sio chuki binafsi ni kweli anaongea kwa wawengewenge sana hatulii
Sio jibu hili Suzie.
majibu yenu ni ya kitoto wote nyie
Lazima utakuwa na chuki binafsi pole
Umenisemea yoote. Hapa si swala la usomi, kiukweli hana 'talking and listening skills'. Kwa hakika mimi huzima TV au kubadilisha channel kila ninapomsikia. Kinachoniudhi ni yeye kujihisi yuko sahihi na 'bora kabisa' pale anapotangaza. Anayebisha hebu ajaribu kumfuatilia ...
jamani katika vipindi vya mahojiano vya tv za tz hakuna mtangazaji wa hovyo kupata kutokea kama gabriel zakaria, hiki ni kimeo hasa, kama gondwe hafai hujui hapaswi hata kusogelea kamera ama kipaza sauti ya chumba cha habari, ni mbumbumbu, ni mbabaishaji, mtu mwepesi , anaehoji kwa kutanguliza majibu, hahhaaaah tbc wamemtoa wapi huyu mjamaa
semeni yote lakini nawakubali sana hawa watangazaji wa ITV kuliko wa clouds fm/tv....sababu ni moja tu they are real....they dont pretend. keep up gg and your team.
Lazima utakuwa na chuki binafsi pole
umeona uso wa huzuni sauti ya kicheko wapi na wapi jamani? kicheko shurti kitanguliwe na smile bwana anaboaKicheko chake ni chakuungaunga kinaboa sana
Mtoa hoja ana pointi ingawa labda katumia maneno makali kidogo................GG ni mtangazaji mzuri wa vipindi fulani fulani, nadhani mahojiano kama ilivyo kwa waandishi/watangazaji wa kibongo ni tatizo. Swali linakuwa para mbili.
- Ushauri GG acha hiyo ''synthetic voice'' kutaka kujitumumua sana, hata kama wewe una umbile dogo huna haja ya kujitumumua sana, maana watu wanapokusikia kwa radio au TV halafu wakikuona live wanashangaa jinsi ulivyo mdogo kulinganisha na unavyojitumumua studio
- Soma sana court proceedings ujifunza kuuliza maswali kwa ufupi na ufasaha
umeona uso wa huzuni sauti ya kicheko wapi na wapi jamani? kicheko shurti kitanguliwe na smile bwana anaboa
Jamani tuwe wa kweli, huyu kijana ana juhudi ya kazi na nasikia ni msomi wa hivi vyuo vyetu vya kata, lakini hana kipaji cha utangazaji jamani.
Anajaribu kuiga ma cow boy wa movie za kimarekani, kicheko chake ni very artficial he is a bad actor, hata kwenye lile tangazo la promotion alilovalishwa suti mpya, lakini bado kicheko kinachafua, halafu naomba Joyce japo husikilizagi la mtu, msimpange kwenye mahojiano hana technique mtu huyu, anaongea zaidi ya mgeni, hana uvumulivu hayuko organized maana anauliza kila kitu wakati mmoja na maswali yake sio maswali ni maelezo ya anachokijua yeye juu ya hilo swala, anaingilia mszungumzaji anauliza maswali mengi wakati mmoja na hajui kufuatilia kama lipi limejibiwa lipi halijajibiwa. Anawezakana ni mwanahabari mzuri lakini sio mtangazaji mzuri especially kwenye TV.
Kwa nini msimuache aka concentrate kwenye u MC wa BSS na taarifa ya habari? hata ninapoongea sasa yuko kwenye kipindi ch akumekucha anazoza yeye hata mzungumzaji hatujui kamuitia nini studio maana angeongea yeye tu
Yani huyo gamba anamuigiza maulid kitenge...
Ila honestly wanapaswa kuchange na ku specialize sio kubangaiza tu wajifunze kwa wenzao.... Mfano Richard quest means business na Dr farid Zakaria ni coverage ya kitaalamu na unaenjoy.....sasa Kama Mtu Ana masters then you cannot tell the difference on what he deliver....you don see creativity and changes unategemea nini....
Nadhani tujiulize ni kwanini Mtu mmoja anafanya coverage kwenye Sheria , biashara , uchumi na vinginevyo hili ndilo linalosababisha dharau....
Unajua ukiwa kwenye field uko sawa nadhani no one will concentrate on sauti,kicheko na vinginevyo...ni challenge kwa wote Kama Angekua anakua objective kwenye Topic hakuna ambae ange concentrate on his voice and kicheko chake... Sasa Hawa watangazaji wetu wanajikita kwenye facial , scrub na Mavazi lakini delivery Zero...
Wabadilike ndio Maana wengi wanawadharau na kuona kua they just fake
Mimi sipendi staili ya utangazaji na uulizaji maswali ya yule wa dakika 45. Sijui ni jinsi kipindi kilivyotengenezwa kipropagandapropaganda ama ndio kupwaya kwa mtangazaji mwenyewe.