goggles
JF-Expert Member
- Apr 1, 2017
- 2,417
- 2,356
Puto halijafanyiwa usafi mda mrefu sana itakuwa limechafuka sana. Shikamoo JPM. Hao ilikuwa hawaguswi na mtumishi wa serikali ukiwagusa unaharibikiwa.Habinder Seth, anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha, wakili wake Michael Ngalo ameieleza Mahakama ya Kisutu leo.
---
Harbinder Sethi anayekabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ameandikia barua kwenda kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kukiri makosa yake na kuomba msamaha
Wakili wake, Michael Ngalo amesema hayo leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Huruma Shaidi wakati kesi hiyo ilipotajwa
Sethi, Mwenyekiti Mtendaji wa PAP pamoja na James Rugemalira ambaye ni Mkurugenzi wa VIP wanakabiliwa na mashtaka 12 wanayodaiwa kuyatenda jijini Dar, Afrika Kusini, Kenya na India
Wakili wa Jamhuri, Wankyo Simon ameeleza kuwa wamepokea barua ya Seth wanaifanyia kazi na majibu yatatolewa ila kuhusu upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika
Miongoni mwa mashtaka yao ni kujihusisha na mtandao wa uhalifu, kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu, kutakatisha fedha na kusababisha hasara ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Tsh. Bilioni 309.