Mwinjilisti Mkweli
Member
- Nov 21, 2023
- 10
- 24
Siku ya Jumamosi ya tarehe 21 iliandikwa historia ya kunyesha mvua isiyo ya kawaida iliyosababisha maafa makubwa sana. Pamoja na maeneo mengine, jimbo la Kawe liliguswa vibaya sana na mvua hizi.
Madaraja mengi yalikatika, nyumba ziliondoka na kukabaki misingi tu. Magari na samani nyingi zilisombwa na maji. Tangu siku ile jana mbunge Gwajima amekuwa bega kwa bega na watu wake kuhakikisha anakuwa nao huku akipambana kurudisha tumaini tena kwenye maisha yao.
Gwajima ameonekana sana kwenye site za madaraja na barabara huku greda alilonunua likipambana na tope usiku na mchana kusaidia wananchi. Madaraja mengi yamerudishwa katika hali yake na mawasiliano ya barabara yamerudi kuimarika vyema.
Kama vyombo vya habari havioni jambo hili sisi wananchi tutatumia midomo yetu kumwambia mbunge asante kwa moyo wako wa ukarimu. Jitihada zako tangu ulipoamua kugombea mpaka leo zinaonekana.
Mtu akija jimboni na aweke akili yake sawasawa. Ukituletea masentensi ya ovyo eti mbunge hajatusaidia tutakufundisha hii ndio Kawe ya Gwajima. Mitaro ya Mbweni, mitaro ya Msasani, vivuko na barabara alizotengeneza unaweza kudhani Gwajima wako 1000 kumbe jamaa ni mmoko lakini shughuli ni ya kubafu aroooo.