Kama ilivyo kawaida maisha ni fedha, kwa lissu, mbowe, Lema na wote mnaowaona wanapiga kelele kwa kivuli cha Demokrasia,
Bwana Gwajima alishayaona ya mbeleni ya kwamba kwa kuwa hakuna alilowafanyia Wana Kawe lolote lile la msingi, kurudi kwake bungeni itamuwia vigumu sana, ukizingatia wakati akiwa bungeni, kanisa liliporomoka kwa kiasi fulani kwa sababu bunge na maslahi yake yalimtosheleza kwa kiasi kikubwa sana,
Sasa kwa kuwa upande wa bunge unakwenda kutamatika aliona ni vyema akaliimarisha kanisa kwa njia ya Kiki, ili kuvuta hisia za walio wengi ili hatimaye kanisa lipate nguvu upya! for next survival
#Hesabu zake ameziwahisha mapema mno!, muda ulikuwa bado sana!
#Intelegensia!
Mkuu unapotosha wazi wazi tena asubuhi, kwanza Askofu Gwajima kahoji jambo ambalo lipo na ushahidi upo! Kwa hili tukubaliane mapema kuwa hajasema uongo!
Pili, mkuu majukumu ya ya msingi ya mbunge ni 3 mengine ni nyongeza tu. Moja na muhimu ni kuwawakilisha na kuwasilisha maoni ya wananchi wa jimbo lake bungeni jambo ambalo mimi na wewe tunakiri kuwa kalitendea haki kwa kipindi chote.
Jukumu la pili mkuu, ni kutunga sheria, kwa kipindi chote ameshiriki kikamilifu kutunga sheria kama wajibu wake, hakuna mahali popote ambapo spika amesema kuwa Askofu Gwajima alikuwa mtoro bungeni.
Na jukumu la tatu, ni kupitisha bajeti ya serikali na kuisimamia serikali katika utekelezaji wa bajeti hiyo bungeni.
Tukubaliane hapa, mbunge hana bajeti ya maendeleo katika jimbo lake. Serikali ndio inawajibu na jukumu la kupeleka maendeleo katika kijiji, Kata, wilaya na mkoa chini ya watendaji wake husika.
Kwa maana hiyo unadanganya makusudi na kwa nia ovu kwa sababu ya uchawa na chuki zako binafsi dhidi ya Askofu Gwajima, mbunge ambaye ametimiza wajibu wake ipasavyo.
Mkuu, isitoshe unajinasibu hapa kuwa wewe ni mkereketwa wa chama cha CCM ambacho moja ya misingi yake mikuu ni kusema ukweli. Askofu Gwajima ambaye kada mwenzako, mbunge wa CCM na mjumbe wa NEC ya CCM kasimamia ukweli, kahoji jambo la msingi mno, halafu unaleta unafiki mbuzi hapa!
Mkuu inaonyesha ni jinsi gani huwezi kuaminika kwa lolote! Ujue muda huwa ni mwalimu mzuri, kuwa na akiba ya maneno!