Gold Digging? ? Wanamme ni Kiboko . . .

." Kutia mimba si kazi, kazi kulea mwana.

kutia mimba ni starehe na sio majukumu and thus why mimba nyingine zinakuwa out of plan ya hao wanaojistarehesha. cha ajabu sana ni baadhi yetu sisi wanaume kukataa kulea watoto waliotokana na starehe zetu
 
Reactions: BAK
Kwa vyovyote tutakavyoamua katika hali kama hii, ni jambo la muhimu kufikiri kama wazazi.... na kwa hiyo kama wapenzi wa watu wengine sasa au in the past...!!

Namshauri Nyamayao na wengine wenye issues na wazazi wao wawasamehe mara moja....

Kwani sisi wenyewe hatujawahi kuwatenda wapenzi wetu? Na what if katika kuachana nao tuliwaachia majeraha ya kudumu ikiwemo watoto??

cc: King'asti, BAK, Mkirua, Kongosho, watu8...

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:

dah!
shemeji umeongea pwenti mpka vinyweleo vimestand up!
dah!:A S 41:
 
Mkuu Dark City...Juzi kazini wakati nawajibu akina Nyamayao, King'asti na mkundeoriginal kupitia PM maana kwa sisi watatu Nyamayao aliamua kutushirikisha kwa pembeni na watu waliandika michango mizuri sana. Rafiki yangu kipenzi na pia ni office mate (tumetokea kuelewana sana) akapita kunisalimia akaniuliza unafanya nini maana aliniona niko busy kuandika kwenye pc. Nikamwelezea kuhusu discussion yetu halafu nikakumbuka naye ana situation kama hii ila Baba yake bado kaingia mitini tangu akiwa na miaka mitano. Tangu tuwe marafiki siku zote humzungumzia mama yake tu. Basi siku moja ndio nikaamua kumuuliza siku zote huwa unamzungumzia mama yako tu baba yako yuko wapi!? Akanijibu Baba alitukimbia tangu nikiwa na miaka mitano hivyo sijawahi kumtafuta hata yeye kututafuta. Nikamweka kwenye kiti moto kwa kutumia huu mfano wa Nyamayao. Nikamuuliza baba yako sasa hivi tuseme ni mtu mzima labda anaishi maisha ya shida anaamua kukutafuta na kufanikiwa kukupata na kuelezea matatizo yake aliyonayo kimaisha na kukuomba msamaha kwa kuwatelekeza na pia kukuomba msaada, je utamsamehe!? Jibu lake lilikuwa kama kweli amebadilika (hakufafanua kubadilika kivipi) naweza kumsamehe. Sikutaka kuendelea tena na mjadala wetu maana jamaa huwa anabadilika sana akimuongelea Baba yake nadhani mpaka leo hii bado inamkosesha raha sana, hivyo nilipomuona amebadilika nikaamua kubadilisha topic.

Kwa hiyo kwenye hili inaweza kukujia roho ya kibinadamu kumsaidia kwa namna moja au nyingine lakini bado utakuwa na usongo hasa ukikumbuka mama alivyokuwa anahangaika ili kuhakikisha mnakula vizuri, mnalala mahali pazuri na kupata elimu nzuri. Wako wataosamehe na kuamua kutoa msaada na wako ambao watasemehe bila kutoa msaada na wako ambao kamwe hawatasemehe.

 
Last edited by a moderator:

May be I am missing something.

Kwani ni lazima mzazi wa namna hiyo akutafute kwa ajili ya kutaka misaada kutoka kwako?

Na suala la kuwasamehe waliotukosea tunaliongeleaje?

Babu DC!!
 
sijui kwa nini nimeifungua hii topic... Wababa wa kibongo mtihani sana mpaka unakua hakujui,hajui kula yako hajui soma yako afu ukishajielewa kidogo tu utamuona huyoo kajileta na shida aaaaa sijui wa kizungu wapo hii?Embu nikagombanie zangu daladala mie sahivi.
 

Mama mkatoliki mkamilifu na ile sala ya baba yetu unasalije?especially mstari unaosema utusamehe makosa yetu kama na sisi............!ulishakaa ukautafakari na kuuelewa?
 
waweza msamehe akakutwisha majukumu mpaka ujute kumfahamu. haya mambo we acha tu, yanaumiza kweli kweli. pole my dear ila tu jitahidi kuretain furaha yako kwa gharama yoyote.

No at times sio kwamba anataka msaada huwezi jua ana regret nini ndani ya roho yake just find a place in yu to forgive him no matter what he did or didnt do he is still a father msamehe tu
mbona kila siku twamkosea huyu Mungu wetu ila anatusamehe,
Find away to forgive him thow its not as easy as am writting
 
Mama mkatoliki mkamilifu na ile sala ya baba yetu unasalije?especially mstari unaosema utusamehe makosa yetu kama na sisi............!ulishakaa ukautafakari na kuuelewa?

You have said it....Kwanini kushikilia watu wenye dhambi zao wenyewe huku ukujiongezea mizigo wewe binafsi?
 
May be I am missing something.

Kwani ni lazima mzazi wa namna hiyo akutafute kwa ajili ya kutaka misaada kutoka kwako?

Na suala la kuwasamehe waliotukosea tunaliongeleaje?

Babu DC!!

Na hata akihitaji msaada, ni msaada kiasi gani atakaouhitaji hadi uone ugumu wa kusamehe kisa utafilisika wa kumsaidia mzazi wako? Wengine wako njema na wana maisha yao wanahitaji tu ile harmony. Na je sisi ni wangapi tunawakosea? Kama hatuwakosi wao, je ni mangapi tunamkosea Mungu? Akiwa kama sisi je kuna atakayepona?

Ceteris Peribus unashindana na mtu ambaye keshaafikia saa moja unusu usiku wakati pengine wewe ndo kwanza unaitafuta saa saba mchana!
 

Tuko ukurasa mmoja.

Kuna kitu watu hawataki kukielewa. Kwa wanaume wengi, ukishakorofishana na mke inakuwa vigumu kuwa karibu na watoto. Kwa uzoefu wangu, ndiyo maana nilishaamua kuwa ndoa yangu ikivunjika leo, nitakuwa tayari kuishi kiseja ili mradi nilee wanangu kwa mikono yangu.

Babu DC!!
 
Mama mkatoliki mkamilifu na ile sala ya baba yetu unasalije?especially mstari unaosema utusamehe makosa yetu kama na sisi............!ulishakaa ukautafakari na kuuelewa?

sasa msinilaumu jamani, ni roho yenyewe inagoma, niilazimeshe kumfurahisha mzee wakati rohoni naugulia?
 
Hivi mnajua ni kwa nini baba na mama zenu hawakuweza kuishi na kuwalea wakiwa pamoja na kuwabwaga.Je mnadhabni mama zenu wanaweza kuwaambia kila kitu??Somettimes makosa huwa ya mama zetu ingawa mara nyingi hupenda kusema kwamba baba zetu ndiio walikuwa wenye makosa kwa sababu tu muda huo wanakuwa hawapo karibu kuweza kujitetea,tusipende kuwalaumu wababa kila wakati na kwa kila kosa,muwachunguze mama zenu je ?walikuwa wapo fair kipindi cha mahusiano yao yaliyopelekea wewe kupatikana au kuzaliwa??????NINA EXPERIENCE NA HILO JAMBO,WAMAMA WENGINE WALIKUWA JEURI KIIPINDI CHA USICHANA WAO NA HUWEZA KUMFICHA BABA KWAMBA ANA MIMBA YAKE,NA MWISHO WA SIKU ANAKUJA KUKULISHA UPEPO KWAMBA BABA YAKO ALIKUTEREKEZA ULIPOKUWA MIMBA!!1
 
Je mna uhakika baba ni lofa?
what if baba ni millionaire?

the boss uko sawa kabisa...hako kabinti mwanzoni kalichomoa na kumkandia huyo mshua...nafikiri kalipogundua mshua yuko vizuri akaona bora kakubali.....kwa akili ya haraka unafikiri kama jamaa angekua mchovu kasinga kubali.
 

ugomvi wa mama na baba hausiani na watoto, wewe kama mzazi ni jukumu lako kumlea mtoto. hata kama mama alikuwa ni mbaya kiasi gani baba asiache jukumu lake na watoto wakikuwa watajua tu mwenye shida ni mama au baba. ila ukiwatupa kabisa wewe ndio uko na shida. nimeona hii kwa baba yangu mkubwa pamoja ya kwamba alitengana na mkewe, mke aliwalisha watoto maneno ya chuki sana ila baba mkubwa hakuacha jukumu lake la kuwa baba leo hii watoto ni wakubwa wamejua mama yao ndio yuko na shida na wanampenda na kumtunza baba yao vizuri sana.
 
Mtoto kafanana na Baba, hata DNA isipo hitajika amna shida.
 
kuna watu wana mioyo ya ajabu sana yaani unamuacha mwanao bila hata kumsalimia kwa miaka zaidi ya 20,dah kweli watu tumeumbwa tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…