RIP HABIBA!
This is yet another time to reflect on maternal mortality in this country!
MIMI WOS kama mwanamke....najua kabisa kuwa, Mungu alipomuumba mwanamke na kumpa jukumu la kushiriki uumbaji na kuleta viumbe duniani, alimpa adhabu moja tu - kuumwa uchungu wakati wa kuzaa lakini siyo kufa!
Tujiulize- kama kodi zetu zingetumika kwa vipaumbele sahihi, wamama wengi wangezaa salama! Ni aibu kwa nchi yetu kutokushtuka pale wakina mama wanavyozidi kupoteza maisha kwa vile ati wanatekeleza majukumu yao ya kijinsia/jinsi.
Nchi za wenzetu waliondelea, wanawake kufa kwa uzazi ni kitu kisicho cha kawaida.Huku kwetu, mwanamke anapokaribia siku ya kuzaa huona kifo kikimnyemelea..nakumbuka kupitia hofu hii ya kutisha.
Tumwombee ,mwenzetu aliyetangulia mbele ya haki, MUNGU AMPE HURUMA YA PEKEE NA AMSAMEHE MAKOSA YAKE, AMLAZE PEMA PEPONI - AMEN!