Tulimumu
JF-Expert Member
- Mar 11, 2013
- 14,395
- 13,273
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es salaam,Guninita,aimeitaka CCM imdhibiti Nape Nauye kwa kukiuka maadili ya chama,na kuropoka majukwaani akiita wenzie mizigo!Chanzo Gazeti Majira uk.3
Guninita amshambulia Nape 27/01/2014 | Posted by Josephat Isango | Kitaifatangulizi | 0 comments | 362 views
HALI si shwari ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kufuatia uteuzi wa mawaziri uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete hivi karibuni ambapo sasa makundi mbalimbali yameanza kuibuka na kushambuliana kwa maneno makali, wengine wakiwatetea mawaziri mizigo, wengine wakihoji rais kutozingatia ushauri wa Kamati Kuu ya CCM iliyopendekeza baadhi ya mawaziri kutoswa kutokana na utendaji mbovu.Aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita, jana alitoa tamko na kulisambaza akiponda mkutano uliofanywa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kuwa anatumia vibaya nafasi yake kujitafutia umaarufu binafsi na kusema kuwa chama ndiyo kimemwagiza wakati ni maoni yake binafsi.
Akiungwa mkono na baadhi ya wenyeviti wa CCM kutoka mikoa kadhaa, na kutoa tamko alilolisaini, Guninita alisema kuwa Nape ni kiongozi wa CCM ambaye anafanya kazi bila kuzingatia mipaka yake, hasa kwa kitendo chake cha kuhoji uteuzi wa rais.
Guninita aliwatetea wale waliotajwa kuwa ni mizigo kuwa wengi wao walikuwa tayari na mipango na michango mizuri kuhakikisha wanafanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM, huku akiponda uteuzi wa Nape kuwa alipata kazi ya uenezi wa CCM kimjomba mjomba kutoka kwa Rais Kikwete kwani ni mwoga wa chaguzi za demokrasia.
Aliongeza kuwa Nape ni mropokaji na katika tamko alilotoa kuhusu mawaziri mizigo ameonyesha dhahiri kuwa anampinga rais asifanye kazi yake kwa uhuru, hivyo kuwaonya wanachama wengine wa CCM wanaosema Nape na Kinana wajiuzulu wanakosea, badala yake waseme Nape adhibitiwe kwani hana sifa kwa nafasi anayoongoza.
Nape ameamua kufanya kazi makao makuu ya CCM, mwenyekiti sasa ni yeye, katibu yeye, vikao vya kamati kuu yeye, vikao vya halmashauri kuu yeye, hii ni hatari sana kwa chama chetu, aliandika Guninita.
Vile vile alisema yote yaliyotamkwa na Nape katika mkutano na waandishi wa habri ni maneno yake sio maamuzi ya chama kwa kuwa hakuna kikao kilichoketi kuamua na akaongeza kuwa Nape kama anataka haki ya kuteua mawaziri, agombee urai sio kumwingilia rais madaraka yake.
Akijibu tuhuma hizo, Nape aliliambia Tanzania Daima kuwa hajapinga popote uteuzi wa rais, isipokuwa Guninita amekurupuka, hakusoma tamko, na anatumiwa, tena anatumika vibaya na anajua kuwa anatumika.
Aliongeza kuwa Guninita kusema kuwa yeye kapata kazi kwa ujomba ni matusi kwa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) ambayo ina mjumbe toka kila wilaya nchini, ambao ndio waliompitisha yeye kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama, Itikadi na Uenezi, tena ni matusi pia kwa Mwenyekiti wa CCM aliyemteua.
Matusi ya Guninita ni historia yake, Watanzania wanamfahamu, na watampuuza, kwani anatumika, hana kazi, hivyo akipata fedha kidogo na kuombwa amchafue mtu hatasita kufanya hivyo, alisema.
Tanzania Daima 27/01/2014