Google Map walipataje majina ya mitaa na barabara zetu?

Google Map walipataje majina ya mitaa na barabara zetu?

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
25,093
Reaction score
27,182
Nimekuwa mtumiaji wa Google Map na Google Earth kwa zaidi ya miaka sita sasa. Sikuwahi kujiuliza ni utaratibu gani uliowawezesha Google Map kuyapata majina ya vitongoji na vijiiji hadi barabara za maeneo mbalimbali, hususani ya kwetu huku ndani Tanzania.

Hivi karibuni nilikuwa ninatengeneza security za simu janja (smart phone) yangu na moja ya features za hiyo app ilikuwa ni location. Haikuwa ajabu kwangu kwani nilishatumia google map before.

Hata hivyo nimeona ni wakati muafaka wa kutafuta majibu kutoka kwa wadau wengine kuhusu hili swali; Hao Google Map developers walitumia utaratibu gani kupata majina ya hasa barabara zetu za huku vichochoroni?

Nawasilisha
 
World Satellite
Mkuu soma vizuri swali langu. Sitaki kuamini kama satellite inaweza ikajua kuwa hapa panaitwa Marwa Road na pale panaitwa Wasira Street
 
raia wengine tunasaidia ku-map.... especialy sehemu za ndani ndani, hata we unaweza kufanya hivyo na baadae wao watapitia na kuhakiki!!!!
 
Mkuu soma vizuri swali langu. Sitaki kuamini kama satellite inaweza ikajua kuwa hapa panaitwa Marwa Road na pale panaitwa Wasira Street

Kwani hayo majona ni siri kwamba hawatakiwi kuyajua. Yapo kwny ramani za miji hivyo wakitaka wanaomba kutoka jiji/miji husika
 
Ok, nataka nijue hiyo project ilitumia utaratibu gani kupata majina ya vichochoro. Wazawa walifuatwa wakaulizwa au watendaji wa vijiji au ni kitu gani?

Nijuavyo mimi, ramani nyingi sana za mipangomiji na master plans ziliandaliwa wakati wa ukoloni na hata baada ya uhuru kuna wazungu waliendelea kidogo kufanya kazi kwenye eneo hili kwa hiyo wana data nyingi mno hata zaidi ya majina ya mitaa.

Hata Topographical maps nyingi tunazozitumia sasaivi ni zile zile ambazo waliziacha wao kwa hiyo hata vijiji, misitu na rasilimali nyingine nyingi wanazifahamu vizuri pengine kuliko hata taasisi zetu zilivyotakiwa kujua.

Inawezekana hii imechangia sana wao kujua ila lazima kuna protocol fulani ya kuhusisha mamlaka kutumia hayo majina...
 
Mkuu soma vizuri swali langu. Sitaki kuamini kama satellite inaweza ikajua kuwa hapa panaitwa Marwa Road na pale panaitwa Wasira Street

Kwa sababu Google ndiyo mtandao mkubwa duniani,na kwa sababu world satellite ndiyo inayoongoza kui-view dunia nzima.Kuna uhusiano kati ya Google na world satellite.
 
Kama ulivyoelezwa hapo mwanzo kuwa wachangiaji wakubwa wa kurekebisha mitaa hiyo na vitongojp na majengo ni wewe mwenyewe. Kama uMember wa Google kuna option katika Google map ya kujiunga na kutoa majina na kusahihisha Baadhi ya wenzako nao watachangia kwa kuikubali basi wanaiweka lakin wakikataa basi inaondolewa
  • Wataulizwa wenzako km ni kweli wakikubali imepita wakikaa kimya haujapita wakiikataa haijaputa
  • Mimi nimeshachangia marekebisho na kuipa mitaa ya Mji wa Dodoma na wakaikubali km Barabara ya 6,7,8,9,10,11&12 kwani ilikosewa wakanikubalia
  • lakini baadhi ya Hotel za Mji wetu kuna Member tola India alipinga sana hasa kutokana na majina ya Kizungu haikupita lakini kweli zipo
 
Watu wa tech mkishindwa kumjibu huyu jamaa kisawasawa mtakuwa mmetia aibu sana jukwaa hili! Okoeni jukwaa lenu fasta!
 
darasa la nne nafiki tulifundishwa ramani zinavyotengenezwa.

-wanatumia aerial image. picha zinapigwa na satelite then wanaziconvert kuwa ramani

-wana map maker ambazo mtu kama mimi na wewe tunaweza ku contribute kutengeneza

-wana magari yenye camera zinazozunguka nyuzi 360 ambayo nayo yanamap
 
raia wengine tunasaidia ku-map.... especialy sehemu za ndani ndani, hata we unaweza kufanya hivyo na baadae wao watapitia na kuhakiki!!!!
Kama ulivyoelezwa hapo mwanzo kuwa wachangiaji wakubwa wa kurekebisha mitaa hiyo na vitongojp na majengo ni wewe mwenyewe. Kama uMember wa Google kuna option katika Google map ya kujiunga na kutoa majina na kusahihisha Baadhi ya wenzako nao watachangia kwa kuikubali basi wanaiweka lakin wakikataa basi inaondolewa
  • Wataulizwa wenzako km ni kweli wakikubali imepita wakikaa kimya haujapita wakiikataa haijaputa
  • Mimi nimeshachangia marekebisho na kuipa mitaa ya Mji wa Dodoma na wakaikubali km Barabara ya 6,7,8,9,10,11&12 kwani ilikosewa wakanikubalia
  • lakini baadhi ya Hotel za Mji wetu kuna Member tola India alipinga sana hasa kutokana na majina ya Kizungu haikupita lakini kweli zipo

Thank you for your answers. Mjadala utakuwa umefungwa, ni kiasi cha kujua namna gani naweza kusaidia kurekebisha majina ya barabara zinazoonekana kuteleta sense ya hali halisi.
 
Kwa sababu Google ndiyo mtandao mkubwa duniani,na kwa sababu world satellite ndiyo inayoongoza kui-view dunia nzima.Kuna uhusiano kati ya Google na world satellite.

Acha story za vijiweni. World satellite ndo nini? Kama hujui mambo bora ukae kimya.
 
Watu wa tech mkishindwa kumjibu huyu jamaa kisawasawa mtakuwa mmetia aibu sana jukwaa hili! Okoeni jukwaa lenu fasta!

Mkuu si kila kitu ni tech,vingine ni udadisi tu.Hata wewe unaweza kumjibu kama unajua,wewe unaturushia mpira ili jibu likitoka na wewe upate.Hahaha ninapita tu,take easy.
 
Ile ni volunteers ndio wanafanya. Mimi pia nimejianga. huwa wanaitwa Google map maker. Unakuwa una name streets, pinpoint business au buildings. Kwa Street View Maps nadhani bongo bado
 
Back
Top Bottom