PreGE2025 POTOSHI Godbless Lema, anaiunga mkono CCM uchaguzi mkuu

PreGE2025 POTOSHI Godbless Lema, anaiunga mkono CCM uchaguzi mkuu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2

1756184622087.png
 
Tunachokijua
Godbless Lema awali aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Msajili wa vyama vya siasa, na kisha baadaye kuteuliwa tena kwa ajili ya kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mnamo tarehe 14 Januari, 2025 Lema alifanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ambapo pamoja na mambo mengine alitumia fursa hiyo kutangaza msimamo wake dhidi ya kumuunga mkono Tundu Lissu alipokuwa akigombea uenyekiti CHADEMA Januari, 2025.


Video inayomuhusisha Lema kuiunga mkono CCM

Ipo video inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha Lema akisema 'hata nchi ikibadilisha utawala wa kisiasa, kikaingia chama kingine cha upinzani, hicho chama hakiwezi kubadilisha nchi hata kama hicho chama kitakuwa ni chama cha siasa. jambo la msingi ni chama cha mapinduzi kuendelea kutawala nchi"

Uhalisia wa video hiyo

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia marejeo ya video umejiridhisha kuwa video hiyo imepotoshwa uhalisia wake kutoka kwenye hotuba ya Lema aliyoitoa Januari 14, 2025 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Video imepotoshwa kwa kukata vipande kutoka kwenye hotuba hiyo na kuviunganisha isivyo stahili hatimaye kubadili ujumbe uliokusudiwa na Lema.

Aidha katika video halisi Lema alisisitiza kuwa chama chochote cha siasa kinapaswa kuwa na maono ya vizazi vijavyo huku akitahadharisha chama kisichokuwa na msingi wa kukataa ubaya na hakifikirii kuhusu vizazi vijavyo basi hakiwezi kubadilisha nchi.

"Vyama vya siasa vinatengeneza culture (Utamaduni) za nchi kwa sababu siasa ndiyo inafanya kelele za kila siku za nchi na kelele za kila siku za zinatengeneza culture ya nchi.

Sasa CHADEMA wakikosea kutengeneza culture bora, CCM wameshakosea kutengeneza culture bora, ni kimsingi hata nchi ikibadilisha utawala wa kisiasa kikaingia chama kingine cha upinzani, hawa watu kama akili zao hazina msingi wa kukataa ubaya, hawana upendo, hawafikirii kuhusu generation 50 (vizazi) ya miaka 500 inayokuja hicho chama hakiwezi kubadilisha nchi hata kama hicho chama kitakuwa ni chama cha siasa.

Msingi wa kwanza wa upinzani ni 'mindset transformation' ni bora kuchelewa kuchukua mamlaka lakini ukajenga watu wenye culture ya ubora wa hali ya juu sana"​
Back
Top Bottom