Ghorofa gani leo ntaruhusiwa kupanda juu

Ghorofa gani leo ntaruhusiwa kupanda juu

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,253
Reaction score
15,748
Wakuu nipo natafakari hapa leo nataka usiku wa saa sita nishuhudie zile fataki kila pembe ya jiji.

Naombeni location nzuri kama kwenye ghorofa hivi lolote refu niweze kuona jiji zima kwa uzuri.

Nafaham magorofa mnegi ila sijawahi kuyapanda mpaka kule juu.. sasa kama kuna atayefanya kama mimi embu naomba mwongozo. Itakuwa rahisi kwangu maeneo ya Sinza, Ubungo, na Makumbusho.

Asanteni
 
Nenda kanunue fataki na ww urushe ili ulione.
Ningetaka kwenda kununua fataki ningeandika hapa. Ila mimi nataka kwenda kuangalia kama nilivosema kwenye uzi wangu. Usinilazimishe kufanya kitu ambacho sitaki, nimeomba tu ushauri kwa watu kama hujui ungekaa tu kimya mkuu. Ama nimefanya kosa kuuliza?
 
nenda magogoni (jumba jeupe) utaonywesha mahala pakupanda
Nimesema nahitaji location ama Sinza, Ubungo, na Makumbusho. Hayo ya kwenda magogoni mi sijasema. Saa nyingine ni bora kukaa kimya kuliko kumshauri kitu asichokitaka. Si lazima kila uzi mtu u comment
 
Hall 5 UDSM, kule ni kilimani pia kwa hiyo jiji lote unaliona kwa uzuri.

Hata Hall 2, sema lile lina expansion joints nyingi.
Asante mkuu wakati nasoma kila mwaka mpya ilikuwa lazima nipande mule.. ila sasa naona sitakuwa comfortable.. nlitaka sehemu ya uraiani zaidi
 
Hall 5 na 2 yalishafungwa hayatumiki kwa sasa mpk yafanyiwe ukarabati
Hata hivo yameshafika ukomo wa matumizi nadhani. Na bora wameyafunga kulikuwa na harufu ya kifo pale hasa hasa Hall 2. Ukarabati wenyewe hauwezekani labda wapunguze zile ghorofa zibaki 6 ama wabomoe kabisa
 
Aisee tuko tofauti...
Ulidhani watu tupo sawa mkuu?

From today elewa hivi --> "Binadamu wote ni sawa ila watu wote sio sawa''

Na ukijiona upo sawa na wenzako jitafakari sana maisha yako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom