KadaMpinzani
JF-Expert Member
- Jan 31, 2007
- 3,715
- 92
‘Chanjo ya ukimwi yaonyesha mafanikio'
na Lucy Ngowi
na Lucy Ngowi
MRADI wa utafiti wa chanjo ya ukimwi unaosimamiwa na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba Muhimbili (MUCHS), unaendelea vizuri, kwa kuwa haujaleta madhara yoyote kwa wote waliofanyiwa chanjo hiyo.
Mtafiti Mkuu wa majaribio ya kuchunguza usalama kwa binadamu na uwezo wa chanjo hiyo kujenga kinga mwilini, Profesa Freddy Mhalu, alieleza hayo jana alipozungumza na Tanzania Daima.
Profesa Mhalu, alisema mradi huo unaendelea vizuri kwa kuwa nusu ya watu waliotegemewa kufanyiwa majaribio wamepatikana na hakujatokea madhara ya aina yoyote.
"Dalili nzuri ya uwezo wa hiyo chanjo kuweza kujenga kinga mwilini zimeanza kuonekana," alisema Profesa Mhalu.
Kwa mujibu wa Profesa Mhalu, utafiti huo utaendelea mpaka mwaka 2009. "Kupata chanjo itachukua muda mrefu na majaribio mengi kabla haujapatikana ufumbuzi, hivyo itahitaji uvumilivu," alisema.
Alisema tatizo wanalokabiliana nalo katika kipindi hiki cha utafiti, ni kutokana na kusambaa kwa fununu zisizo za kweli kwamba wanapofanya majaribio hayo, wanawaachia virusi vya ukimwi watu waliokubali kuchanjwa, jambo ambalo amesema halina ukweli wowote.