Godbless Lema avuliwa ubunge

Status
Not open for further replies.
Godbless Lema wewe bado ni Mh. Mbunge wetu tutapiga kura tena kudhihirishia ulimwengu wote na mafisadi wote kuwa wewe ni chaguo la wananchi wa Arusha.

Tupo Pamoja Brother.
Peopleeeeeeeeeeeeeeeeeeees Power
 
Mazungumzo kupitia simu itv, G. Lema ameshtushwa na uamuzi wenye shindikizo ndani yake. Kizuri hawajamnyang'anya haki yake ya kushiriki uchaguzi tena.
 

Mahakama ishasema anaruhusiwa kugombea,sasa hyo pingamizi itaenda kwa nani msuluhishi? Hayo maneno hatuyachukui,CDM itamsimamisha LEMA na atashinda kwa 99% we subiri tu!
 
Nimeumia Lema kunyang'anywa nafasi aliopata kihalali.

Nimeumia zaidi kwa mfumo wa mahakama, kwa mfumo huu wa mtu mmoja kuamuru nani ana hatia na nani hana hatia INATISHA sana.

Kama ni personal attack, arumeru imeonesha akina nani ni qualified kwa mchezo huo.


Yaelekea kimekuuma sana,,,,,pole sana, tunataka Tanzania inayoendeshwa kwa misingi mizuri. Kwa personal attack aliyoifanya Lema dhidi ya mpinzani wake hakustahili kabisa kuliwakilisha jimbo lenye hadhi kama Arusha mjini bungeni
 
Hivi hakuna vifungu vya sheria vitakavyomzuia Lema kugombea tena? hebu wajuzi wa sheria tujuzeni hapa

Kama kuna suala la kutoa rushwa na limethibitishwa na mahakama basi hataruhusiwa kugombea. Rejea kesi ya Waryoba na Wassira baada ya uchaguzi wa 1995.
 
Mimi naona niachane na mambo siasa. Siasa itasababisha mauti yangu, siku marehemu Regia alipochakachuliwa live mchana kweupe, roho iliniuma cna kipomo!..then akaja akafa, sikuambii! Haya tena leo, cku yangu ishaaribika,na wiki yote hii cwezi kurudi ktk hali yangu ya kawaida! Mi naona niachane na siasa. Kwanini nipate shida, taabu, kwa mambo siyo yangu? Kuanzia sasa,jukwaa la siasa basi!
 
Lazima tuangalie wapi tulifanya makosa tuweze kujikosoa na tuweze kulirudisha jimbo letu la Arusha. Wao wananguvu za kimahakama na dola kiujumla sie hatuna ila for the name of 'PEOPLE'S POWER' pamoja tutashinda.
 
Lema anaruhusiwa kugombea tena, kosa la rushwa ndo lina mzuia mtu kugombea tena refer kesi ya ubunge kati ya Warioba na Wassira.
 
Baada ya mahakama kumuengua kamanda lema baadhi ya viongozi wa ccm wameapa kulipiza kisasi cha kunyang'anywa arumeru kwa kunyakua Ausha Mjini. Nasubiri picha
 
CCM inatumia mahakama kuhujumu upinzani na hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi!!

halafu bado waafrika wanasema ICC iko kwa ajili ya kuwaonea waafrika acheni ICC iwepo hakuna haki kabisa kwenye hizi mahakama zetu
 
Magamba kazi imewashinda badala ya kutuangaikia wananchi kutuletea maendeleo wao na wapinzani
ila kazi wanayo wasitegemee kuwaondoa kirahisi
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…