Grand Theft: Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel na Sasatel - Wanachochea ufisadi?

Mwanakijiji Thanks kwa kulileta hili suala.
Hata mimi nilipokuwa Tanzania, nilishajiuliza mara Nyingi, mbona Pesa ninayoweka inakwenda haraka kuliko wanavyotangaza Maredioni kuhusus gharama kwa sekunde?, nikafanya kautafiti kidogo kwa kufanya timing ya muda ninaotumia ili nicalculate gharama halisi(simu yangu ina stopwatch)!, nikaona kuwa nyakati nyingine inakuwa chini nyakati nyingine inakuwa juu hata katika nyakati zile ambazo wanatangaza kuna upungufu wa Gharama, lakini cha aajabu siku nyingine nikifanya mahesabu sioni kupunguziwa Gharama zozote.

Pia nikaja kugundua kwamba wanapowatangazia Wananchi kuhusu gharama kwa sekunde n.k kwenye Redio na TV , vyombo vinavyowafikia wengi zaidi, hawatangazi kwamba VAT included, ila wanapoweka maelezo kwenye Website zao na mabango ndo wanasema VAT included.
 
wadau mi nshachoka na kudhulumiwa na hawa wapuuzi wachache wanaoshirikiana na majambazi wa kigeni...nawapa ishu..nipo tayari kujilipua na fisadi papa mmoja..and iam serious cuz my blood is boiling,..i have nothing to lose...check this out..
celtel-zain-airtel wamiliki ni kigoda,mwinyi,mkapa,salim A salim etc
vodacom wamiliki wote mnawajua
tigo sijui
zantel sijui
sasatel lowassa
 
Mkuu nipo safarini ila nitapitia points za wachangiaji nikifika Dar, ila nimeshindwa kujizuia juzi asubuhi nilitumiwa msg kwenye mtandao wa tiGO kuwa nikitumia tigo rusha napata pesa mara mbili yake baada ya mishemishe nikaweka elfu 5 cha ajabu sikupewa bonus ya credit ambayo ilieleza ingeweza kutumika kwa mtandao wowote. Badala yake nilipewa muda wa maongezi wa saa moja na dakika kadhaa zitakazotumika ti/+ kwenda tiGO cha ajabu baada ya elfu 5 kwisha nilishindwa kutumia ule muda wa ziada wa kupiga tiGO nilikasirika sana nikaona hawa jamaa wameshatugeuza mandondocha sasa!
 
  • Thanks
Reactions: Paw
MM kwanza nataka nikupe few hints:

1. muda huu ambao unaonyesha matumizi ya simu yamekuwa makubwa sana kumbuka ulikuwa ni kipindi cha harakati za kura za maoni kuelekea uchaguzi mkuu, kwahiyo naamini kwamba wakati ule matumizi yalkiluwa makubwa sana.
2. kwenye soko la huduma za simu kuna vitu viwili lazima uvijue; i. operators strategies and ii. consumers' behaviour

Makampuni ya simu yana mipango yao ya ufanyaji wa biashara, kila kampuni ya simu inataka iwe na wateja wengi inavyowezekana na inataka pia wateja wake wawe wanapigiana wenyewe kwa wenyewe kupitia mtandao wao kama tigo-tigo au voda-voda, sababu kubwa ni kwamba kila simu inayopigwa nje ya mtandao mmoja kwenda mtandao mwingine (offnet calls) kampuni ya simu inalazimika kuilipa ile kampuni pigiwa kiasi fulani(interconnection charges) na hii ni gharama kwa kampuni wakati kama wateja watawasiliana ndani ya mtandao mmoja (onnet calls) kunakuwa hakuna malipo yoyote, ndio maana unaona gharama za tigo to tigo au aitel to airtel is cheap than airtel to voda au to tigo....

Sasa wateja (consumers) nao wanajua nikimpigia mtu nje ya mtandano mwingine ni gharama zaidi, hata wewe jaribu weka voda 5000 piga mtandao mwingine uone kinachofanyika, unaweza kutukana, lakini kama nikipiga kwenye mtandao uleule gharama zinakuwa kidogo sana...sasa angalia yafuatayo....

Gharama ya kununua line ya simu Tanzania ni ndogo sana, kwa wastani ni shilingi 1000, lakini pia bei za simu za mkononi zimeshuka sana na wachina wamesaidia kuleta simu za line zaidi ya moja (dual sim), siku hizi kwa taarifa yako unapata fancy phone, durable and good quality kuaunzia 20,000, au unasikiaga makampuni ya simu yakitoa simu za bei nafuu au wakifanya promotion ya kununua line mpya..

Everyone wants to push lines to the market....sasa unaona hapa kama ni wewe ungefanyaje? Na hii tabia ya kuwa na line zaidi ya 2 sio kwa watu wa kipato cha chini tu...hata matajiri nao wanyo, Ninawajua hata wafanyakazi wengi wa kampuni hizo za simu wan zaidi ya line ya kampuni anayofanyia....

kwahiyo studie zinaonyesha matumizi ya simu yanapungua zaidi ya 30% ukiwa una line zaidi ya moja na ukawa unapiga mostly onnet calls, na kumbuka in TZ hatuna monthly charges, unaweza ukakaa na line na usiitumie kwa muda kama sikosei wa miezi mitatu maximum.

kitu kingine ni kwamba the only time u can enjoy flat rates to all calls ni when u r a Postpaid customers na hii ni asilimia ndogo sana ya wateja katika kila mtandao wapo kwenye hii huduma kutokana na masharti ya kuipata na gharama zake, kwa hiyo ni kwa wenye uwezo tu...asilimia kubwa ya wateja ni prepaid, na kumuka ARPU (average revenue per user per month) haivuka sh 25000....

kitu kingine nipende kuweka wazi ni kwamba sheria za kuanziasha makampuni ya simu inataka lazima 35% imilikiwe na local (watanzania) utakumbuka kuna wakati RA alitaka kuuza share zake za voda ilizua mgogoro na TCRA na akashindwa.

kuhusu kwamba mashirika hya ni chanzo cha rushwa naweza kusema inawezekana lakini pia inachangiwa sana na serikali yenyewe haswa TRA, mpaka leo TRA hawajui jinsi ya kuwalipisha kodi makampuni ya simu hakuna jinsi ya kucontrol mapato ya kampuni za simu na kumbuka haya makampni yanatoa hesabu za uongo ili wasikatwe kodi kila siku wanasema wanapata hasara, wanachangia sana jamii, bado wanainvest....blablablah.......

aiseh nahisi hili darasa linaweza kusaidia katika kazi yako..........

mimi ina line 4
natumia zaidi tigo
matumizi yangu ni zaidi ya 200,000 kwa mwezi( kutokna na shughuli zangu)
na hiyo sijui ni asilimia ngapi ya mapato yangu...hahahhaaa
suala lako la f tayari zantel wanafanya lakini watu hawatumii, ndio ninachosema behaviour...
 
Halafu kitu kingine watanzania hatuna utamaduni wa kuchunguza whether hizi tsh 3 kwa sekunde au 1 tsh kwa sekunde ni kweli

Hapo umenigusa kweli sijawahi kuhakikisha kama ni kweli naghalamia kiasi hichi kinachotangazwa
 
Hapo umenigusa kweli sijawahi kuhakikisha kama ni kweli naghalamia kiasi hichi kinachotangazwa

Wanajua hizi sijui nusu shilingi, sijui robo shilingi hauwezi kufuatilia kumbe ni wizi mtupu hakuna cha robo, nusu wala shilingi moja
 
Mhhh!!!! I see
 
Yawezekana watu wengine wanaona kuwa ni kawaida tu.

Mimi natofautiana kidogo na mwanakijiji kuhusu matumizi ya simu kwa sababu matumizi ni matokeo ya demand/supply function. Anayeona gharama za simu ni kubwa ataacha kupiga na kampuni ikikosa mapato itafikiria kupunguza bei ya charge ku atract subscribers. Kwa li nchi likubwa kama TZ ambapo watu wametawanyika sana simu bado muhimu sana. TCRA wanatakiwa tu wasimamie ushindani wa kweli hizi kampuni zisije zikaunda cartel ya kuseti price limit ili kuwakamua wa tz. Tofauti ya simu na Buzwagi ni kwamba huwezi ukaamua leo kuwaondoa wawekezaji lakini simu ukiichoka unaweza ukatupa laini ukaendelea na ustaarabu mwingine
 
Kusema ule ukweli wasomi watanzania niwavivu kukemea uovu unapoonekana. Hapa ninapoishi mfano ninalipa bili ya simu kwa dakika 750 kwa mwezi, kwa dola 89, iwe umepiga ama umetuma text message, ili mradi hutumi nje ya nchi. rate ni statandard kwa mwezi mzima, ninalipia internet kwa mwezi dola 45. Sasa nilipoludi nyumbani likizo nilinunua zantel internet kwa shiling 150,000. Nilikuwa nawasiliana kwa email kwa kipindi cha wiki moja bila ku download wala nini iliisha nikaambiwa niongeze fedha. Mpaka naondoka Tanzania kuludi kwenye mabox yangu nilitumia si chini ya 500,000 kwa ajili ya internet. Swali langu ina maana hakuna viwango kuwa mtu ulipie/alipie kiasi gani kwa mwezi?? huu si wizi tena wa machomacho kabisa na wahusika wanatamba na Ma VX ya kodi za mtanzania wakijiita wakurugenzi??

Mzee MM za leo Mzee mwenzagu.

Leo nimeona nije na Avatar inayo nionyesha sura yangu halisi. Mbweha.

Najua wengi hawanipendi eti kazi yangu ni kula mifugo yao hasa nyama laini ya Mbuzi. Lakini wasichosema siku zote ni Uhalifu wa wafuga mbuzi walioifanyia jamii yangu!

Wamevamia makazi yangu na kufanya eneo la kilimo; wameua digididgi na swala wote kwa kitoeo kana kwamba mimi sina meno na njaa, wameua wajomba zangu wengi na kutupa mizoga yao eti nyama ya mbweha ni Haramu, kisha nyika wakazijaza mbuzi na kondoo wa kufugwa.

Wao walikula digidigi na swala walio halali yangu ya asili na mimi nakula mbuzi wao.

Hivi kumwibia aliye kuibia ni Nongwa??

Kuhusu Simu za mkononi,hata mimi nina kilio changu Binafsi.

Nikituma Dila 500 kwa Mshua na Maza kule homu wanachanjiana nusu kwa nusu 300 nzima itaishia kwenye vocha.

500 hapa Marekani na pengine mahali popote duniani ni maji ya shingo nahitaji kubeba Box zaidi ya wiki 2 ili nipate 500.

Ni halali kwa Watanzania kutumia zaidi ya 60% ya kipato chao kwenye simu??

Wametufanya mbele na nyuma kwenye utajiri wetu wa asili kule Buzwagi!

Sasa wanatufanya kwa nyuma kwenye simu za mikononi pia???!

Ni lini tutajinasua kutoka Mbaniko za Mipimbi yao ya udharimu??
 
Yawezekana watu wengine wanaona kuwa ni kawaida tu.
Hilo ni mojawapo la tatizo linalowakabili Watanzania, na mafisadi wanatumia kigezo hicho kuifisadi nchi. Tatizo kubwa la Watanzania ni kukubali kuwa kila kitu ni cha kawaida ili mradi kudumisha 'amani' na 'utulivu'. Hakuna anayejitokeza na kupinga mambo ambayo yanakera wananchi amabayo kwa nchi zingine sio kawaida bali ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Inabidi Watanzania tubadilike na tuanze kuuliza pale tunapoona tunaumizwa. Msemo wa 'mpaka kieleweke' ni mwanzo mzuri.
 
Mkuu Mwanakijiji,

naomba unisaidie tafadhali. Ni wazi kwamba hizi kampuni za simu zinatuibia, pengine kutokana na kwamba serikali yetu haitatutetea (labda kwa sababu wakurugenzi wao ndio policy makers- RA et al)

Isipokuwa sijaweza kung'amua uhusiano kati ya matumizi makubwa ya pesa kwenye simu za mkononi, gharama kubwa za kutumia simu na corruption kama tittle yako ilivyo. please assist?
 
Gurudumu, Mtanzania ambaye mshahara wake ni shilingi 500,000 kwa mwezi anaweza vipi kuhudumia laini nne za simu na kumudu gharama za maisha?
 
Kusema ule ukweli wasomi watanzania niwavivu kukemea uovu unapoonekana. Hapa ninapoishi mfano ninalipa bili ya simu kwa dakika 750 kwa mwezi, kwa dola 89, iwe umepiga ama umetuma text message, ili mradi hutumi nje ya nchi. rate ni statandard kwa mwezi mzima, ninalipia internet kwa mwezi dola 45. Sasa nilipoludi nyumbani likizo nilinunua zantel internet kwa shiling 150,000. Nilikuwa nawasiliana kwa email kwa kipindi cha wiki moja bila ku download wala nini iliisha nikaambiwa niongeze fedha. Mpaka naondoka Tanzania kuludi kwenye mabox yangu nilitumia si chini ya 500,000 kwa ajili ya internet. Swali langu ina maana hakuna viwango kuwa mtu ulipie/alipie kiasi gani kwa mwezi?? huu si wizi tena wa machomacho kabisa na wahusika wanatamba na Ma VX ya kodi za mtanzania wakijiita wakurugenzi??
Kuna wakati nilikuwa na kazi ya research iliyonitaka niwe na access mtandao muda mwingi na nilikuwa likizo. Nikajaribu kutumia hizi kampuni za simu Voda, TIGO na Zantel hadi nikajaribu virushi vyao. Niligundua ni wizi mtu ikabidi niwe naenda ofsini kufanya hiyo kazi ya research.
 
Well, I know this story is posted somewhere around here. But, after my conversation with a number of wadau, I have come to theorize that the current tax regime for phone companies (telecommunication) is somewhat fueling petty corruption as well as grand corruption. I intend to show in an upcoming report/ story that my theory indeed is reasonably true.

For those of you who use phone service in TZ help me answer these questions just to give my an idea which I'll try (with the help of others) to prove the existence of a linkage between current phone service in TZ and the prominence of petty corruption.

a. How many phone lines do you currently own?
b. What major phone companies do you use?
c. What would you consider to be your monthly average bills for all the phone services?
d. How do you afford to pay for all phone services - your phone bill is what percent of your expenditure?
e. What percent of your income is the the amount of money you spend on phone services?
f. If you were given an option to have a phone service with an unlimited service for a flat rate for standard services would you continue to have more than one line?

Standard services: Free local calls, standard rate for interconnection to other carriers, free long distance, free sms and free voicemail?
Ngoja niende field sijui sample size ni ngapi
 
Gurudumu, Mtanzania ambaye mshahara wake ni shilingi 500,000 kwa mwezi anaweza vipi kuhudumia laini nne za simu na kumudu gharama za maisha?

  • Watanzania wengi mishahara yetu ni chini ya 300,000. hiyo laki 5 ni kubwa sana.
  • Mtu wa hali ya chini anatumia wastani wa sh 1000 kwenye simu kwa siku. Hapo ataweka sh 500 kwenye line 2 tofauti kwa matumizi tofauti kama internet nk
  • Matumizi haya ni ya kawaida kwa ajili ya ku beep, sms nk. Ikitokea swala muhimu lenye maslahi au tatizo linalohitaji kupiga simu, gharama inaongezeka accordingly
 
MM,
Kwanza nikupongeze kwa kuibua hoja hii. Ni ukweli usiopingika kwamba watanzania tunaliwa sana kwenye eneo hili la mawasiliano. Wakati mwingine nimekuwa nikihisi kuwa viongozi wetu wa serikali hawafanyai kazi yao ipasavyo ya kulinda wanyonge ambao ndiyo asilimia kubwa dhidi ya wafanya biashara. Kwa ujumla, biashara ya mawasiliano ya simu ya mkononi imefichika kwa kiwango fulani, ikilinganishwa na biashara nyingi. Ni biashara ambayo munuzi wa huduma hana uhakika sana kama anachopata kina thamani halisi ya fedha aliyolipa. Kwa hiyo kuna uwezekano mkubwa sana mteja akawa anaibiwa kiasi fulani bila yeye kujua kwa maana kwamba thamani ya huduma anayopewa inakuwa chini ya thamani ya fedha aliyolipa.

Ngoja nitoe mifano michache.

Mfano wa kwanza:
Wakati fulani nikiwa Dodoma niliongeza muda wangu wa hewani kwenye line ya Tigo wa Sh. 10,000. Baada ya kuongeza, nilipiga simu kwa mtu aliyekuwa na line ya Tigo tukaongea muda usiozidi dakika 2. Baadaye, nilimpigia mtu mwingine kwa line hiyo hiyo ya Tigo, tukaongea muda mfupi sana nadhani ilikuwa chini ya dakika 1. Mida ya jioni nilimpigia mke wangu ambaye nae ana line ya Tigo. Niliongea nae sekunde chache simu ikani-prompt kwamba muda wa maongezi kwenye simu umeisha na kweli baada ya sekunde chache simu ilikata. Kwangu mimi hilo halikuwa jambo la kawaida. Nilighadhabika sana pamoja na ukweli kuwa Sh. 10,000 siyo kiasi cha kunifanya niwe na hasira hivyo. Kilichoniudhi nilihisi ulikuwa ni wizi tu. Kesho yake niliwafuata Tigo head office na kulalamika. Kilichonishangaza waliangalia akaunti yangu na kuniambia kuwa ni kweli kulikuwa na makosa fulani na kwamba wangenirejeshea muda wangu. Baada ya kuondoka ofisi zao, iliingia sms kwamba nimeongezewa muda wenye thamani ya Sh. 5,000. Sasa nilijiuliza, ni watanzania wangapi maskini ya Mungu kwanza wanaoweza kushtuka kuwa wameibiwa, pili wanaoweza hata ku attempt kulalamika na kufanya follow-up?? Almost none; ni kama zero. Wengi wao wanaishia kulalamika kwa marafiki zao na hawachukui hatua yoyote.

Mfano wa pili:
Mimi ni miongoni mwa wateja wa mwanzo kabisa wa kampuni iliyokuwa inaitwa celte, ikaja ikaitwa zain na sasa inaitwa airtel. Kuna huduma ambazo mwanzoni hazikuwepo japo ni muhimu sana katika ulimwengu huu wa uwazi na ukweli. Hivi sasa ukipiga simu kwa airtel baada ya kumaliza maongozi inakuletea summary ya gharama uliyotumia na kweli ukiangalia balance uliyokuwa nayo kabla ya kupiga, muda uliotumia kwenye maongezi, gharama uliyotumia na salio au balance mpya unaridhika. Sasa nimekuwa nikijiuliza wakati ule ambao huduma hiyo haikuwepo wengi wetu si tulikuwa tunaliwa tu bila kujua. Unajua mtu anayeongea dk 5 akiibiwa dk atajuaje? Ni vigumu sana. Sasa fikiria ni wateja wangapi wanaotumia simu na kila mmoja akiibiwa sekunde au dakika kadhaa kwa ujumla wao, fedha itayopatikana definitely itakuwa ni nyingi sana.

Mfano wa tatu na wa mwisho
Wakati simu za mkononi zinaingia nchini kwa wenzetu zilikuwa zimeanza kutumika kwa miaka kadhaa. Binafsi nafikiri kama kuna kipindi ufisadi na wizi wa waziwazi ulifanyika katika sekta ya mawasiliano basi ni wakati huo. Nakumbuka watanzania tulikuwa tunauziwa handset kubwa za analogy aina ya Nokia kwa Sh. 600,000. Ikumbukwe wakati huo hali ya kiuchumi kwa ujumla ilikuwa ni mbaya sana. Kama kawaida ya watanzania, kukurupukia mambo, wengi walijipigapiga na kununua hayo ma handset na wakati huo nakumbuka ilikuwa ni Mobitel na Tritel. Zilipoingia simu za digital tukawa tunanunua line kwa Sh. 20,000 mpaka Sh. 30,00 ingawa baadaye bei ilianza kushuka. Mimi mwenyewe nilinunua line yangu ya Celtel kwa Sh. 15,000.

Kwa ujumla, sekta ya mawasiliano ya simu za mkononi nchini imetumika sana kuwaibia wananchi. Gharama za mawasiliano kwa muda mrefu zimekuwa extremely high lakini viongozi wetu wa serikali aidha kwa umbumbu wao au ufisadi wanakaa kimya. Na sababu kubwa ni kwamba viongozi wanaopaswa kuyanyoshea vidole makampuni ya simu ndiyo wanaorubuniwa na kukubali kuwa wenyeviti wa Bodi za wakurugenzi wa makampuni hayo (rejea mfano wa Mzee Pius Msekwa akiwa spika wa bunge na wakati huo huo akiwa m/kiti wa bodi ya vodacom). Kwa mtindo huo, inawezekana baadhi ya makampuni yame-generate mitaji mikubwa ya biashara kwa kutumia jasho la wananchi maskini na serikali yao ipo inawaangalia tu.

Inasemekana hata uchaguzi uliopita makampuni yamekichangia chama fulani kiasi kikubwa cha fedha ili kufanikisha kampeni zake. Ni namna gani makampuni yatarejessha hizo fedha, wanajua wao lakini chanzo pekee ni jasho la mwananchi.

Mimi binafsi nina line 3 na ninatumia wastani wa Sh. 50,000 kwa mwezi. Kipato changu kwa mwezi (take home ni Sh. 850,000. Wakati nilipokuwa na line 1 gharama kwa mwezi ilikuwa zaidi ya Sh. 70,000. Kwa hiyo, kama walivyochangia wenzangu, line 3 ni kwa ajili ya kukwepa gharama za interconnection.
 
Halafu kitu kingine watanzania hatuna utamaduni wa kuchunguza whether hizi tsh 3 kwa sekunde au 1 tsh kwa sekunde ni kweli

Hakuna ukweli wowote, tena hao tigo wanafiki kweli.... wanadai eti sh1 kwa sekunde lakini ukijaribu kufatilia wanaka hadi sh5/sekunde tigi-tigo wakati mwingine.
Utamaduni wa watanzania kuhoji mambo haupo au hawoni umhimu wowote kwani wanajua nchi iko mikononia mwa MAFISADI na hao mafisadi wamiliki wa hiyo mitandao mf RA hisa 35% voda, mama rwakatale about 50% hisa sasatel.
 
Hiyo ndiyo njia ya kumpumbaza mtu na kumfanya afikirie kile anachoambiwa ndicho anachopata wewe fikiria kwanini makampuni ya simu yanafanya sana marketing kwenye TV na REDIO hasa kwenye promotion ya Sh1 kwa sekunde, Nusu shilingi kwa sekunde na kadhalika
 
Back
Top Bottom