Uchaguzi 2020 Gwajima: Mtia nia CCM anayewaumiza vichwa Chadema

kudamademede

Member
Jan 1, 2020
18
75
Kawe, Dar es Salaam

Toka Gwajima atangaze nia yake ya kugombea ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Kawe kumeibuka wimbi kubwa la vijana wa Chadema na upinzani kwa ujumla kupinga na kumbagaza mitandaoni.

Gwajima anatajwa kama moja ya watu wenye ushawishi mkubwa nchini na moja ya watu walioshiriki kupinga vita ufisadi na Udhalimu mkubwa katika serikali ya awamu ya nne hata watu wengi kudhani ya kuwa ni mpinzani kutokana na aina ya misimamo yake kwenye kusema kweli na kutumia haki yake ya kikatiba ya uhuru wa kuzungumza.

Kwa muda wa miaka kumi (10) jimbo la Kawe limekuwa chini ya upinzani likiongozwa na Halima Mdee ambaye amemaliza muda wake. Kushindwa Kwa CCM Kwa muda wote wa miaka 10 kumetokana na kukosekana kwa wagombea wanaokubalika na wananchi na wagombea wenye mvuto kwenye siasa.

GWAJIMA KUBADILI MWELEKEO WA SIASA
Toka Gwajima ametangaza kutia nia ya kugombea ubunge kwenye jimbo la Kawe siasa za Kawe zimebadilika na kurudi tena kwenye hali ya ushindani na sasa vyama vya upinzani ikiwemo Chadema wanahaingaika namna ya kuweza kushinda.

Gwajima moja kati ya wachungaji walijizolea umaarufu nchini ni kada wa Chama cha Mapinduzi toka mwaka 1994.

Siasa za Kawe toka enzi ya mzee Dewji na Ritha Mlaki wote wakiwa ni wanachama wa CCM hakujawahi kutokea tena mwanachama ambaye amekuwa na nguvu kubwa kwenye jamii kama ambavyo leo hii iko kwa Gwajima ambaye anatajwa kuwa tishio na kuweza kurudisha jimbo la Kawe tena kwenye himaya ya CCM.

KWANINI GWAJIMA ANAFAA KAWE NA CCM?
Ziko sababu nyingi za umuhimu wa Gwajima kwenye jimbo la Kawe na serikali kwa ujumla;
1. Gwajima ni muumini wa siasa za ukweli hivyo atamsaidia sana Rais Magufuli katika kujenga taifa lenye misingi imara ya haki na ukuaji kuelekea malengo ya Taifa ya 2025.

2. Gwajima ni mtu anayejua kusukuma mambo kutokea Kwa haraka na sio mtu wa kukata tamaa. Hii itafanya Serikali kuweza kuharakisha miradi mingi ya Maendeleo kwenye Kata na jimbo zima la Kawe.

3. Gwajima ni mtu ambaye atakisaidia Chama cha Mapinduzi kutokutumia gharama kubwa ya Uchaguzi kutokana na haiba yake kwa kuwepo watu ambao wataenda Kwenye kampeni kumsikiliza ili tu kumuona Kwani wengi wanatamani kumuona Kwa ukaribu zaidi.

4. Gwajima ni kiongozi ambaye siku zote amekuwa akitaka kuona Tanzania inanufaika na rasilimali zake hivyo atakuwa Msaada mkubwa katika serikali ya awamu ya Tano ambayo toka kuanza kwake imekuwa ikipambana kuhakikisha rasilimali za Taifa zinakuwa na tija kwa UHAI wa Taifa.

5. Gwajima anaungwa mkono na makundi mengi ndani ya vyama vya siasa na nje hivyo hii kuwa mtaji mkubwa wa ushindi wake na Chama cha Mapinduzi.

Haya ndio mambo yanayofanya Chadema na vyama vingine vya upinzani kupambana na kuumiza vichwa juu ya Gwajima.

Gwajima ni mtu sahihi wa kuumaliza upinzani na siasa zisizo na matokeo ndani ya jimbo la Kawe.

Ndimi,

Mzee Shaban Malingumu
Kawe Ukwamani.
 

wagotheleopardskiller

Senior Member
Jan 9, 2020
105
225
Mimi ni mwana-CCM lakini sitaki Gwajima awe mgombea wetu hata kwa dawa.

Kwanza ana chuki za wazi dhidi ya makundi mengine ya watu, mfano; hawapendi waislam hata kuwaona (Mdini) na alishaanza kutoa vipeperushi tena kwa lugha ya kisukuma (Mkabila)

Lakini pia huyu bwana atakuwa anakinajisi chama kwani tayari ameshachafuka na ushahidi wa wazi upo.

Kwahiyo kwa maslahi mapana ya nchi na chama huyu bwana ni bora zaidi akiwekwa pembeni maana yeye mwenyewe kashindwa kujitambua na kujiweka pembeni kwa hiyari yake.
 

mwanadome

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,132
2,000
Wewe ni muongo huko kawe ukwamani.
Unajua jinsi waislam walivyokua wanamuwekea vikao Gwajima juu ya chuki zake kwa uislam. ? .

Unajua ngonyani alivyo piga hela Milioni tano ya gwajima akidai ametumwa na msikiti wa shamsia wa Kawe mwisho. ? . Na baada ya hapo Gwajima akawa dhihaki waislam kua msikiti wa shamsia Kuna tofali lake? .

Unajua jinsi Gwajima alivyokua akiushambulia ukatoliki wazi wazi huku akijua pale pekasi aliokua ni karibu na kanisa katoliki. ? .

Unajua jinsi Gwajima alikua ana muhonga hela Hasan Faraji Ngonyani, ili azime malalamiko ya waumini wa kiislam wa hapa kawe mzimuni. ? . Au unadhani ngonyani alivyokua atoa mgao kwa wajunbe wa ccm wakiongozwa na Marehemu Hamza Mwinyimadi na Marehemu kigodora watu hawajui. ? .

Kwa hapa kawe mzimuni na Ukwamani, watao mpigia upatu Gwajima ni wajumbe wa nyumba kumi wa ccm walio kua wanufaika wakubwa wa rushwa zake zilizokua zikipitia kwa alikyekua mwenyekiti wa mtaa wa Kawe mzimuni Ngonyani.

Kwa hapa Kawe Ukwamani, Mzimuni, Udoweni, Mikoroshini, Maringo na mjimpya hunidanganyi chochotee.
 

mwanadome

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,132
2,000
Mimi ni mwana-CCM lakini sitaki Gwajima awe mgombea wetu hata kwa dawa.

Kwanza ana chuki za wazi dhidi ya makundi mengine ya watu, mfano; hawapendi waislam hata kuwaona (Mdini) na alishaanza kutoa vipeperushi tena kwa lugha ya kisukuma (Mkabila)

Lakini pia huyu bwana atakuwa anakinajisi chama kwani tayari ameshachafuka na ushahidi wa wazi upo.

Kwahiyo kwa maslahi mapana ya nchi na chama huyu bwana ni bora zaidi akiwekwa pembeni maana yeye mwenyewe kashindwa kujitambua na kujiweka pembeni kwa hiyari yake.
Gwajima ni mdini na makabila aliye pindukia. Tunao ishi Kawe lilipokua kanisa lake tunajua vizuri.
 

Stores

Member
Jul 1, 2020
53
95
Aah kusema ukweli tu Gwajima Ni hatarii tupu, Great Mind, Yaan namuelewa SANAAA
Wana Kawe mnaenda kupata Mtu atakaye wawakilishaa Vizuriii Sana, Hongereni Wana Kawe # Gwajima Anawapeleka mbali sanna
 

Inanambo

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
3,315
2,000
kudamademede,
Si apitishwe apambane? Yeye anaoneshwa jinsi ambavyo hafai kuongoza Kwa kauli zake na matendo yake. Aachiwe tuu awe Mboga ya Wapinzani. Ina maana CCM wote wameisha kuwakilisha Kawe amebaki Gwajima? CCM ni Makini hawawezi kumpitisha.
 

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
2,930
2,000
Wewe ni muongo huko kawe ukwamani.
Unajua jinsi waislam walivyokua wanamuwekea vikao gwajima juu ya chuki zake kwa uislam. ? .

Unajua ngonyani alivyo piga hela Milioni tano ya gwajima akidai ametumwa na msikiti wa shamsia wa kawe mwisho. ? . Na baada ya hapo gwajima akawa dhihaki waislam kua msikiti wa shamsia Kuna tofali lake? .

Unajua jinsi gwajima alivyokua akiushambulia ukatoliki wazi wazi huku akijua pale pekasi aliokua ni karibu na kanisa katoliki. ? .

Unajua jinsi gwajima alikua ana muhonga hela Hasan faraji ngonyani, ili azime malalamiko ya waumini wa kiislam wa hapa kawe mzimuni. ? . Au unadhani ngonyani alivyokua atoa mgao kwa wajunbe wa ccm wakiongozwa na Marehemu hamza mwinyimadi na Marehemu kigodora watu hawajui. ? .

Kwa hapa kawe mzimuni na ukwamani, watao mpigia upatu gwajima ni wajumbe wa nyumba kumi wa ccm walio kua wanufaika wakubwa wa rushwa zake zilizokua zikipitia kwa alikyekua mwenyekiti wa mtaa wa kawe mzimuni ngonyani.

Kwa hapa kawe ukwamani, mzimuni, udoweni, mikoroshini, maringo na mjimpya hunidanganyi chochotee.
Hivi umesahau kuwa Gwajima amewachimbia waislam maji misikitini au unajitoa ufahamu?
 

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
2,930
2,000
kudamademede,
Si apitishwe apambane? Yeye anaoneshwa jinsi ambavyo hafai kuongoza Kwa kauli zake na matendo yake. Aachiwe tuu awe Mboga ya Wapinzani. Ina maana CCM wote wameisha kuwakilisha Kawe amebaki Gwajima? CCM ni Makini hawawezi kumpitisha.
Sasa hofu yenu ni nini maana yeye ametangaza nia tu tena ndani ya chama lakini naona mnatoa Sana povu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom