Godbless Lema: CHADEMA imepata baraka kuondokewa na Lowassa

Naendelea kusisitiza kwamba Lowassa ni fisadi. Alipojiunga CHADEMA alipigwa sala ya toba, Mungu akamsamehe. Sasa ameamua kurudi kwa mafisadi wenzie aliowaacha, uvumilivu umemshinda. Sasa ajiandae gadhabu ya Mungu inaenda kumshukia. Mungu huwa hadhihakiwi.

Unafanya toba na kusema umebadilika hadi unazungusha mikono. Mungu nakuruhusu umshughurikie Lowasaa na kizazi chake. Kafanya ufisadi hadi nywele zimekuwa nyeupe.
Hivi aliomba sala ya toba?: waliofikiri kuwa yeye ni asset walifanya yao_- Slaa anastahili kuwa diplomat
 
Brother lema sio bure leo fena umepuliza majani yako
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amefunguka kuhusu uamuzi wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa kurejea CCM.

Lema amedai kuwa uamuzi wa Lowassa unadhihirisha kuwa ameweka mbele maslahi yake binafsi kuliko mabadiliko aliyokuwa anayahubiri alipoingia Chadema.

Alidai kuwa Lowassa alifikia uamuzi huo ili kulinusuru shamba lake linaloshikiliwa Mkoani Tanga, shamba lake la mifugo linaloshikiliwa Dodoma pamoja na kumnusuru mkwewe Sioi Sumari na kifungo dhidi ya kesi inayomkabili.

Sumari anatuhumiwa kwa kula njama ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu, kughushi pamoja na utakatishaji wa fedha.

“Mtu huyu alitaka kuwa Rais, hali ya kisiasa ilivyo sasa watu wapo magerezani, wanapata misukosuko ya kibiashara, hawana cha kuipa CCM ili wapate ahueni, lakini kwa sababu yeye anacho cha kuwapa CCM ilia pate amani. Hajaona gharama ya kufanya hivyo,” Lema amekaririwa na Gazeti la Mwananchi

“Chadema imepata baraka kuondokewa na mtu kama huyu. Alikuja kwa ajili ya kutaka urais na sio mabadiliko aliyokuwa akiyanadi. Nchi inataka demokrasia, katiba mpya, sheria mpya na inakabiliwa na ubanaji wa vyombo vya habari… mwanasiasa makini hawezi kuungana na CCM,” aliongeza.

Lowassa alijiunga na Chadema mwaka 2015 baada ya jina lake kuondolewa kwenye kinyang’anyiro cha watu waliokuwa wakiwania nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM. Aligombea urais na kuleta ushindani mkubwa dhidi ya Dkt. John Magufuli wa CCM.

Juzi alipokewa na Dkt. Magufuli, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Lowassa alieleza kwa ufupi kuwa amerejea nyumbani. Alipokewa katika Ofisi ndogo za Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom