Green Guard ina tofauti na Interahamwe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Green Guard ina tofauti na Interahamwe?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Msharika, May 22, 2009.

 1. M

  Msharika JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF, nimesikitishwa sana kusikia kuwa Chama Cha Mapinduzi kina jeshi.

  Je hii ndio katiba ya nchi kuwa kila chama kiwe na jeshi lake? Mbona hapatatosha.

  Ninasadiki kuwa Nyerere (RIP) aliona mbali kwa kuondoa kile kiitikio cha "zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa chama".

  Nielewesheni jamani
   
 2. M

  M-bongo JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 338
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Yawezakana hukupata bahati ya kusoma historia ya nchii hii, sasa historia inabaki kuwa historia tu hata kama haitakuvutia.

  Wakati TANU ikianzishwa kulikuwa na vijana waliokuwa na majukumu ya kulinda chama na viongozi wake, kulinda mikutano ya TANU na kazi zingine ambazo vijana wangeweza kuzifanya kulingana na ujana wao kwa maslahi ya Chama. vijana hawa waliitwa TANU YOUTH BANTU na baadae TANU YOUTH LEAGUE (umoja wa vijana wa TANU)!

  Baada ya kuanzishwa kwa CCM umoja huo uliendelea na kubadilika kuwa UVCCM(Umoja wa Vijana wa CCM) wenye sehemu ya chipukizi na green Guard, hawa green guard majukumu ni yao ni sawa na niliyokueleza hapo kwenye sehemu ya TANU YOUTH BANTU. swali jingine?
   
 3. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Leo wameripotiwa na chombo kimoja cha habari kama Janjaweed wa CCM baada ya kumchakaza mwanachama wa cha cha upinzania na kumvunja mbavu kule Busanda. Janjaweed kule Zanzibar ni maarufu kwa vurugu dhidi ya Wapinzani kama ilivyo kule Dafur Sudan.

  Kwa ufupi ni wasaidizi wa Jeshi la Polisi na hutumika pale inapoonekana Polisi wanashindwa kutimiza maagizo na matazamio ya CCM katika chaguzi mbalimbali.
   
 4. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #4
  Oct 9, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuwa nikifatilia hiki kikundi kinachoitwa green guard kwa muda hivi malengo yake nn?mbona kama baadhi ya vitendo vyake kama kupiga wapinzani vinashabihiana na vilivyofanywa na kile kikundi maalufu kilichotekeleza mauaji ya kimbari kule rwanda?mwenye kujua shughuli zake kwa undani atupashe,usipoziba ufa utajenga ukuta
   
 5. u

  urasa JF-Expert Member

  #5
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mahakama ya uharifu wa kivita inawasubiria,ukiwaangalia hali zao ni ngumu na wanakubali kuendelea kutumika,waache siku zao zinahesabika
   
 6. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #6
  Oct 9, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tofauti ya Simba na chui kwa ukatili haipo kwa hiyo ni walewale....ICT(R)T
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Oct 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Hata wakiwatumia hao Green Guards, ipo siku tu watashindwa na nguvu ya umma.
   
 8. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #8
  Oct 9, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  swali la msingi ni moja, kama tanzania ni nchi ya amani, na ccm ni chama chenye demokrasia safi, kuna haja gani ya jeshi lao jingine nje ya majeshi ya ulinzi na usalama? hakuna tofauti kati ya green guard na wahalifu
   
 9. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Green Guard wanaratibiwa kwa ufanisi zaidi kuliko Interahamwe....
   
 10. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Hao ni sawa na intarahamwe tu
   
 11. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #11
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Swali zuri sana hilo. Kwanini CCM haiamini jeshi letu la polisi hadi kuamua kuwa na jeshi lao?
   
 12. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #12
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hilo ni jeshi la CCM, watatwambia walipata kibali wapi cha kuanzisha jeshi. Halafu Mwema na Mwamunyange wako wapi mpaka chama kinaanzisha na kuimarisha jeshi lake?
   
 13. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #13
  Oct 11, 2010
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  sheria ya nchi inazuia kuanzishwa vikundi vyenye malengo kama ya green guard, sasa wao wako juu ya sheria au ndo mambo ya kibanzi na boriti ndani ya jicho?
  Upinzani umeshindwa mara 3 uchaguzi mkuu lakini hawana hivi vikundi vyenye mrengo na sera za kiinterahamwe/ janjaweed. Sasa anayehatarisha amani ni ccm au wapinzani? madaraka matamu jamani! sheria zinapindishwa haswa (kukidhi matakwa ya ccm)
   
 14. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #14
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  "The military don't start wars. Politicians start wars."
   
 15. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #15
  Oct 11, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa anayetaka kuleta umwagaji damu nchini ni wale ambao hawana jeshi lao au wale wenye jeshi lao ambalo linafanywa siri? Hebu tuelezwe vizuri hapa nani hasa anayetaka kuleta umwagaji damu.
   
 16. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  blue guard je?!
   
 17. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,849
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Mwenyezi mungu awe nasi Wana wa Tanzania, nimesikia sauti ikinipa ujumbe kwamba ni muda muafaka sasa kwa viongozi wa dini wakasema neno juu ya green guard. Inavyoonekana hawajaanza kusema juu ya hilo wakati tayari limeshaanza kuleta madhara.Tunajua watasema maana wao si wanafiki siku zote na tumezoea kuwaona wakiwa hivyo.Zipo sauti za baadhi ya viongozi wa DINI ambao mara nyingi wakiongea huwa nchi inatikisika kwa watu wote pamoja na serikali hufungua masikio, lakini hadi sasa hawajaongea mimi naamini lazima wataongea kwani wao si wanafiki lakini wasiwasi wangu ni kwamba wanaweza waje kuongea muda umepita na madhara tayari yametokea na pengine hayadhibitiki tena.
  Tunawasihi sasa waongee kabla hatujafika huko. Hawa wana karama hiyo si kwamba kuna upendeleo, hapana wamejariwa na mwenyezi mungu kuwa hivyo(sauti zao ni mamalaka kamili) .Naamini hata wewe unayesoma unakubaliana na mimi.Najua pia kwa sasa wako bussy wanasali kwa kufunga novena na hija mbalimbali kwa nia nzuri ya kuombea amani.Basi ni vema watoke mafichoni wasema MOJA KWA MOJA KWA KUKEMEA JESHI HARAMU LA CCM,nasi tutasikia hata serikali isiyo sikivu itasikia na itaweweseka kwa kuelewa ahaaa wenye AMANI, UPENDO NA MATUMAINI wamenena.
  SEMENI BUS LILOBEBA AMANI YA TANZANIA KARIBU LINAOONDOKA HAMTALIPATA KWANI LINA MWENDO MKALI
  Ni hayo tu
   
 18. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hii ni hatari sana!sana mambo ya Rwanda ya 1994 yameshaanza kuandaliwa hapa!
   
 19. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #19
  Oct 17, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  KWELI TUMEFIKA HAPA??


  [​IMG]


  [​IMG]


  Wakazi wa Musoma walivyokatana (Green Guard) mapanga hivi karibuni


  Source: Mjengwa
   
 20. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #20
  Oct 17, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Maggid anaona kwa wanamusoma kuuana siyo tatizo. hiyo amenukuu kwa bosi wake (JK) alipokuwa anaelezea vita vya kikabila musoma kwamba wakurya ni utamaduni wao kuuana wanapohitilafiana.

  Sasa maggid aje huku kufafanua hiyo jadi ya wakurya. halafu fujo za CCM dhidi ya vyama vingine wa kulaumiwa ni polisi.
  haya sisi yetu macho
   
Loading...