Wateja wapo wengi, Ongeza thamani ya kitu unachotaka kukiuza kabla hujakitangaza kukiuza

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
6,939
22,989
Kila siku tunalia biashara ngumu sawa biashara ni ngumu kama hautojiongeza kwendana na wakati wa sasa unataka nini,usipoelewa wakati unataka nini basi "wakati" utakuelewesha unachotaka.

Lazima tutambue kuwa wakati uliopo sasa watu karibia wote ni "wabahili" usijidanganye ukiona mtu anaagiza kitu dukani/mahali halafu haulizi punguzo ukafikiri ni kweli yupo hivyo kwenye kila kitu,huo ni uongo na zuga za muda mfupi tu.

Sasa kama kila mtu dunia ya leo ni bahili na mchumi,tufanye nini sisi wafanyabiashara ili hawa watu wabahili "wachumi" tuweze kupata pesa zao kiulaini bila hata kupigizana nao kelele?

ONGEZA THAMANI YA BIDHAA UNAYOTAKA KUIUZA

Unaelewaje nikisema kuongeza thamani?

MFANO NAMBA 1
yawezekana unataka kuuza simu lets say ni samsung uliyoinunua laki 3,unataka kuiuza laki 3 au zidi ya hiyo laki 3,utafanyaje?

Simu yako ina sifa zifuatazo storage 16GB,Ram 4GB,nk ili uiuze hii simu kwa bei nzuri kwakua umeshaitumia basi tuipandishe thamani kabla hatujaiuza utakachofanya ni unaenda nunua external memory 64GB or 128GB `hizi memory sasa hivi zimejaa mitaani hazizidi hata 30,000 kuipata.

Utaenda utanunua wireless earphone 10,000,utanunua wired earphone za kawaida 5,000,utanunua cover mbili nzuri ya kike na kiume zote 10,000,utaiweka simu protector 3D either black or white (unique one). Accessories zote zinaweza kukugharimu kama 50,000Tsh.

Baada ya kuwa na hizo accessories utaipost sasa hiyo simu utaandika List ya vitu unavyouza kwa pamoja na simu yake simu ya laki 3 utaweza andika tangazo kuwa unaiuza 370,000,mteja akikwambia naomba picha unamtumia picha Ya simu ikiwa na makorokoro yote hayo.

Akikwambia nipunguzie bei utampunguzia 20,000 akikupa 350,00 utakua umepata hela yako ya simu + hela yako ya accessories,mteja kimoyo moyo ataona amekupiga na wewe utaona umempiga (amani kila mtu moyoni mwake).

MFANO NAMBA 2
Una gari lako unataka liuza Namba A km inasoma 200,000 kwenda mbele,unataka liuza Mil.4 utaliuzaje?

Hamna pesa inakuja kabla ya kutumia pesa (tambua hilo) hata hilo gari unaliuza leo kwasababu ulitumia pesa kulipata,sasa hili gari lazima tulipandishe thamani kisha ndo tuliweke sokoni.

Utalipiga rangi mpyaaa,unaweza ukalitia sticker kuliongeza nakshi,utaliongeza taa flani mbele na nyuma,Utali pimp kidogooo kubadilisha matairi utaongeza spacer ili uweke sports rim kali kabisa kwakua haya unayafanya ili uuze gari na sio ili ulitumie gari hakikisha hununui kitu kipya vyote hivyo ni used utapata nzuri kwa bei ya chini,

Kama huwezi badilisha rim unaweza nunua zile "plastic Dip" unazipachika kwenye Rim zako, then mwisho utaingia ndani ya gari utafunga mziki simple unaosikika,seat cover utaweka mpya,steering cover nzuri kabsa,Gia kile kichwa nacho badilisha vifanane na stering yako, Yani gharama zote za Gari hakikisha haizidi 1.5M.

Tukija liuza hili gari litakua kwanza lina ng'aaa ukiliangalia tu unajua yes hili gari kweli,japo namba A ila mteja akiangalia tu hata ile namba ilivyo kua designed ipo kwenye kibao namba safi yani kwa bei ya unaweza kuanzia 6M utashuka nae hadi 5.5M trust me atachukua ataona kakupiga na wewe utaona umempiga (ngoma droo)

MFANO NAMBA 3
Una kiwanja unataka kukiuza formula yetu ni ile ile,ili hiki kiwanja ukiuze angalia mahitaji ya msingi ya binadamu kwanza kubwa ni Maji,unachofanya unaweza chimba kisima pale kwenye kiwanja chako,Ukajenga banda la kuku la mabanzi mawili au matatu vizuri kabisa,yani unaweka kiwanja kwenye mkao flani mteja akiangalia tu anashawishika hata kufanya ufugaji au kilimo cha umwagiliaji.

Kisha unaweza panda miti flani flani kwenye kiwanja chako asee trust me hicho kiwanja utakiuza hela nzuri sana kuliko ukiliacha tu eneo liko flat mtu "mpaka wa kiwacja" tu mpaka aende umuonyeshe kisiki umwambie hiki kisiki ndio mwisho wa kiwanja, wakati unaweza panda miashoki ile miti inaota imesimama wima matawi yanalalia chini angle zote za kiwanja chako.

Unakiweka kiwanja kionekane mtu akikiangalia anashawishika kukinunua,kama hela unayo unaweza jenga hata ka rum ka 1 kwenye kiwanja then unakuja uza unajiwekea gharama zote ulizotumia kisha unajumlisha kwenye bei ya kuuza kiwanja chako.

MFANO NAMBA 4
Unafanya biashara ya Duka la nguo,viatu,simu,computer,nk chochote kile ila ni DUKA bidhaa zako zina bei yake kila moja ili uongeze thamani unga au sukari unayoiuza dukani kwako utafanyaje?

gawana faida na wateja wako
Utagawanaje nao faida? dukani kwako sukari kilo unauza 2500 maduka mengine sukari wanauza 2200, usiogope Baki na bei yako hiyo hiyo ya 2500 (hamna kushusha bei hapa) ila sasa usiwe mbinafsi, chakufanya nunua kopo la pipi la ivory au bablish sh 5000 ndani zinakaa bablish/pipi hadi 100,kila mteja ataenunua sukari dukani kwako mpe kapipi ka 1 akawape watoto wake.

Kama mteja kanunua kilo 5 mwambie asante kwa kumpa zawadi ya vipipi awapelekee wanae nyumbani mpe pipi hata 5 mpe (bure) nakwambia mteja atakuona bonge moja la lofa akifkiri kakuweza kumbe wewe ndio umemuweza yeye.Wakija watoto wametumwa kununua kitu dukani kwako hao hakikisha kila mtoto unampa kapipi.

Nakuhakikishia utauza mpk watahisi wewe mchawi,vitu vyako vya bei ila vinauzika (ni akili tu) AU

Unaweza ukawa unauza duka la simu au computer mteja kaja kununua simu ya laki 7 au laki 8 ukiangalia faida uliyoipata umepata laki 2 au 1 na nusu nzima, hivi unapata hasara gani ukimwambia mteja Shika hii ear phone (nakupa bure kama asante) au unashndwa nini kumzawadia mteja zawadi ya Free mouse au keyboard kwa sababu kanunua computer dukani kwako? Huko ndio kuongeza thamani kwenyewe huko.

Unauza duka la nguo,umemvalisha mdoli pale nnje Top ya 20,000 skin jeans 15,000 Jumla 35,000 faida ya mteja akinunua vyote hivyo faida unapata 20,000 Unachofanya ukishajua faida yangu ni 20,000 unatoa 5000 kwenye faida yako,unanunua saa ya kike au cheni unamvalisha yule mdoli pale nnje kisha mteja akija akiulizia unamwambia huyo mdoli kama alivyo bei yake ni 35,000,ataku uliza hadi na hii cheni/saa utamjibu ndio?

Atanunua, si kwamba kanunua kisa kapenda ile nguo ila kavutika na ile ofa ya saa na cheni (si unajua ubahili wa wateja) ataona kakupata ila kumbe wewe ndio umempata.

Asee mifano ipo mingi sana,Muhimu na la msingi wewe kama ni mfanya biashara acha kukariri kuuza vitu kwa kuiga bila kuviongeza thamani,bei haimvuti mteja ila mteja anavutwa na vitu vingi, na wateja wengi wa siku hizi anataka kununua Kiatu apewe na soksi,anunue Fridge apewe na fridge guard ebu tujifunze wa wachina kwenye hizo pochi za kina dada.

Mchina atakuletea pochi kubwa ndani ataongeza kapochi kadogo,ataweka ka mdoli,ataweka ka holder yani hapo point yake ni 1 tu auze ile POCHI wala sio hivyo vikorombwezo vingine,wadada kila siku wananunua mapochi Asee ndugu hamna pochi ya mdada ya chini ya 30,000 ukiingia Dukani,ila mdada ukiingia room kwake ana mnara wa pochi kama ule wa babeli.

Ukimuuliza vipi anakwambia pesa hana,na sisi ebu tujifunze kufanya wafanyavyo wenzetu tuache ubinafsi,tugawane tunachopata na wateja zetu, mama ntilie ukipika chakula nunua ndizi kata vipande vi 3 ukimpa mteja chakula mpe na ki tunda chake atakupenda sana.

Nimalizie kwa kusema kwamba "wateja wapo sana tu,ni kwamba basi watu hatutaki kujiongeza"

=====
Mimi katika hili nitoe ushauri wangu kulingana na mgahawa mmoja niliouona toka unaanza day one mpaka leo umekua sana.

Ukiwa pale mawasiliano stendi,kwenye lango la kuingilia stendi kuna mgahawa uko opposite lango hili unitwa Best Fast Food. Kuna wakati niliishi maeneo yale na nilikuwa nakula hapo.Jamaa mmiliki pale wamezoea kumuita "Mtumishi"

Wakati huyu jamaa anaanza alikuwa ame rent frame moja tu, na pembeni yake frame inayofata kulikuwa na Mgahawa pia,...that was way back in 2015. Ushindani pale ulikuwa mkali, kuna migahawa mingi, kuna mama ntilie kibao, n.k

1. Huyu jamaa aliwekeza kwanza kwenye muonekano wa mgahawa wake, aliweka viti na meza nzuri kimuonekano, aliweka vyombo vya kulia vizuri kimuonekano. Kaweka Tv kadhaa, kwa nje kaweka structure inayotoa kivuli kwa wateja wanaoamua kukaa nje.

Akatengeneza bango kubwa, zuri kimuonekano lenye logo na jina la mgahawa, Hata ukiwa umbali wa mita kadhaa bado unaweza kuona maandishi na logo. Nje akaweka sehemu ya chipsi na mishikaki, samaki wa kuchoma, kukaanga n.k

2. Huyu jamaa akawekeza kwenye quality ya service husika, yaani chakula. Aiseh pale ukiagiza wali au ugali samaki, ni samaki kweli kweli, si wa mchezo mchezo. Maana yake huyu jamaa nao watu wanaomletea sato na sangara wa kueleweka. Ana vinywaji vya kutosha including maziwa mtindi, juice za matunda za kutengeneza yeye, yaani ni full package.

In this point, kama wengine walivyosema hakikisha chakula chako kina ubora ambao mteja ataona kweli hela yake imeendana na huduma aliyopata. Huduma yenye quality watu wataifata tu popote. Nakumbuka wakati fulani mimi na jamaa yangu tulikuwa tunakaa Jet Lumo(Airport), ila kuna mgahawa tulikuwa tunaenda kula una huduma nzuri upo kama 1 km away from tunapokaa.

Make sure kwamba yaani mteja akila hapo, atamani kurudi tena kwa utamu wa chakula. Tafuta wapishi wazuri hao ndio wataleta wateja au watawafukuza. Taste ya chakula ina matter sana in this business.

3. Customer care
Hapa huyu jamaa aliajiri wahudumu ambao wengi ni wadada ambao kwanza wana lugha nzuri kwa wateja, ni wasafi, wanavaa sare always so wanakuwa easily identified na wateja. Last time nimeenda pale nikakuta wamebuni mbinu ya kuwapokea wateja na mwavuli wakati wa kipindi cha jua kali au mvua. Hii inampa mteja feeling ya kujaliwa kwamba yeye ni wa muhimu sana. Lugha nzuri huwakaribisha wateja, lugha mbaya kwa wateja huwafukuza.

4. Muda wa kusubiria huduma
Kwa huyu jamaa chakula utakipata timely, hakuna delays. Hakikisha mteja anapata huduma aliyohitaji in time. Yaani walau dakika 5 au 6 zitoshe kumpa mteja chakula alichohitaji. Si ile mteja ameenda pale anakaa 15 mins ndipo aone chakula, au anahitaji kitu fulani anaambiwa hakipo au ndiyo kinaandaliwa au kinapashwa. Always make sure vyakula vyote vinaandiwa ontime. Kuwa na vitu kama microwave.

5. Kuwashukuru wateja pindi wamalizapo kupata huduma.

Hili linaweza kuonekana dogo sana but ni la muhimu. Kumshukuru mteja baada ya kumaliza huduma aliyoihitaji na kumkaribisha tena mara nyingine ni suala linalo deal na emotions za mteja.

kama ilivyo business marketing kwa sehemu kubwa ina deal na emotions za consumers, mteja atajiona yeye anajaliwa sana, na umemuheshimu. Probability za yeye kurudi ni kubwa sana kama ukiteka emotions zake na umempa huduma nzuri.

Huyu jamaa mwenye mgahawa hapo mawasiliano, ilikuwa kila nikiwa pale namuona anawashukuru wateja wanaomaliza kula akiwa ana-smile na kuwakaribisha tena...mimi ndiyo kama alijenga na urafiki kabisa, nikishanawa atanishukuru kwa kunishika mkono, hakika nilikuwa mteja wake kwa miezi mingi.

6. Pricing ya huduma.
Kwa vile huyu jamaa aliwekeza kuanzia kwenye muonekano wa eneo lake, plus vyombo vizuri, chakula chenye ubora...bei yake ilikuwa kubwa kulinganisha na washindani wenzake wanaomzunguka...but wateja walikuwa ni wengi na wako willing to pay... why? Kwa sababu huduma ni nzuri na hata eneo jinsi linavyopendeza hata ukiambiwa hiyo bei hushituki sana. Ila huwezi kwenda mgahawa uko shagalabaghala then utajiwe bei kubwa, ten ukubali kirahisi, lazima kutazuka mjadala hapo.

7.Lastly...siku nilipotembelea tena maeneo yale in 2018 baada ya kutokwenda kwa muda mrefu nilikuta jamaa amepiga hatua kubwa. Hii ikionesha kuwa ana positive growth. Amechukua frame ya mshindani wake mwenye mgahawa uliokuwa anapakana naye. Sasa ana eneo kubwa na wateja pale stendi ni wengi sana. Ni ulimwengu wa ushindani usipokuwa innovative na good marketing strategies...you will be left behind.
 
Nataka kununua kuku wa kienyeji vijijini, niuze mjini dsm, naongezaje thamani??

Karibu, mchumi
Unaponunua kuku ili uwauze lazima uwe na malengo mawili na uwafahamu wateja wako ni wa aina gani

Kuku wako unawaleta uwauze kwa wateja wakafugwe au wakaliwe kwa nyama? Maana unapoleta kuku lazima ujue hawa kuku napeleka kwa ajili ya wateja wanaotaka nyama na hawa ni wa wateja wanaotaka kuku wa kufuga.

Tuanze na wateja wa kuku wa nyama hawa kuku wako hawana mbwembwe thamani ya hawa kuku itapatikana huko jikoni mpishi atae enda mpika na wala sio wewe muuzaji,ila kama unataka muongeza thamani zaidi customer care imetulia basi akinunua mchinje,mkatie,muwekee kwenye package nzuri,Mpe bei..soma ushauri wa CALLION

Tukija kwa hawa kuku unao wauza mteja akawafuge hawa kuku lazima uwaongeze thamani na thamani ya hawa kuku unaweza kufanya kama ifuatavyo Tengeneza kibox cha kuuzia kuku wako tengeneza vibox hata 20 vya mbao vidogo tu vya kubebea kuku Watu wengi wanauza kuku wanamkabidhi mteja kuku mkononi kama mkate au mchele.

wewe usiwe kama wao hakikisha una vibox vyako simple vya kuuzia kuku wako,mteja akija akiona ki box cha mbao hawez kukwambia nipe kuku mkononi n lazima atanunua kuku amuweke ndani ya kile kibox, Bei ya kibox unawza uza 3000 - 5000

hiyo ni moja lakini pia unaweza chagua mtetea unaejua kashaanza kutaga unamuweka kwenye kibox chake chini unaweka maranda,unamdumbukizia na yai lake kisha huyo kuku unamtenga pembeni,Mteja akija unamwambia huyu kuku kashaanza kutaga na hilo yai unaloliona kalitaga leo mchana,unampa bei ya huyo kuku (bei ya maana),mteja akiangalia kweli anaona kuku katengwa na yai analiona kwann asikupe hela unayotaka kuku akaendelee kutaga kwake?

Unaweza tengeneza box la kuku wawili mtetea na jogoo unawadumbukiza humo,hao kuku wako unawauza kwa pair yani mteja akiwataka sharti awachukue wote jogoo na mtetea wake, ukiweka bei zako hapo kwa kuku wawili plus ki box aaah pesa nzuri tu.



Bado una swali lingine? (tusitegane tafadhali)
 
CONTROLA,

Shukrani sana, kuna kitu nime gain hapo kwenye maelezo yako.

Sasa mimi nataka ku ji position kuuza kuku kwa ajili ya nyama, ila ni wale pure kabisa sio hawa chotora.

Na target market yangu ni watu wenye kipato kikubwa na kidogo pia.. mtu akiwa akiwa na 10k aweze kula kuku wa kienyeji, na mwenye 18k pia aweze kula kuku. Hii ndio target yangu.


Pia nilifikiria kutumia strategy ya online business, kufanya advertisements, kwa sababu hii project itaenda ku oparate katika level ya mediam scale, it won't be operated under very small scale,

Apart from online business, nitaweka kibanda , barabarani..kama wanavyo fanya wengine.

But my greatest mission, ni kufanya hii business katika advance level kidogo, from packaging, logo or branding name, advertising, home delivery etc..

So , you can add your advices, to strive my project's objectives to attainable in a good manner
 
Entreprenuare,
Karibu sana ndugu yangu Entreprenuare Maelezo na ufafanuzi kuhusu unachotaka nadhani tayari yapo kichwani mwako,una mawazo mapana sana,una ona mbali YES utafika mbali "keep that spirit".

Ongeza kitu kimoja kwenye hiyo biashara yako,Tambua wateja tulio nao ulimwengu wa sasa ni "wavivu" yes ni wavivu ndio maana online business zinaenda speed na zinakua, sasa hapo weka kitu ya door to door "delivery".

Mteja akitaka kuku mpe bei then mwambie unaweza mpelekea hadi mlangoni kwake Andaa bei ya delivery,Fanya biashara yako kwa wakati,mteja akitaka kuku kwa ajili ya Nyama fahamu huyu kuku anaenda kupikwa so akikwambia namuomba kuku saa 5 kamili, Wewe mlangoni kwake fika saa nne na dk 50 upo pale mlangoni kwake.

Ukiweza fanikisha wateja 30 wa delivery (uhakika) each day Amini nakwambia 2020 utakua mwaka wako wa level zingine Jipange na tambua Huduma nzuri hufatwa popote na kwa gharama yeyote,kwa maelezo yako Soon utaanza pokea order za mahoteli. Nakuonya : Usiwasahau hawa wateja wa nyumbani "usisahau ulipotoka".
 
Back
Top Bottom