia vielelezo wamwachie maramoja, tkkr mtumieni huyu Kama shahidi namba moja.
Hao hawatajwi... tunakata matawi ili watu waone tunavyopambana na ufisadi huku mashina na mizizi vikinawiri kwa maana tunahusika navyo...
KWA SAUTI KUBWA "Hakuna fisadi asiyeshirikiana na CCM. NA BILA UFISADI HAKUNA CCM"
 
Habinder Seth, anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha, wakili wake Michael Ngalo ameieleza Mahakama ya Kisutu leo.

---
Harbinder Sethi anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ameandikia barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukiri makosa yake na kuomba msamaha

Wakili wake, Michael Ngalo amesema hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipotajwa

Sethi, Mwenyekiti Mtendaji wa PAP pamoja na James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa VIP wanakabiliwa na mashtaka 12 wanayodaiwa kuyatenda jijini Dar, Afrika Kusini, Kenya na India

Wakili wa Jamhuri, Wankyo Simon ameeleza kuwa wamepokea barua ya Seth wanaifanyia kazi na majibu yatatolewa ila kuhusu upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika

Miongoni mwa mashtaka yao ni kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Tsh. Bilioni 309.

gerezani hakuns kansa Wala koresto
 
Huyu muhindi kamuachia msala mzito Jacob Zuma. Kule Kenya alimpiga Uhuru za kugosha tuu !
 
Njia nzuri ya baraka ilikuwa ni kuharakisha upelelezi wa kesi zao na ushahidi kuwekwa mahakamani. Unawezaje kuwaweka watu mahabusu zaidi ya miaka 3 eti upelelezi haujakamilika! Hii ni "saikolojikol tocha" na makusudi na kuwaumiza binadamu wenzako.
Walipokuwa wakiiba na kutuwekea capacity charges, ilikuwa saikolojiko tocha na stress juu
 
Back
Top Bottom