Godbless Lema katika kashfa ya kuiua CHADEMA Arusha

Godbless Lema katika kashfa ya kuiua CHADEMA Arusha

mama porojo, hufiki popote mwishi hata wanokulipa posho watachoka, kwa taarifa yako humu Jf walikuwepo akina MS, lakini walishindwa baada ya kuona kuwa wanalipwa posho za bure.

walioandaa hiyo document ni masalia. umeingia choo cha kike
 
Mm ni mmoja wa wanachadema ambaye nilimpa kura Lema mwaka 2010, lakini kiukweli mwenendo wa Lema ni wa kutia mashaka sana, Hana maadili ya kiuongozi wala mipango thabiti ya kumkomboa mwana arusha, ndio maana hili swali halijibiwi "LEMA KAFANYA NINI ARUSHA TOKA ACHAGULIWE?" kuna siku alipaki lile benz lake old model pale Pembeni ya NMB Clock tower Arusha halafu akafungua mlango mmoja akaweka mguu kwenye Dashboard na kuanza kusoma Gazeti! dah! Mbunge???
 
Nimezisoma hizo nyarakafeki, sijaona ukashfa wala chembe ya kuiua chadema!

Mods: kumekuwa na taswira flani ya uachaji wa mijadala ya kizushi inayotupotezea mda na kushusha hadhi ya jukwaa hili!

Uzushi kama huu haina haja ya kuuacha watu waendelee kuangalia!

Barua hiyo inashindwa kuaminika kweli kama imetoka kwa makada wa CHADEMA na uongozi wa Arusha maana hakuna logo ya Chama. Lakini kama majina hayo yanayoonekana ni ya wanachama kweli wa CHADEMA jibu lako hili limekuwa jepesi mno. Ifike mahali tusilewe unazi unless kama na wewe una malengo ya kuiua CHADEMA.

Watu tumepiga kelele hapa jamvini mara nyingi. Hivi inakuaje Chama kinachangisha mamilioni ya fedha za Wananchi bila mrejesho wowote? Hizi fedha kamati kuu ya CHADEMA ina taarifa nazo? Zinaratibiwa vipi? Kuna tatizo gani slaa au akina John Mnyika kuja public na kueleza mapato na matumizi ya M4C? Kama hilo tu linashindikana itakuaje kwa kodi za wananchi baada ya hiyo 2015? Let us be serious jamani.

Hata kama kilicholetwa na MAMA POROJO ni porojo kama lilivyo jina lake lakini ukiunganisha dots na michango iliyokwishapitiswa bila mrejsho unafanya watu makini waanze kupata wasiwasi.
 
Last edited by a moderator:
Bila kamanda godbless lema tusingetwaa jimbo la arusha mjini..!

Saa nyingine chama kinasaidia lakini bila juhudi za mtu binafsi, chama hakiwezi kupata ushindi mnono..!
Mfano mzuri mbozi magharibi na kibaha mjini,chadema kilikuwa na nguvu kubwa ya kushinda lakini
kutokana na viongozi wadhaifu mtela mwampamba na habib mchange chama kikashindwa kunyakua hayo majimbo sasa wanatumikia ccm kuivuruga chadema kwa kumwaga matutsi hapa jamvini na kugombanisha viongozi wa juu wa chama..!

Nikija suala la arusha, niulize mama porojo umelipwa shs.ngapi kumchafua lema, kumbuka godbless lema ana nguvu ya umma na ana nguvu ya mungu ipo nyuma yake, hata ccm walimtaka kumchukua kwaajili ya uchaguzi ubunge 2010,

godbless lema hagombani na wenye uchungu na hii nchi,wapenda haki,wapambanaji wa ufisadi bali anagombana na wala rushwa,mafisadi,wezi,wazinifu,na wasiopenda haki na kudhulumu watu maskini..! Mfano mzuri ni ww mama porojo

godbless nusura afe kwaajili yha kugombania kiti cha umeya, baada ya polisi kutumia nguvu na kumpiga inanikumbusha hayati patric lumumba alivyouwawa na wabelgiji akipambania haki

godbless najua ameahidi mengi,lakini ubunge wake uliingiliwa na ccm, kuhusu ambulance,trekta,pesa za nmc is non of ur business, lema baba tutachangia paka mifuko itoboke, kwani matunda tunayaona.,hatuchangii bure

naona ccm mmekuja na mbinu mpya ya kuidhoofisha cdm, kwa kutumia vibaraka ndani ya chadema

ujumbe kwako kwa mama porojo,

godbless lema ni nguvu ya umma, maneno yako ya nguoni hayawezi kumteteresha ama kumpungizi ari,andika utakavyo barua, lakini lema atakujibu kwa maendeleo 2015,


mlianza na dk.slaa, sasa lema,baadaye mbowe, kisha sugu, n.n.

Porojo nyingi za nini? Kama unajua kweli kinachoendela jibu swali rahisi tu. Je, Dr. Slaa amepokea barua hii iliyoandikwa kamati kuu ya Chadema?
 
Is this how you inspire confidence? With brouhahas and hullaballoo?
 
Usichotwe kirahisi na chuki za mtu mmoja kwa mwingine akitaka nawe umchukie bila hata wewe kujua source ya chuki yake kama ni personal au lah.

Huwezi kuniambia kuwa Lema Arusha ni maarufu kuliko CDM nikakuelewa, ni majuzi tu Lema akiwa amevuliwa ubunge wana Arusha wenyewe walikuwa wakitamka kuwa Hata likiwekwa jiwe Lenye nembo ya CDM na mgombea yeyote wa CCM watalichagua Jiwe....
Je hili halitoshi kutoa uwiano wa umaarufu wa CDM na Lema Arusha??

Kamanda siwezi kuchotwa akili kirahisi hasa kwa wanajf ninao wajua vizuri.Hoja ya kujenga taasisi badala ya watu ipo pale pale na ninavyoijua Arusha( nimeishi kule nusu ya umri wangu) ni wapinzani toka zamani lakini wanapenda watu wa aina fulani na wenye misimamo haswa.

Lema anapendwa sana ARUSHA lakini tusijisahau na kuwekeza kwake badala ya Chama!!! Mkuu Ngongo najua anasimama wapi nafahamu vizuri sana!
 
Namwona Invisible yupo, ngoja niende zangu nisije pigwa ban
 
Mkuu Munyangaa utashanga hautojiwa sana sana utaambulia matusi na kupachikwa majina ya ajabu ajabu mara msalia mara msaliti hapa bado hawajachukua nchi hawataki kujibu hoja bali viroja ha ha ha ha.

[1] Tunataka kujua kwanini kiwanja cha Hospitali kimeandikwa jina lake na mke wake ?

[2] Tunataka kujua michango ya M4C anayokusanya inafanyiwa audit mara kwa mara ,Tayari kuna fedha zimeshatafunwa ingawa zipo juhudi kubwa za kuficha huu wizi kwania ya kutowakatisha tamaa wachangiaji

[3] Tunakataa uhuni wa Lema kutumia jina la wajane kwaajili ya kujipatia trecta kwa faida zake.

[4] Tunataka wasomi wajitokeze kugombea nafasi katika ngazi mbali mbali badala ya kuwapiga vita kwa hoja hafifu kwamba ni wanausalama wa taifa.

[5] Tunataka michango kwaajili ya waanga wa mauaji ya Arusha ziwafikie walengwa bila kupungua hata ndururu.

Naomba kuwasilisha.
 
Last edited by a moderator:
Mimi kama mkazi wa Arusha na mpenda mabadiliko ya kweli, tuhuma zilizotolewa juu ya Lema ni nzito sana na zimewakilishwa makao makuu ya Chadema. kwanza Lema anatakiwa ajitafakari na kuona kama zinaukweli wowote, na kama zinaukweli basi hana budi kujirekebisha kwa maslahi ya chama, ya wananchi na wapenzi wa Chadema Arusha.

Pili Chadema tusilewe sifa tukajisahau kwamba siku zote tutaendelea kukaa juu, pale mtu anapokosea sisi kama wadau tunatakiwa tumrekebishe (kama Mwenyekiti Taifa- Mhe Mbowe anakubali kurekebishwa kwanini Lema akatae!).

Mtoa mada ameleta barua iliyotumwa makao makuu kama ilivyo ila inashangaza wadau tunaanza kumshambulia kama yeye ndio mwandishi wa hiyo barua. Tulitakiwa tuchambue yaliyoandikwa kama yana ukweli wowote ndio tutoe hoja, kubisha bila misingi inaashiria hatujakomaa kifikra.

kama Great Thinkers lazima tujiulize hicho kiwanja kimeandikishwa kwa jina gani? Je Trekta lipo na nani alishasaidiwa kulima? ambulance ipo wapi na nani ameshawahi kuiona? ArDF imeshapokea kiasi gani cha fedha na watoto wangapi wameshasaidiwa?

Tulianza na Mungu,tutamaliza na Mungu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Chadema.

Mkuu,
Wewe umesema.

Tatizo kuu hapa jf kumetokea kuwa na kikundi cha watu ambao wamelishwa dictatorial propaganda ambazo zinawafanya baadhi ya viongozi kuwa kama hawagusiki katika lolote lile huku viongozi wengine wakiwa kama punchbag.

Mambo kama haya yanachangia kuleta matabaka na Unfairness kwa viongozi na wanachama matokeo yake ndiyo kuwepo kwa makundi ndani ya chama.

Tabia ya ukweli ni kugusa kila mtu na kama unafichwa basi utaendelea kujitanua mpaka hapo utakapojipambanua.
 
katika haya malalamiko baadhi yaliyoorodheshwa ni kama ifuatavyo, kwa wale ambao hawawezi kufungua hili file.

1.Lema anavunja katiba ya chama kwa kuwafukuza uanachama baadhi ya makamanda na viongozi ambao walikuwa ni nguzo kwa ustawi wa chama bila kufuata kanuni na taratibu za chama mfano kamanda MBOYA alifukuzwa kwa maagizo ya wadhifa wake akiwa mbunge, pia katibu wa wilaya KREDO ADAM alivuliwa ukatibu wa wilaya kwa maelekezo ya Lema. CHAMA KICHUNGUZE
 
Mkuu Munyangaa utashanga hautojiwa sana sana utaambulia matusi na kupachikwa majina ya ajabu ajabu mara msalia mara msaliti hapa bado hawajachukua nchi hawataki kujibu hoja bali viroja ha ha ha ha.

[1] Tunataka kujua kwanini kiwanja cha Hospitali kimeandikwa jina lake na mke wake ?

[2] Tunataka kujua michango ya M4C anayokusanya inafanyiwa audit mara kwa mara ,Tayari kuna fedha zimeshatafunwa ingawa zipo juhudi kubwa za kuficha huu wizi kwania ya kutowakatisha tamaa wachangiaji

[3] Tunakataa uhuni wa Lema kutumia jina la wajane kwaajili ya kujipatia trecta kwa faida zake.

[4] Tunataka wasomi wajitokeze kugombea nafasi katika ngazi mbali mbali badala ya kuwapiga vita kwa hoja hafifu kwamba ni wanausalama wa taifa.

[5] Tunataka michango kwaajili ya waanga wa mauaji ya Arusha ziwafikie walengwa bila kupungua hata ndururu.

Naomba kuwasilisha.



(1)kwan lema ana mke??
 
kwa wakati huu ambao barua imetolewa inaonyesha ni mkakati wa waliokataliwa kuonyesha kuwa malalamiko yapo dhidi ya wengine ila hayashughulikiwi. kwa mwendo huu CDM mnachelewa kuchukua hatua dhidi ya wanaokisaliti chama pendwa. hivi huyu lema anaetuhumiwa ndio yule yule aliyefunga barabara ya moshi arusha kwa masaa matano?
 
Lema ni Mwiba kwa Mamluki na CCM.Mlitegemea wangekaa kimya muda huu?Lengo ni kurusha tuhuma tu katika namna ya kujinusuru.uongo mtupu.Mlikua wapi siku zote?Hamtaweza kututoa kwenye ajenda yenu ya usaliti.hizi zinajibiwa au kupuuzwa na kisha tunaendelea na ajenda yenu ya vibaraka.nothing more,nothing Less....

Kamanda BEN acha mahaba mkuu, be objective....utachekwa na watu na utapoteza heshima yako...soma kwa makini hoja zilizoainishwa na wana wa arusha dhidi ya lema kabla hujarukia keybord na kupost.
 
Mods,

Msaada sisi wenye simu za mchina tuweze japo kusoma.
Mkuu Ritz,nimeamini hiki chama kina wenyewe Lema anapiga watu jukwaani halafu uongozi,wakombozi na wanajiita makamanda ndio kwanza wanapiga makofi na vigelegele mkutanoni.
 
duh, hii ndo siasa, kusifiana na kushambuliana!
 
Mtu anapitishwa kugombea Ubunge bila kufaynika kura za maoni!!! Kweli wenzetu demokrasia mnaielewa tofauti sana...
 
Kamanda BEN acha mahaba mkuu, be objective....utachekwa na watu na utapoteza heshima yako...soma kwa makini hoja zilizoainishwa na wana wa arusha dhidi ya lema kabla hujarukia keybord na kupost.
Wala usihangaike nae huyo baada ya kuomba radhi amepewa probation ndio maana anatetea kila upuuzi anatumika kama kingamuzi.
 
Back
Top Bottom