Wakuu
Hawa magamba ni wahuni wa kupitiliza wamepiga risasi hewani baada ya makamanda wa CHADEMA kushtukia masanduku waliyokuwa wanataka kuyaingiza kwenye chumba cha kura ili wachakachue, cha kushangaza polisi inawakamata wana CHADEMA pamoja na gari ya LEMA wanaacha wezi.
Cha kushangaza zaidi matokeo kwenye vituo vyote yalikuwa yamebandikwa saa 12 jioni na vituo vikubwa vilikuwa 2 ambavyo viko umbali wa ka mita 600, ka hiyo usafiri hata kwa miguu ni dakika zisizozidi 10, lakini majumuisho ya hivyo vituo vikubwa 2 ( vinavyobeba vituo vidogo 39) yalichukua zaidi ya saa 4 yakatangazwa usiku wa saa nne na nusu.
Nasikia walipanga jana wamkamate nassari na Lema baada ya huyo mwehu wa ccm kupiga risasi juu ili watu wawafuatilie polisi na ccm wapate nafasi ya kuchakachua, ila jana Lema na nassari wakawa wanatumia boda boda kuzungukia vituo kwa hiyo wakachemka.