Godbless Lema: CHADEMA imepata baraka kuondokewa na Lowassa

Huu ujumbe pia unamuhusu Dr.Slaa.
Dr Slaa yule aliyesaliti misimamo yake na kwenda kuungana na aliowatuhumu kuwa wezi, wauaji wa raia wasio na hatia, mafisadi n.k huyu mzee nashangaa sana wanaompa hadhi ya kuwa mwanasiasa bora.

Alipaswa aende kwenye vyama vingine vya upinzani ili kupata jukwaa la kutetea haki za wananchi ikiwamo katiba mpya kwa ajili ya ustawi wa taifa hili kwa miaka mingi ijayo, lakini cha ajabu akaenda kuungana na adui wa wananchi wa nchi hii aliokuwa akiwapigania kwa jasho na damu

Huwezi kuwa na misimamo ya kile unachokiamini halafu ukaenda kuungana na adui yako ili kuteketeza wale uliokuwa unawapigania, Slaa kwangu simtofautishi na hawa wapiga zumari la mfalme akina Msukuma, Lusinde, polepole, Mwakyembe n.k maana hawako kwa ajili ya wananchi ila wako kwa ajili ya kudhulumu wananchi haki zao

Kilichompeleka huko aliko leo yule mzee Slaa ni kwa sababu ya kupigania tumbo lake maana kaona miaka inasonga sana lakini mama mshumbusi bado anauhitaji ujana kwa nguvu kubwa, hivyo ili amridhishe na ndoa iendelee kuwa na furaha ni lazima apate kazi nzuri ya kumuingizia kipato kizuri zaidi, kwahiyo aliamua kuwa mnafiki wa misimamo yake ili apate alichokipata

Masikini hana kiapo, na unafiki unalipa hiki ndicho kilichotokea kwa Dr Slaa, huyu mzee alishindwa kufia misimamo yake kwa tamaa ya madaraka, japo kuondoka kwake Chadema ilikuwa katika utata mtupu ila hakuwa na uhalali wa kuungana na hawa maadui wa nchi hii, na hapa ndipo nilipomuona hana maana kabisa

Leo hii kuna matukio ya kuuawa watu, kutekwa watu, kushambuliwa watu, kuuawa raia kwenye vituo vya polisi lakini Dr Slaa yuko kimya kwa maana kwamba anayatetea maovu yote haya

Aliulizwa kuhusu tukio la kushambuliwa Lissu akasema ni tukio la kawaida sana wala halina upekee wowote, huyu mzee nilimuona mjinga sana kwa sababu angekuwa Chadema asingetoa kauli ile ya kufedhehesha sana, kwahiyo mzee Slaa leo hii anahalalisha maovu yote yanayotendeka nchi hii.
 
Napenda kumuita Lema ni mnafiki wa kiwango kikubwa sana, tena bora akakaa kimya. Yeye na viongozi wenzake wa cdm ndio walimpokea Lowassa baada ya kupokea hela yake na kumsafisha, leo ndio anatoka na lugha za kipuuzi eti shamba sijui ujinga gani.kwani walipompokea huku sisi tukisema ni makosa hayo anayosema leo alikuwa hayajui?

Hakuna kura wala idadi ya wabunge tuliopatiwa na Lowassa kwani alikuwa na miezi miwili tu ndani ya cdm, hata bila yeye cdm ingepata kura na viti vingi na chama kingebaki na heshima yake. Kama yeye ndio alileta hizo kura akiwa na miezi miwili, aliongeza wangapi akiwa na miaka mitatu ndani ya cdm? Acha upotoshaji.
Hujui usemalo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwacheni Huyo aende zake ,mradi kaondoka mapema na kuacha muda nzuri tu wa chama kujipanga ,yaliyopita si ndwele tugange yajayo ,njia nyeupe kwa Lissu 2020 .
 
Dr Slaa yule aliyesaliti misimamo yake na kwenda kuungana na aliowatuhumu kuwa wezi, wauaji wa raia wasio na hatia, mafisadi n.k huyu mzee nashangaa sana wanaompa hadhi ya kuwa mwanasiasa bora.

Alipaswa aende kwenye vyama vingine vya upinzani ili kupata jukwaa la kutetea haki za wananchi ikiwamo katiba mpya kwa ajili ya ustawi wa taifa hili kwa miaka mingi ijayo, lakini cha ajabu akaenda kuungana na adui wa wananchi wa nchi hii aliokuwa akiwapigania kwa jasho na damu

Huwezi kuwa na misimamo ya kile unachokiamini halafu ukaenda kuungana na adui yako ili kuteketeza wale uliokuwa unawapigania, Slaa kwangu simtofautishi na hawa wapiga zumari la mfalme akina Msukuma, Lusinde, polepole, Mwakyembe n.k maana hawako kwa ajili ya wananchi ila wako kwa ajili ya kudhulumu wananchi haki zao

Kilichompeleka huko aliko leo yule mzee Slaa ni kwa sababu ya kupigania tumbo lake maana kaona miaka inasonga sana lakini mama mshumbusi bado anauhitaji ujana kwa nguvu kubwa, hivyo ili amridhishe na ndoa iendelee kuwa na furaha ni lazima apate kazi nzuri ya kumuingizia kipato kizuri zaidi, kwahiyo aliamua kuwa mnafiki wa misimamo yake ili apate alichokipata

Masikini hana kiapo, na unafiki unalipa hiki ndicho kilichotokea kwa Dr Slaa, huyu mzee alishindwa kufia misimamo yake kwa tamaa ya madaraka, japo kuondoka kwake Chadema ilikuwa katika utata mtupu ila hakuwa na uhalali wa kuungana na hawa maadui wa nchi hii, na hapa ndipo nilipomuona hana maana kabisa

Leo hii kuna matukio ya kuuawa watu, kutekwa watu, kushambuliwa watu, kuuawa raia kwenye vituo vya polisi lakini Dr Slaa yuko kimya kwa maana kwamba anayatetea maovu yote haya

Aliulizwa kuhusu tukio la kushambuliwa Lissu akasema ni tukio la kawaida sana wala halina upekee wowote, huyu mzee nilimuona mjinga sana kwa sababu angekuwa Chadema asingetoa kauli ile ya kufedhehesha sana, kwahiyo mzee Slaa leo hii anahalalisha maovu yote yanayotendeka nchi hii.
Huna lolote mwana mkosaji!Hoja ni lema ajabu unamahambulia Slaa!Ulikuwa hujazaliwa nini kipindi Slaa anawatahadharisha wazungusha mikono wenzako kumhusu El ewe mkosaji?!
 
Siasa hapo ndio huwa zina furahisha kama mnajua mtu ata wageuka au mbinafsi ana jipigania yeye kwanini hawakuja adharani na kutuambia akiondoka ndio kila mtu ana kuja na yake
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kurejea CCM.

Lema amedai kuwa uamuzi wa Lowassa unadhihirisha kuwa ameweka mbele maslahi yake binafsi kuliko mabadiliko aliyokuwa anayahubiri alipoingia Chadema.

Alidai kuwa Lowassa alifikia uamuzi huo ili kulinusuru shamba lake linaloshikiliwa Mkoani Tanga, shamba lake la mifugo linaloshikiliwa Dodoma pamoja na kumnusuru mkwewe Sioi Sumari na kifungo dhidi ya kesi inayomkabili.

Sumari anatuhumiwa kwa kula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kughushi pamoja na utakatishaji wa fedha.

“Mtu huyu alitaka kuwa Rais, hali ya kisiasa ilivyo sasa watu wapo magerezani, wanapata misukosuko ya kibiashara, hawana cha kuipa CCM ili wapate ahueni, lakini kwa sababu yeye anacho cha kuwapa CCM ilia pate amani. Hajaona gharama ya kufanya hivyo,” Lema amekaririwa na Gazeti la Mwananchi

“Chadema imepata baraka kuondokewa na mtu kama huyu. Alikuja kwa ajili ya kutaka urais na sio mabadiliko aliyokuwa akiyanadi. Nchi inataka demokrasia, katiba mpya, sheria mpya na inakabiliwa na ubanaji wa vyombo vya habari… mwanasiasa makini hawezi kuungana na CCM,” aliongeza.

Lowassa alijiunga na Chadema mwaka 2015 baada ya jina lake kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha watu waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Aligombea urais na kuleta ushindani mkubwa dhidi ya Dkt. John Magufuli wa CCM.

Juzi alipokewa na Dkt. Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lowassa alieleza kwa ufupi kuwa amerejea nyumbani. Alipokewa katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Lema kaongea ushuzi.anajitekenya na kucheka mwenyewe
 
Huyu jamaa hana chembe ya aibu, duh.

1551624309900.png
 
Back
Top Bottom