Godbless Lema live Channel Ten

Godbless Lema live Channel Ten

Sheet!Tanesco?Ndo nini hivi tunafanyiana mambo ya ajabu.Kukata tu bila taarifa manake nini bana???Watu tushapata na hasara za mafuta kufuatilia kinga'amuzi!!!Hongereni channel ten kwa kulipa hilo jembe air tm kwani smtm huwa linaminyiwa chini.
 
Anasema Tanzania tuna Pamba, Korosho, Kahawa, gas , mafuta, uraniam, Tanzanite, mlima wa pili kwa urefu duniani, mbuga za wanyama kubwa kabisa duniani, hali ya hewa nzuri, nk, nk, sasa hapo tukisema Tanzania ni maskini ni kufuru.

Anasema tatizo ni hatuna viongozi wenye upendo na nchi yao ndiyo maana tuko hivi tulivyo!

Alipoulizwa kuhusu ahadi yake ya kujenga Hospitali jimboni kwake kwamba atawezaje kuitimiza wakati amekaa nje ya ubunge kwa muda mrefu, amesema ni kweli amekuwa katika usumbufu kwa takribani miaka miwili LAKINI LAZIMA NDOTO YAKE HIYO ITIMIE KUFIKIA 2015. Hataki kuwa mtu wa kutoa sababu tuu za kutokimiza ahadi.
Ahadi moja tu imemshinda,mpuuzi tu huyu
 
Vipi kuhusu kujenga Machinga Complex mbili alizoahidi kafikia wapi.
 
Hata kama elimu yake ni ndogo kama tunavyoaminishwa ila jamaa yupo smart kuliko hata hao wenye elimu kubwa hapa tz.....kasema kama kupigania haki ni fujo bs waendelee kumwita kinara wa fujo kwani hata nyerere wakt anapigania uhuru wazungu walisema anavunja sheria za nchi
Ana Advanced Diploma ni form 6 Leaver!!
 
Vipi kuhusu kujenga Machinga Complex mbili alizoahidi kafikia wapi.

ORODHA YA AHADI ZA KIKWETE KWA WANANCHI 2010 - 2015​

AHADI - ALIITOA AKIWA WAPI...

1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36.Kulinda haki za walemavu - Makete
37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43.Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido

44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma

47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini

52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha

Kati ya ahadi sitini na tisa (69), ngapi zimetekelezwa mpaka sasa
 
[QUOTE
lema ni mpiganaji hodari tena jasiri. lakini nampa ushauri kwamba katika ksema ukweli ajenge hoja kwa sentensi chache kisha kuhitimisha hoja yake kwa kuzingatia zile hoja. hapo wasikilizaji wake watashindwa kubisha au kumpinga. mfano kama unataka kusema X ni mwizi utaanza:
1. X anapata mshahara wa kima cha chini
2. X hajarithi mali popote na hana shughuli inayomwongezea kipato
3. X kwa muda mfupi ameweza kuhodhi jumba la kifahahari
4. X kwa vyovyote ni mwizi hivo ni lazima atueleze amepataje hizo fedha
hata madai ya udini yafaa yajengewe hoja kwa njia hii. akifanya hivi atajenga heshima kubwa
 
Ahadi moja tu imemshinda,mpuuzi tu huyu

Mkuu mtu mwenye hekima na kujielewa ujenga hoja kuipinga hoja!sasa hapa wewe na Lema nani ataonekana mpuuzi?maana unachojaribu kufanya ni kuidanganya nafsi yako kwa kujiambia Lema ni mpuuzi lakini ukweli unaujua kua Lema ni muelewa kuliko wewe,na anajenga hoja zenye mashiko mpaka jamii inamuelewa na kumkubali,kujidanganya mwenyewe ni hatua ya mwisho kabisa ya u.p.u.m.b.a.v.u mkuu
 
kamanda anafunguka pale.

Anasema tanzania tuna pamba, korosho, kahawa, gas , mafuta, uraniam, tanzanite, mlima wa pili kwa urefu duniani, mbuga za wanyama kubwa kabisa duniani, hali ya hewa nzuri, nk, nk, sasa hapo tukisema tanzania ni maskini ni kufuru.

Anasema tatizo ni hatuna viongozi wenye upendo na nchi yao ndiyo maana tuko hivi tulivyo!

Alipoulizwa kuhusu ahadi yake ya kujenga hospitali jimboni kwake kwamba atawezaje kuitimiza wakati amekaa nje ya ubunge kwa muda mrefu, amesema ni kweli amekuwa katika usumbufu kwa takribani miaka miwili lakini lazima ndoto yake hiyo itimie kufikia 2015. Hataki kuwa mtu wa kutoa sababu tuu za kutokimiza ahadi.

kamanda lema usiniangushe, hatuna mlima wa pili mrefu duniani. Tuna mlima mrefu kabisa ndani ya bara la afrika.
 
kamanda lema usiniangushe, hatuna mlima wa pili mrefu duniani. Tuna mlima mrefu kabisa ndani ya bara la afrika.

Kunradhi, basi labda nilimnukuu vibaya, huenda hakutamka hivyo.
 
Back
Top Bottom