sengobad
JF-Expert Member
- Aug 13, 2017
- 8,085
- 7,455
Sadaka za Waumini mnazitumia vibaya, hata malipo haya amechota hapo.Kawe, Dar es Salaam
Toka Gwajima atangaze nia yake ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Kawe kumeibuka wimbi kubwa la vijana wa Chadema na upinzani kwa ujumla kupinga na kumbagaza mitandaoni.
Gwajima anatajwa kama moja ya watu wenye ushawishi mkubwa nchini na moja ya watu walioshiriki kupinga vita ufisadi na Udhalimu mkubwa katika serikali ya awamu ya nne hata watu wengi kudhani ya kuwa ni mpinzani kutokana na aina ya misimamo yake kwenye kusema kweli na kutumia haki yake ya kikatiba ya uhuru wa kuzungumza.
Kwa muda wa miaka kumi (10) jimbo la Kawe limekuwa chini ya upinzani likiongozwa na Halima Mdee ambaye amemaliza muda wake. Kushindwa Kwa CCM Kwa muda wote wa miaka 10 kumetokana na kukosekana kwa wagombea wanaokubalika na wananchi na wagombea wenye mvuto kwenye siasa.
GWAJIMA KUBADILI MWELEKEO WA SIASA
Toka Gwajima ametangaza kutia nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo la Kawe siasa za Kawe zimebadilika na kurudi tena kwenye hali ya ushindani na sasa vyama vya upinzani ikiwemo Chadema wanahaingaika namna ya kuweza kushinda.
Gwajima moja kati ya wachungaji walijizolea umaarufu nchini ni kada wa Chama cha Mapinduzi toka mwaka 1994.
Siasa za Kawe toka enzi ya mzee Dewji na Ritha Mlaki wote wakiwa ni wanachama wa CCM hakujawahi kutokea tena mwanachama ambaye amekuwa na nguvu kubwa kwenye jamii kama ambavyo leo hii iko kwa Gwajima ambaye anatajwa kuwa tishio na kuweza kurudisha jimbo la Kawe tena kwenye himaya ya CCM.
KWANINI GWAJIMA ANAFAA KAWE NA CCM?
Ziko sababu nyingi za umuhimu wa Gwajima kwenye jimbo la Kawe na serikali kwa ujumla;
1. Gwajima ni muumini wa siasa za ukweli hivyo atamsaidia sana Rais Magufuli katika kujenga taifa lenye misingi imara ya haki na ukuaji kuelekea malengo ya Taifa ya 2025.
2. Gwajima ni mtu anayejua kusukuma mambo kutokea Kwa haraka na sio mtu wa kukata tamaa. Hii itafanya Serikali kuweza kuharakisha miradi mingi ya Maendeleo kwenye Kata na jimbo zima la Kawe.
3. Gwajima ni mtu ambaye atakisaidia Chama cha Mapinduzi kutokutumia gharama kubwa ya Uchaguzi kutokana na haiba yake kwa kuwepo watu ambao wataenda Kwenye kampeni kumsikiliza ili tu kumuona Kwani wengi wanatamani kumuona Kwa ukaribu zaidi.
4. Gwajima ni kiongozi ambaye siku zote amekuwa akitaka kuona Tanzania inanufaika na rasilimali zake hivyo atakuwa Msaada mkubwa katika serikali ya awamu ya Tano ambayo toka kuanza kwake imekuwa ikipambana kuhakikisha rasilimali za Taifa zinakuwa na tija kwa UHAI wa Taifa.
5. Gwajima anaungwa mkono na makundi mengi ndani ya vyama vya siasa na nje hivyo hii kuwa mtaji mkubwa wa ushindi wake na Chama cha Mapinduzi.
Haya ndio mambo yanayofanya Chadema na vyama vingine vya upinzani kupambana na kuumiza vichwa juu ya Gwajima.
Gwajima ni mtu sahihi wa kuumaliza upinzani na siasa zisizo na matokeo ndani ya jimbo la Kawe.
Ndimi,
Mzee Shaban Malingumu
Kawe Ukwamani.