Habiba Kawawa afariki Dar

Hii ni habari ya kusikitisha sana. Poleni sana familia nzima ya Kawawa, ndugu, jamaa na marafiki.
Mwenyezi Mungu Amlaze Mahala Pema Peponi, Amen.
 
Upumzike kwa amani. Poleni wote mliokumbwa na msiba huu. Mungu awajaze nguvu.
Nakasirika lakini bado nina hofu na mungu. Hivi inakuwaje nchi ya Tz. swali la akina mama kupoteza maisha kwa sababu ya uzazi halipati ufumbuzi? Hizi kodi walalal hoi wanalipa kazi yake ni nini?
 
Jamani ndugu zangu wanaJamii Forums. Nimepokea taarifa za kifo cha mtoto wa Simba wa Vita- Rashid Mfaume Kawawa, Habiba Kawawa.

Habiba ambaye alikuwa kipenzi cha Mzee Kawawa, amefariki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jioni hii ambako alikuwa amelazwa kwa matatizo ya uzazi.

Habiba alikuwa ameolewa na Maleko wakiishi Tegeta, jirani na Tegeta Bynight.

Nitawaletea zaidi baadaye.

Bwana ametoa. Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.

Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu na faraja wafiwa katika kipindi hiki kigumu kwao~AMEN.
 
Poleni sana wafiwa. Inasikitisha zaidi kuona kwamba vifo vya namna hii ni preventable and we were once on a right track. But some pple will come by November/ December to tell us how developed we are and how far they have brought us from. Shoddy and cooked statistics on afya will be in the air but the truth will keep on revealing. We strongly need to do something anywayz!!!!!!!!!!
 
Poleni sana wafiwa inasikitisha sna. Labda viongozi wetu wanaweza kushituka na kifo hiki wakabadilika jamni agrrrrrrrrr!!!!!!!!!!
 
Jamani ndugu zangu wanaJamii Forums. Nimepokea taarifa za kifo cha mtoto wa Simba wa Vita- Rashid Mfaume Kawawa, Habiba Kawawa.

Habiba ambaye alikuwa kipenzi cha Mzee Kawawa, amefariki Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jioni hii ambako alikuwa amelazwa kwa matatizo ya uzazi.

Habiba alikuwa ameolewa na Maleko wakiishi Tegeta, jirani na Tegeta Bynight.

Nitawaletea zaidi baadaye.

Bwana ametoa. Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe.

Jamani,! poleni wafiwa,

RIP.
 
Huyu ni yupi? yule aligombea NEC ya ccm?

R.I.P......! Kazi ya mungu haina makosa!
Habiba ni Lawyer by profession, mara ya mwisho nilimfahamu akiwa ni mwanasheria wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. Ameolewa na kijana wa familia ya Mzee Humprey Maleko(RIP) aitwae Johson.

RIP Habiba, poleni sana familia za Kawawa na Maleko.
 
MUNGU ameamua kulichuma uwa lake bustanini. Uamuzi wake hauna makosa, wala haurekebishwi na binadamu yeyote. Sote tuko njia moja, tangulia Dada yetu mpendwa ukatuandalie makao. Poleni wafiwa MUNGU awapunguzie machungu
 
MH!!!! Naam inasikitisha kuona na kusikia habari kama hizo.Si walikuwa wamepanga kumfanyia MZEE WA NCHI?? Itakuweje?? Wata ahirisha au watafanya kimya kimya?
MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU HABIBA
AMEN
 
Back
Top Bottom