Mwenyezi mungu awe nasi Wana wa Tanzania, nimesikia sauti ikinipa ujumbe kwamba ni muda muafaka sasa kwa viongozi wa dini wakasema neno juu ya green guard. Inavyoonekana hawajaanza kusema juu ya hilo wakati tayari limeshaanza kuleta madhara.Tunajua watasema maana wao si wanafiki siku zote na tumezoea kuwaona wakiwa hivyo.Zipo sauti za baadhi ya viongozi wa DINI ambao mara nyingi wakiongea huwa nchi inatikisika kwa watu wote pamoja na serikali hufungua masikio, lakini hadi sasa hawajaongea mimi naamini lazima wataongea kwani wao si wanafiki lakini wasiwasi wangu ni kwamba wanaweza waje kuongea muda umepita na madhara tayari yametokea na pengine hayadhibitiki tena.
Tunawasihi sasa waongee kabla hatujafika huko. Hawa wana karama hiyo si kwamba kuna upendeleo, hapana wamejariwa na mwenyezi mungu kuwa hivyo(sauti zao ni mamalaka kamili) .Naamini hata wewe unayesoma unakubaliana na mimi.Najua pia kwa sasa wako bussy wanasali kwa kufunga novena na hija mbalimbali kwa nia nzuri ya kuombea amani.Basi ni vema watoke mafichoni wasema MOJA KWA MOJA KWA KUKEMEA JESHI HARAMU LA CCM,nasi tutasikia hata serikali isiyo sikivu itasikia na itaweweseka kwa kuelewa ahaaa wenye AMANI, UPENDO NA MATUMAINI wamenena.
SEMENI BUS LILOBEBA AMANI YA TANZANIA KARIBU LINAOONDOKA HAMTALIPATA KWANI LINA MWENDO MKALI
Ni hayo tu