Godbless Lema katika kashfa ya kuiua CHADEMA Arusha

Mods, ziweke wazi hiyo document naona naandamwa mimi au mwanaJf yeyote aziweke wazi kwani zina ushahidi wa ninachosema dalili hizo ni mbaya kwa chadema Arusha.
mmeshindwa mahakamani na sasa kilaza wenu nepi ndio kawafundisha hivi muandae upuuzi wenu mfikiri watanzania wa leo ni wale wa miaka 47,nawashauri hizi karatasi kwa kuwa serikali yenu imeshindwa hata kuwapa maji basi mzifanye toilet paper msije mkaendelea kunuka mav.... kama magamba inavyonuka sasa!!!!
 
Kwa nini pro chadema msi discuss issue yenyewe badala yake mnaporomosha matusi halafu mod mancheka tu kwenu rahaaa

Hakuna hoja ya kudiscuss hapo. Kwani yeye aliyeileta hii mada alitegemea nini, kama kweli ni mtu mwadilifu? Dawa ya moto ni maji siyo moto.
 
nimepewa na mdau kutoka chadema makao makuu ilishafika kwa Dk. wa kweli

asnte bwana lamecki kwa taarifa kesho wekeni kwenye magazeti yenu ya chama uhuru,habari leo na yale mengine nunueni kurasa za mbele ili mtimize lengo lenu. lakini kamwe kwa mbinu hii hamtafanikiwa chadema ipo kwa mpango wa mungu na hakuna wakuzuia
 
Kama imeenda makao makuu ndio mahala pake ila kuja jamvini ndo sijaelewa kdogo, sitaki kuamini kama ni mpango wa kuchafuana!
 
CDM kama taasisi nyingine inapita kwenye misukosuko mingi,kati ya hiyo mingi ni ya kupandikizwa ili chama kipoteze mwelekeo kama ilivyokuwa kwa vyama vya NCCR Mageuzi na TLP.CDM ILIANZA NA MUNGU,INAENDA NA MUNGU NA ITAMALIZA NA MUNGU.Haya yanayotokea sasa yatamalizwa na Mungu tu.
 
Na tazama sasa nilivyosakamwa kosa langu liko wapi? au kuleta barua hii hapa kwa ajili ya mjadala? it is not fair at all.

kuleta barua si kosa bali nyaraka hizo zinakutia aibu kuzileta. Hizo nyaraka pamoja na kushindwa kutoa tuhuma na kubaki kuonesha majungu, zinge pitia hata ofisi ya chama kata au tawi igongewe mhuri, pili barua imeandikwa kupitia katibu mkuu alafu inakwenda kwa katibu mkuu tena? Kanuni za wapi hiyo! Sasa ww badala ya kuangalia kwa umakini unakurupuka na kupost. Humu kuna wachambuzi wa mambo, tofauti na huko CCM mnapoambiwa zidumu fikra za mwenyekiti.
 
Hawa watoto sasa wamekuwa kero yaani sasa wanataka kugombea uraisi wakati hata ukiranja hawajawahi kupata.ona mijadala yao mtu kaleta mada na evidence wao matusi.kama cdm kufa itakufa tu.hasira zenu haziwezi kuuzuia hilo.iliyobaki leteni maji ili kife kwa aamani.
 
Na tazama sasa nilivyosakamwa kosa langu liko wapi? au kuleta barua hii hapa kwa ajili ya mjadala? it is not fair at all.

Mama Porojo yuko kila mahali sasa anadai yuko Ndago huko Singida na watu wamekufa hivyo anatuma ujumbe kwa siku...........4 hours ago alikuwa busy anajaribu ku-up load barua ya kashfa ya Lema kutokea Arusha. Hivi unataka kweli tukuamini hapa??

Pamoja kuwa barua ni ya Chadema lakini haionyeshi ni ya tawi gani au wilaya. Haina address ya waandishi. Kama kweli ni petition kwa nini walioi-sign ni mwenyekiti na katibu tu?? Kama wameamua kutumia official letter head ya Chadema mbona haina logo. Na kwa nini hakuna address za hao watu?? Inawezekana kabisa hata hayo majina haya-exist!!
 
 
 
by Demas.
Na hiiNaomba leo niweke hadharani na Msimamizi wa jf tafadhali usichanganye mada hii.

NI mara yangu ya kwanza kutuma ujumbe ingawa najua wenzangu wengi huwa wanarusha mambo mengi tu. Kuna barua ambayo nakumbuka nilishiriki kuitunga kwa lengo ya kumchafua Mh. Lema na uongozi wa chama wa wilaya na mkoa kwa lengo la kudhoofisha cHADEMA Arusha, tulifanya jambo hili tukiwa na Gerald, Mfinanga na Mamuya ambaye baadae nilikuja kugundua ni shushushu wa Lema ambaye Lema alijifanya wamegombana nae ili muda mwingi akae na maadui zake kwa ajili ya kupata habari zao.

Ukweli wa barua hii ni ya kutunga na mimi nimeuchoka kufanya mchezo huu ambao Gerald na Mfinanga wanapewa fedha na system ili kufitinisha. Baada ya kuandika barua tuliligawa kwa baadhi ya waandishi.

Nitawaanika wote kama Mamuya na Ben walivyofanya kwa wale wa BAVICHA na CHAUMMA ili mjue na muone Lema na uongozi wa chadema unavyowindwa kuvurugwa. Barua hiyo ilikuwa wote tusaini lakini waligoma kusaini baada ya mmoja wetu kumhisi D++ O++ amepewa fungu kubwa na alikuwa amelibania.

Niliwahi kumueleza kiongozi mmoja wa mkoa wa chama anajua hadithi yote hii, na yupo humu JF tafadhali uthibitishe maneno yangu.

========
Moderator
========
Hoja hii imefungwa, hadi mhusika aje kwa jina halisi na si vinginevyo
 
Ila mi naamini hzi tuhuma kwa elimu ndogo aliyokuwa nayo lema hzi tuhuma ni za kweli
 
Ole wenu enyi wanawake mnaotumiwa kuchelewesha ukombozi wa watanzania, dhambi hii itawatafuna vizazi na vizazi.kama ni kweli ulikuwa na lengo la kukisaidia chama je mahali hapa ulipoleta ni sahihi? mbona matatizo ya ndoa yako hautuletei hapa JF?
 

barua imeandikwa na slaa afu anatumiwa slaa daa kweli mfa maji haachi kutapatapa,
maccm bwana sijui ndo yamerogwa na wananchi
 
Wewe ni mtu wa kueneza habari mbaya tu za Chadema na tena za uzushi.

Leo uko Iramba kwenye mauaji, kesho umebomolewa Kawe, siku nyingine uko Ubungo. Simply huaminiki!!!!!!!!!!!!!!!!!!

mi nadhani unamuonea mleta mada bure, yeye ameweka hapa kile alichopata kwa vyanzo vyake ili watu waone na washauri ipasavyo.. nadhani ingekuwa bora sana kama ungeshambulia hoja zilizoelekezwa kwa lema kuliko kumshambulia mleta mada, utakuwa unapoteza mda wako bure coz watanzania wana akili kuliko wewe unavyowaona
 
ole wenu enyi wanawake mnaotumiwa kuchelewesha ukombozi wa watanzania, dhambi hii itawatafuna vizazi na vizazi.kama ni kweli ulikuwa na lengo la kukisaidia chama je mahali hapa ulipoleta ni sahihi? Mbona matatizo ya ndoa yako hautuletei hapa jf?
hatuwashangai ubaguzi ndio dira yenu.ona sasa mlianza na ukanda,udini sasa jinsia.
 
Marry chatanda acha ujinga wako,i know you very well.
Kumbe ule ujinga uliokua unanieleza ndo umeamua kuuleta rasmi humu
 
barua imeandikwa na slaa afu anatumiwa slaa daa kweli mfa maji haachi kutapatapa,
maccm bwana sijui ndo yamerogwa na wananchi

inaonekana una macho lakini hayaoni au yanaona giza giza...barua imeelekezwa kwa kamati kuu ipitie kwa slaa kutoka kwa wananchi wa arusha, tuliza kichwa mapepe ya nini??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…