Graca Simbeni Machel

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,270


Alizaliwa mwaka 1945 huko Gaza Province ambayo ndiyo Msumbiji ya sasa. Ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto sita. Baba yake ambae alikuwa mchungaji wa kanisa la Methodist, alifariki wiki sita kabla ya kuzaliwa kwa Graca. Usia alioacha baba yake wakati anakufa, aliwahusia watoto wake watano wakubwa, kuhakikisha Graca anamaliza A levels. Alifaulu vizuri masomo yake ya A level na kupata Methodist Scholarship kwenda Lisbon University nchini Ureno. Graca anaongea kwa umahiri mkubwa Kijerumani, Kispanish, Kireno, Kiingereza na lugha yake ya kuzaliwa Shangan.

Alianza uana harakati akiwa mwanafunzi Ureno, polisi walimfuata na kumshauri aache masomo na kukimbilia nchini Switzalernd amasivyo kilichokuwa kinamkabili ni kifungo. Akiwa Ulaya Graca alijiunga na harakati za FRELIMO mwaka 1973. Baada ya uhuru wa Msumbiji mwaka 1975 Graca alichaguliwa kuwa waziri wa kwanza wa Elimu na Utamaduni. Aliolewa na rais wa kwanza wa Msumbiji Samora Machel. Walibarikiwa kupata watoto wawili, Josina na Malengani,

Graca ni mwanamke wa kwanza kuolewa na marais wawili walio madarakani. Ndoa yake ya pili ilikuwa mwaka 1998 kwa rais wa Afrika ya Kusini wakati huo Nelson Mandela.

Hizi ni nafasi mbali mbali alizowahi kuzishika Graca Machel

  • Mozambican Minister for Education and Culture (1975-1989)
  • Chairman of National Organization of Children of Mozambique
  • President of National Commission of UNESCO
  • Chancellor of the University of Cape Town
  • Chancellor of the African Leadership University[14]
  • Chairperson of ACCORD's Board of Trustees[15]
images


images
 
Back
Top Bottom