Godbless Lema: Pesa aliyolipwa Bilionea Laizer ni pungufu sana, ungefanyika mnada angelipata karibia mara kumi ya alicholipwa

Biashara ni makubaliano, BOT/Serikali wamewekeza mtaji wao lazima faida itapatikana ili hii nchi ifaidike kuendelea kuleta maendeleo yenye tija kwa Watanzania.

BTW Lema amekuwa mtaalam wa madini, mbona hakusema bei yake basi tufahamu na kutueleza hiyo bei ni pungufu kwa kiasi gani? Ndio majungu yenyewe na Propaganda hizo.
Serikali imewekeza kwenye nini?

Ilikuwa inamsaidia huyo masai gharama za kuendesha mgodi wake?!

Au serikali imewekeza kwenye kujenga ukuta!.
 
Huenda kuna ukweli. tusubiri muda utasema maana hesabu hazidanganyi

Haihitaji kusubiri muda useme. Una smartphone angalia bei ya mawe sokoni utajua ukweli. carat moja inaenda shilingi ngapi?

Kilo moja ni sawa na carats 5000.

Saniniu's Tanzanite in 14kg sawa na 70,000 carats.

Bei ya soko kwa carat moja inakwenda kuanzia dola za kimarekani 300 hadi 425.

Mawe yote ya Saniniu hayawezi kuwa pure stone worth market price. Tuseme tukate kilo tano kama magonga au taka (kumbuka gonga waweza uza pia) zinabaki kilo 9 sawa na carats 45,000 ambazo ukizidisha na kwa tuseme dola 350 unapata dola million 15.75 sawa na billion karibia 33 za kitanzania.

Naunga mkono serikali kusimamia sekta mbalimbali na kuimarisha ukusanyaji wa kodi kwa maendeleo ya nchi.

SIUNGI mkono serikali kufanya biashara hata kidogo, serikali inatakiwa tu kuunda mifumo imara ya kusimamia biashara na shughuli za kiuchumi.
 
Biashara ni makubaliano, BOT/Serikali wamewekeza mtaji wao lazima faida itapatikana ili hii nchi ifaidike kuendelea kuleta maendeleo yenye tija kwa Watanzania.

BTW Lema amekuwa mtaalam wa madini, mbona hakusema bei yake basi tufahamu na kutueleza hiyo bei ni pungufu kwa kiasi gani? Ndio majungu yenyewe na Propaganda hizo.

Lema amekuwa kwenye biashara ya madini muda mrefu, hasa hayo madini vya Tanzanite, hivyo ana ufahamu wa kutosha kuhusu biashara hiyo ya madini. Sio lazima alichokisema kiwe kweli, lakini ana ufahamu wa kuridhisha wa biashara hiyo. Kama ni kutaja kiasi, amesema ingeweza kulipwa mara kumi zaidi ya alicholipwa.
 
Nishaelewa wanataka wamshawishi ajiunge Chadema ili wapige hizo hela kwa kupitia michango akiwa kama mwanachama hizi ni harakati za kumnasa huyo jamaa tayari weshaona fursa hiyo.
 
Huyo mwuzaji alishafuatwa sana auziwe zaidi ya hiyo pesa,nadhani jamaa aliangalia zaidi usalama,kwamba hela serikali ina usalama zaidi,maana watu binafsi au makapuni unaweza kutapeliwa pia

Mkuu serekali haiwezi kukutapeli? Rejea mkulima wa ndege nk.
 
Lema amekuwa kwenye biashara ya madini muda mrefu, hasa hayo madini vya Tanzanite, hivyo ana ufahamu wa kutosha kuhusu biashara hiyo ya madini. Sio lazima alichokisema kiwe kweli, lakini ana ufahamu wa kuridhisha wa biashara hiyo. Kama ni kutaja kiasi, amesema ingeweza kulipwa mara kumi zaidi ya alicholipwa.
Niliwahi kusema hizi siasa za kudandia dandia kila hoja hazina mashiko hizi lakini bado hawaelewi.
 
Nishaelewa wanataka wamshawishi ajiunge Chadema ili wapige hizo hela kwa kupitia michongo akiwa kama mwanachama hizi ni harakati za kumnasa huyo jamaa tayari weshaona fursa hiyo.

Sioni tatizo la mtu kushawishiwa kujiunga na chama chochote kwa hiari yake. Hata hivyo kama anahitaji kujiunga na chama, bado hawezi kujiunga na cdm, kwani nchi zenye mirengo ya kikomunisti, huwa zinasonga matajiri na kutowaacha kuwa huru. Na ikitokea akajiunga na cdm, ni lazima atafililisiwa kwa kufanyiwa mizengwe.
 
Back
Top Bottom