Godwin Mwalusamba [M-NEC Arusha] afyatua risasi Daraja 2 Arusha

ngurati

JF-Expert Member
Feb 14, 2011
221
240
Aliyekuwa mkiti wa #UVCCM wilaya ya Arusha na kwa sasa MNEC, Dan Mwalusamba amedaiwa kufyatua risasi hewani huko Daraja mbili Arusha ili kutisha wananchi waliokuwa wamekusanyika kulinda kura katika shule ya Felix Mrema.

Inadaiwa polisi walimshikilia lakini cha ajabu akipigiwa simu anapokea, sasa sijui inakuaje anakuwa na simu sero. Hii ilikuwa ni baada ya ccm kubanwa kisawasawa na makamanda na wananchi wa Arusha katika uchaguzi mdogo aw udiwani ambapo mwisho wa siku CDM imeibwaga ccm vibaya na kwa kura za Aibu.

Ikumbukwe kata hii ilikuwa ni ya CCM, Diwani aliyefariki alikuwa wa CCM. Polisi acheni double standards. Dereva wa Lema na watu wengine kadhaa wameshikwa wakiwa wanna patrol ndani ya gari la Lema kitu ambacho sio kosa lakini anayefyatua risasi anaendelea kuchonga kwa simu.

Iko Wapi Kweli?
 
Uhuru ni gazeti linalomilikiwa na CCM, UNATEGEMEA NINI HAPO???. hushangai magazeti mengine yote ambayo ni credible na yanaheshimika hayajaandika? Taarifa zinasema Gody Mwalusamba amekiri lakini akasema alikuwa anajihami baada ya kuona Wafuasi wa CDM ni wengi kuliko wa CCM. Nassari alikuwa Arumeru Magharibi - Bangata.
 
Nassari alifungulie mashtaka Hilo gazeti.Babu yangu hulitumia kuvutia tumbaku baada ya kugundua linampotosha.
 
Inasemekana hivyo. Yule mdada alikua amekufa lakini akiwa anatabasamu!!.

Inasemekana pia kua huyu jamaa anatumiwa na RIZIone kwenye biashara ya magari ya kukodisha. Wanadai sio yake ni ya Riz.

Labda ndo anakopata jeuri kama ni kweli.

Ya kweli haya...ila la kutumiwa na riz1_sina shaka nalo kabisa,....maake lo
 
HUyu Riz1,iko siku mtasema hata Urais ni wa kwake amemtuma JK amuongozee!
 
Mnajua namna ya kuandika !Wakati even mtoto wa std 1 anaweza ku konnect dots.wewe tiririka tu usiogope,man'ake hapa pamekuwa kama kijiwe cha kahawa kila kitu mnamwaga tu,We need great thinkers sio waimba mchiriku!
 
Back
Top Bottom