Girlfriend wangu kanitongozea rafiki yake.

Girlfriend wangu kanitongozea rafiki yake.

Mbinu za kitoto za wadada eti anakupima km anampenda au vipi. Mimi nilifanyiwa hivyo na mamsap wakati huooo! Shida aliyenigonganisha nae dah sio type zangu kabisa. Eti anapanga kidate wanakuja wote halafu anajifanya kaitwa na dada yake anatuacha na Mimi na rafikiye. Mie zangu Watoto wa kitusi dizaink zile yeye anaenda kunigongesha kwa mbantu mwenzangu wote sura paaana pua zetu zinafanana hahaha. Nikamtext niko home na rafiki yako weeee alimpigia simu akataka kujua tuko wapi. Hee bidada akashangaa. Sasa wengine huwa wanaunga wanatafuna tuu
Hahahah we jamaa bana eti pua pana, alikua kisu lakin? au umekariri pua ndefu za kitutsi ndo wanakua wazuri pekee?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu sijaelewa hapo juu umesema ilikua night kali halafu ulikua na gari ukawarudisha makwao akiwemo huyo Anna, sasa inakuaje unamuuliza gilfriend wako kwamba Anna alifika salama? Wakati ni wewe uliempeleka? Utanisamehe hua nasoma vitu kwa makini kidogo...embu fafanua vizuri hio script naona kuna sehemu kama vile unafeli...
 
Inaonyesha uu fisi sana na kalitambua hilo gf wako, kibuti kinakuita.

Ila huyo Anna naye mbandue tuu haviachi alama

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuhh ... inshort jamaa mtoa mada na demu wake wote ni mafisi ...wajua mafisi huwaga wana mioyo migumu kama mahindi makavu ... yaani wakiumia nikidogo tu then wanapoteza ... haiwezekani demu asiwe fisi halafu awe na guts za kiasi hicho

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuu imekaaje hii? Nina girl wangu namwelewa sana mzuri nampenda. Sasa majuzi hivi ilikuwa ni Siku yake ya kuzaliwa. Basi ili kumfurahisha nikajichanga na kumfanyia ki party cha kiaina.

Iyo Siku ya party walikuwepo rafiki zake kadhaa na mmoja wapo ambapo nilimuliza akaniambia anaitwa Anna ( isn't real name). Basi party ilikwenda fresh na baadae kila mmoja aliondoka, wengine niliwapeleka mimi na gari kwa sababu ilikuwa night sana na mmoja wapo ni uyo Anna.

Baada kama Siku kadhaa nikiwa nae geto nilimuliza kama wale rafiki zake walifika salama, akajibu ndio. Nikamuliza na Anna je? Akajibu ndio lakini baada ya mda aliniuliza kama nimempenda Anna maana namulizia sana.

Me nikamjibu hapana sio kwa hivyo ulivyowaza. Kumbe yeye akawa serious zaidi na kwenda kumwambia Anna kuhusu mimi. Basi juzi ivi kabla ya sikukuu nikiwa mbishe, Anna kanitafuta kwa simu na kuniambia flani kasema unashida ya kuonana na mimi. Katika kuongea nikajikuta nimemuliza kama yuko tayari tuonane.

Akatiki basi jumapili tuka onana ..kiukweli uyu Anna ni mkali balaa kuanzia shepu mpaka sura yani ameiva kila idara. Tukapiga stories za hapa na pale kufahamiana nini.. badae sasa ndo nikamuliza kuhusu Jenipha( my girl, siyo real name) alimuambia nini.

Mtoto akaanza kutiririka Jenipha kamwambia mim nimwelewa sana na tangu ile Siku ya party nimemwona basi nimekuwa nikimuwaza. Mimi nikamuliza kama yuko single basi akajibu kuwa yuko single kwa zaid ya mwaka sasa.

Nikamuliza pia yuko tayari kuanza relationship akanijibu kama akipata mtu sahihi kwake yeye yupo ok na yupo tayari. Nikashindwa nimkatae vip maana hajui kama rafiki yake ni mpenzi wangu.

Kristmass alinialika na anakaa peke yake, nikashindwa kwa sababu nilikuwa na my girl Jeni. Japo dah! Niliumia kimtindo kukosa huo mwaliko. Sasa tangu juzi tuna chart nakurushiana picha wasap na nini ( sio picha za utupu) kama tuna anza kuwa close vile.

Sasa wakuu nauliza huyu girl wang alikuwa na lengo gani kwenda kumpanga mwenzake wakati yeye anajijua kuwa yupo? Ni mtego gani ananitegea apo? Na uyu Anna nashindwa nimkatae vip maana ni mzuri sana anatamanisha.

Wakuu nishaurini nipige kwa Uyu Anna halafu nimkatae au nimwambie tu ukweli kuwa aliyekutuma kwangu ni mpenzi wangu.?

Kama ni ndefu sana mtanisamehe wakuu, ni ukweli na siyo maneno ya kutungwa.

Nishauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Paragraph ya tatu Mwisho inakuhudu...


Ova..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamkosea Sana Gf wako ,amefanya hivyo out of hasira as why ulimspot Anna pekeAke Kati ya rafiki zake wengine afu bado unamuongelea ongelea!!!
Inshort girl wako kafanya out hasira na sio kwamba hakupendi sababu inachukiza Sana kuona boyfriend wako amekeep an eye Kwa rafiki yako inakera
Na Huyo Anna ni mwehu anajua Kabsa mahusiano yenu ila bado tu na yeye anajipendeza, for a humble girl hata Kama ingekua Jeni anamuunganisha Kwa kakayake, Anna lazima angesubir huyo Kaka amuanze na sio kuanza kupiga lisimu na mwaliko juu khaaaa

Pole sana ukiachika Kisa Anna, she's not typa girl to keep for a serious relationship .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tarehe 7 january ifike haraka,ili shule zifunguliwe na hawa wanafunzi warudi mashuleni Jf ipumue kwa muda.Maana hizi ni kero sana,upo nyumbani kwa baba na mama,umekula ugali wa wazazi na kushiba halafu unapata nguvu za kuandika hizi hadithi!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom