Gombe National Park

ni maisha ya kuishi porini flani hivi maana gombe ni kisiwa kilicho katika ziwa Tanganyika, kimaslahi sijui yakoje.
 
Kafanye kazi wewe TANAPA wana kisu kikali, hakuna hata park moja iliyo Mjini hivyo tegemea kuwa maporini na kuwa karibu na Masokwe kila siku.
 
Kaka usijali wewe nenda tu ukafanyekazi jitume, kuwa mtiifu na mchapakazi. Hivyo vyote kwa pamoja vitakuwezesha kuhamishiwa unakopapenda zaidi. Pamoja na hili maisha ni vita murrra pambana, usichague.
 
Mimi nilianzia kazi kijiji mtiriangu huko kondoa , baada ya miaka mitatu nikahamia Itiso huko huko Kondoa na kukaa miaka mingine minne. Sasa hivi nimepenyeza niko mitaa ya posta (DSM). Kwa hiyo unahitaji uvumilivu. cha muhimu ni kukaa kimkakati zaidi usijisahau utafikia sehemu unayohitaji. Uwe mvumilivu we nenda kachape kazi tu
 
ni maisha ya kuishi porini flani hivi maana gombe ni kisiwa kilicho katika ziwa Tanganyika, kimaslahi sijui yakoje.

nipo Kigoma kikazi na kesho naenda kutembelea Gombe. Gombe sio kisiwa ila ni mwambao mwa ziwa Tanganyika. Vijiji vingi vya mwambao mwa ziwa Tanganyika havijaunganishwa kwa barabara kutoka Kigoma mjini ndo maana usafiri wake asilimia kubwa wa majini. Maisha ya kule ni pori kama National Parks zingine.
 
ni maisha ya kuishi porini flani hivi maana gombe ni kisiwa kilicho katika ziwa Tanganyika, kimaslahi sijui yakoje.

Ndugu yangu unapaswa ujifunze jiografia ya Tanzania. Gombe National Park siyo kisiwa, na wala haiko ndani ya ziwa Tanganyika, isipokuwa hifadhi inapakana na ziwa Tanganyika, au iko ukingoni mwa ziwa Tanzanyika kwa upande wa Magharibi. Angalia ramani ya hifadhi za taifa hapa http://www.tanzaniaparks.com/tanzania_map.htmlhttp://www.tanzaniaparks.com/tanzania_map.html
 
Mkuu ulitakiwa kutafuta information za mapori/hifadhi za taifa kabla ya kuomba kazi. Hifadhi zote ni mapori isipokuwa makao makuu yake tu, huko Arusha. Nakushauri nenda kachape kazi kwani kuna uhamisho wa mara kwa mara hutokea yawezekana baada ya muda ukahamia hifadhi kama za kilimanjaro, manyara na arusha.
 
thanks very much for the advise guys am in dsm my salary here is low there im going to get double of what im getting here
 
thanks guys for the advise for the advise
.nilishaenda gombe 2 timesnajua uaogopeshwa kuwa kgma kuna uchawi.mim nilikaa 12 yrs bila tatizo.gombe ni park nzuri.usafiri ni boti mnatumia masaa 2 na nusu frm kgm. Ni green place na utapenda kukaa kule.
 
Gombe ni pazuri kwavile hata watalii wanapendelea kwenda kwa wingi. tatizo la muda ni kuwa redio utakayoipata ni ya burundi na mawasiliano ya simu ni radio call. niliambiwa airtel walikuwa na mipango ya kuwapatia mawasiliano huko. hata hivyo usikate tamaa kwavile shopping yote inafanyika kigoma mjini na wanazo boti zao.
 
mh...if you are single go and work make money then fanya michakato ya kutoka kabisa TANAPA watu wengi tumeacha mazingira magumu sana hasa ukioa alafu mkeo anafanya kazi town .Hamna ruhusa mpaka mwaka upite ndo uchukue likizo . watu walio na wake zao huko porini wamewaoa vijijini huko huko other wise mkeo akubali kuwa house wife !! Hakuna off days , pori pori jamani acheni nyinyi ..kisu kipo lakini maendeleo huwezi fanya coz upo porini angalia usiwe mlevi kwa frustrations kama wengine . and for your info ukioa work mate wana wahamisha kuwatenganisha . Trend ya AIDS kwa Tanapa inatisha .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom