Kama tatizo ni mitandao ya kijamii, najiuliza kwanini mitandao ya kijamii ionekane kuharibu vijana wa Arusha zaidi kulinganisha na maeneo mengine?
Je, kweli hili tatizo ni kubwa kama linavyozungumzwa kwenye hizi forum?
Kwamba leo mtu yeyote akienda Arusha, basi lazima atakutana na hali isiyo ya kawaida machoni pake, ambayo hajawahi kuiona maeneo mengine hapa Tanzania?
Siwatetei hao vijana wa Arusha Mjini, lakini nijuavyo kila sehemu ina watu wake waliovurugwa.
Kama tatizo ni kuogopa mavazi, nadhani hao watoto wa kike wanaweza kuolewa na wale wanaopenda mavazi hayo, kwani wapo pia wanaovaa madera siku zote na bado hawajaolewa.
Hii dunia haijawahi kueleweka, ukijisumbua kuielewa utachanganyikiwa, mtengeneze kwa kwako nyumbani.