Godwin Mwaipongo mpinzani wa Tundu Lissu TLS, alishawahi kugombea kupitia CCM

Asante kwa utafiti mzuri Mkuu. sasa wapinzani wa Lissu tafuteni propaganda nyingine.
 
Yaani Mtukufu kila mahali anataka kuweka kada.. Na kwa vile inaonekana hata waliostaafu nafasi yake wanamgwaya kumrekebisha, basi tujiandae kwa mabovu mengi yanayokuja mbele yetu..
 
Kwani Rais aliposema kua wanasiasa wanataka Uongozi Kwani akili yenu mnazani alimlenga Lisu, kwanini msizani alimlenga huyu wa CCM.. Ni ujinga wenu kuzani kila jambo linawahusu nyinyi, kila vita ambayo Rais anapambana nayo mnasingizia inahusu Chadema ni ujinga sana

Rais alipoingia madarakani, alianza kutumbua, chadema wakatoka barazani kua anatumbua watu waliounga mkono Chadema au watu wa kaskazini

Alipokataza maandamano, mkasema nayo wamelengwa Chadema

Walipoanza kushughulikia watu wa madawa, mmesema inalengwa Chadema kisa katajwa Mbowe, wakati Manji, azani, na Kina Wema ni CCM, ujinga..

Wamekataza viroba tena mnasema wanalengwa Chadema

BAHALULI NYINYI
 
Ila kusema kweli kama ni rais tumempata! Yaani rais anatamka hadharani kuwa akiletewa mapendekezo ya kuteua jaji kutoka upinzani hata teua? Kwa hiyo majaji kumbe huteuliwa kwa imani za kisiasa na ni lazima awe ccm?
 
Marehemu babu yangu Eng.Dr Peter Komba alikua wizara ya ujenzi miaka hiyo kabla ya kukumbwa na kashfa ya rushwa yeye na wenzake akina Kiula.
Nilimsikia akimwambia msure maneno haya...
“Huyu kijana Magufuli hafai kabisa simpendi, anajifanya mjuaji kwenye mambo ambayo yanahitaji utaalam anachokitaka yeye ndicho anataka kiwe hata kama kitalaam siyo sahihi” babu aliendelea kusema “ni mnyanyasaji,mtu wa visasi na mwenye kiburi sana, hapo alipo ni Junior tu imagine akiwa senior!?!?”
“huyu kijana akija kupewa mamlaka makubwa, atalewa sifa na kuharibu kazi za watu”

Ilikua mwaka 2002 one year later he passed away.
13 years later jamaa akashinda uchaguzi fair au kimagumashi it doesn't matter... Lakini a year and few months later baada ya kua raisi maneno ya babu yamepata uhai.
Aliyokua akimwambia msure ndio yanayo tokea sasa.
Babu huko aliko atakua anajisemea “nilimwambia kijana , angalia kinachotokea”.
 
Uchaguzi wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika TLS umevutia hisia za wengi ikiwemo Waziri wa Sheria na Katiba Harrisson Mwakyembe kutoa tishio la kuifuta TLS na hii hapa ni Kauli ya Mh. Rais kuhusu habari za uchaguzi wa Tanzania Law Society


source: Khelef Nassor
 
Back
Top Bottom