Good News ! - Kampuni ya Precisionair kuingiza ndege saba mpya Tanzania

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Ifuatayo ni habari njema kwa Watanzania, adha ya usafiri wa anga natumaini itapungua sasa..

Source: Mwananchi.co.tz

SteveD.
 
Nadhani itapendeza sana kuwa na ndege nyingi, huenda na nauli zikashuka. Inabidi jamaa wajikongoje, wawe kama Easy Jet, ama Sterling, kwa kutoa huduma kwa bei rahisi.
 
Nadhani itapendeza sana kuwa na ndege nyingi, huenda na nauli zikashuka. Inabidi jamaa wajikongoje, wawe kama Easy Jet, ama Sterling, kwa kutoa huduma kwa bei rahisi.

kazi kweli. hii itakuwa changamoto kweli.
 
Hizi ni habari nzuri!

Naskia sasa Hili shirika ni la pili kwa umaarufu na ukubwa ktk E and C Afrika baada ya Kenya Airways!

Hii ni poa tu.. nawapongeza!
 
Hongera Precision Air! Huduma bora ya kiwango cha juu inaonyesha kumjali mteja. keep it up!
 
Wakuu hii ndo ya kwanza ATR-72-500 Brand New hiyo. Ndo ilitua tarehe 3 March mida ya sa 3 unusu asubuhi DIA kutoka Ufaransa. Hongereni Precision ila nauli mpunguze
 
Attachments

  • Precision New ATR 72.jpg
    33.7 KB · Views: 70
Wakuu hii ndo ya kwanza ATR-72-500 Brand New hiyo. Ndo ilitua tarehe 3 March mida ya sa 3 unusu asubuhi DIA kutoka Ufaransa. Hongereni Precision ila nauli mpunguze

Mbona ukiangalia imeandikwa Rombo Ubavuni??? Kwani Rombo ni nembo ya bishara ya hii kampuni?
 
Heshima mbele wakuu!
Nivigumu sana kununua ndege mpya,na nivigumu saana kushikilia soko lako,kuliko kupata jipya,nawapongeza hawa pw(precision)kwa mafanikio hayo yao,mind you wanaingiza boing nyingine end of this moon,lakini pia,wanaingiza ndege nyingine mpya kabisaa yaani brand new ATR72-500,
Nahapa ndipo kwenye somo kwa hawa ATCL,kuna advantage za kutumia hizi ndege za kifaransa,kuliko boing ama air bus,katika fuel consumption,ntakupa mfano rahisi kidogo,safari moja ya atr72,kutoka dar kwenda kigoma kupitia shy na tabora,na kurudi ni sawa na safari ya boing kuto dar kwenda mwanza pekee,bila kurudi,pia ukiangalia na idadi ya wasafiri wetu watumiao ndege,unaona atr ni bora kwetu kuliko ma airbus na hizo boing,haina maana kwamba pw walishindwa kupata boing,ama airbus,lakini waliangalia mbali zaidi kuliko wakina mataka,na dialo,ni matumaini yangu kua wamejifunza somo muhimu toka precision,
Once again,bravo kwa management ya PW na Wafanyakazi wote wa PW maana bila wao kusingekua na hayo muyaonayo mafanikio,one more thing,Nauli jamaani,punguzeni japo kiduuchu,tujimwayemwaye nasie kina yakhe,
LONG LIVE JF!
 
nasikia atc nao wameshusha kitu aina ya dash8 toka canada, chakushangaza imeenda sauz kupigwa chata! sasa kama ni mpya singepigwa chata kiwandani? au nisekandihendi? isijetuua bure!
 
nasikia atc nao wameshusha kitu aina ya dash8 toka canada, chakushangaza imeenda sauz kupigwa chata! sasa kama ni mpya singepigwa chata kiwandani? au nisekandihendi? isijetuua bure!

hapana Eddy,ile ndege dash 8,sio mpya,na ilishawahi kufanya kazi hapahapa bongo,nahaohao atcl,lakini ikaprove wrong,kwenye viwanja vya changarawe,wameirudisha tena tuone kitakachojiri maana,viwanja nivilevile,hakuna kuilichobadilika,yawezekana ni sehemu ya ufisadi,maana ni ndege cheap kwa kukodi.
 
Hivi kuna mtu anajua bei ya hii ndege mpya ya PW? Je wamechukua mkopo Benki au ni faida ya kukua kwa biashara?

Hivi nini kifanyike nayo ATC ifufuke iwe ktk chart kama PW?

Hivi kuna ndege zinaenda Mbeya kwa sasa? Hivi ule uwanja utakamilika lini?
 
Thamani ya ndege mpya ya pw ni dola m17.4,na nisehemu ya faida na mkopo wa citibank,ambayo itaiwezesha pw kupata ndege saba mpya,mbili kila mwaka,kuanzia mwaka huu,pia ni ubunifu wa management ya pw,determinations,na vision yao,nawajua viongozi wa pw,nawale wa ATCL,lakini hata kwa mazungumzo yao tu utaona tofauti zao,kusema ukweli atcl ya mataka,inasafari ndefu saana,time will prove me wrong!
 
Mbona ukiangalia imeandikwa Rombo Ubavuni??? Kwani Rombo ni nembo ya bishara ya hii kampuni?

Ahh, unajua Mzee wa Rombo (Shirima) alikuwa initial owner, baadae ikaja kuwa-acquired, lakini bado ana-own majority share ya Precision, ndio maana anatukuza kwao eti, wouldn't you?
 
Sidhani kama hizo ndege zilikuja zote.

Thanks Magezi kwa kufufua mada.... Labda tuwaulize walio karibu na jikoni,

A few days ago tulikuwa Mwanza tukiugulia jinsi ya kupanda ile Dash-8 ya ndege yetu ya Taifa, lakini hatukuwa na cha kufanya kwani nege mbadala kwa siku ile ilikuwa ATR42 ile isiyo na AC bomba....

On a positive note, ATR 72 iko poa sana na kwakweli ni ndege iliyotulia, pia wana boeing inayosaidia japo huenda mwanza mara tatu kwa wiki kama sikosei
 
Hizi ni habari nzuri!

Naskia sasa Hili shirika ni la pili kwa umaarufu na ukubwa ktk E and C Afrika baada ya Kenya Airways!

Hii ni poa tu.. nawapongeza!

Mkuu nakuunga mkono kuwapongeza Precisionair; lakini hebu tusiongeze chumvi kusema wao ni maarufu zaidi ya Ethiopia Airlines katika E & C Africa.

Wakuu hii ndo ya kwanza ATR-72-500 Brand New hiyo. Ndo ilitua tarehe 3 March mida ya sa 3 unusu asubuhi DIA kutoka Ufaransa. Hongereni Precision ila nauli mpunguze

Nadhani itapendeza sana kuwa na ndege nyingi, huenda na nauli zikashuka. Inabidi jamaa wajikongoje, wawe kama Easy Jet, ama Sterling, kwa kutoa huduma kwa bei rahisi.

Wakuu,

Kweli hili la kutaka wapunguze nauli ni kama mnawaonea tu. I am just thinking aloud here....watapunguzaje nauli wakati

1. Ndege hizi wamekopa na wanatakiwa kulipa mikopo, riba na wapate faida.

2. Viwanja vya ndege Tanzania vingi ni vibovu na hivyo kuongeza gharama za service na matengenezo mengine ya mara kwa mara kwenye ndege zao.

3. "Karibu" kila aina ya spare part ya hizi ndege inaagizwa nje ya nchi kwa kutumia USD.

4 Gharama za kufundisha rubani, mafundi na wahudumu wengine ziko juu (nje ya Tanzania - mara nyingi South Africa) na iko siku itawalazimu kutoa "experts" ng'ambo.

5. Precisionair wamejitosa kiume kupanua biashara ingawaje soko la kujaza kujaza ndege zao kila trip halipo hivyo hao abiria wachache waliopo ndio wanaendesha biashara...

6. Sasa hivi ni kama wana-monopoly kwenye hii biashara ndani ya Tanzania...ni mfanyabiashara gani ambaye hatatumia mwanya wa monopoly kujiongezea faida kwa kadri awezavyo.

Kwa kumalizia, hii changamoto kwa Watanzania; siku tukiamua kufanyakazi kwa bidii, nidhamu na maarifa tunaweza kuendesha biashara kubwa na kujenga uchumi wetu bila kutegemea kuomba omba kwa nchi yoyote.

Hongera sana Shirima na Timu nzima ya Precisionair; you make us proud.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…