Gharama za uzalishaji katika biashara yoyote

LOVINTAH GYM

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
459
643
TOTAL COST

Variable cost + Fixed cost= Total cost

Total cost
ni gharama za uzalishaji wa kitu chochote

Total cost imeundwa na gharama ambazo hazibadiliki hata ukizalisha kidogo na gharama ambazo zinabadilika kulingana na idadi ya uzalishaji.


Fixed cost

Hizi ni gharama ambazo hazibadiliki katika uzalishaji wa kitu chochote.

Huwezi kuzikwepa.

Uzalishe kitu kimoja au 10 gharama ni ile ile, uuze au usiuze gharama ni ile ile.


Mfano:

1. Machinga auze au asiuze ni lazima alipe kodi ya manispaa, awe na mzigo wa million 1 au laki 2 bei ni ile ile.

2. Wakala ni lazima alipe kodi yake ya mwezi haijalishi amepata wateja au hajapata wateja, haijalishi mtaji wake ni laki 8 au million 50.

3. Muuza bidhaa wa insta, haijalishi ameongeza mzigo au hajaongeza, ameuza au hajauza lakini gharama za matangazo ni zile zile.


Variable cost

Hizi ni gharama ambazo hubadilika kutokana na uzalishaji.

Mfano:

1. Muuza mihogo, ata gharamika kununua mafuta ya ziada ili akaange mihogo mingi zaidi.

2. Sales person, atalipwa comission kulingana na mauzo atakayofanya.

Fixed cost ndio hufanya watu wengi kushindwa kuanzisha biashara kubwa, maana hizi ni gharama ambazo kama mtaji wako ni mdogo au uzalishaji wako ni mdogo basi lazima utafeli.

Mfano:

Unataka kufungua biashara ya pharmacy

Fixed cost zake kwa mwezi:


Kodi, umeme, kulipia cheti cha mphamacia, kumlipa pharmacist wa kuuza dawa


Variable cost zake kwa mwezi:

Commission kwa muuzaji, cost ya delivery kwa mteja, mifuko ya kuwekea dawa nk

Profit = Sales - Total cost

Karibuni kuchambua fixed na variable cost za biashara nyengine

#sales #pharmacy #pharmacist #cost #totalcost #fixedcost #variablecost #profit #smallbusiness #startup

Fixed and Variable Costs.png
index.png
 
Je issue ya electricity inakua variable cost kwenye business nyingine?
Inategemea, mfano kila mteja anapokuja ndio utaanza kumenya viazi umkaangie chips zake peke yake, na wateja wanakuja kwa mida tofauti huenda ikawa variable cost. Japo kwa biashara nyingi especially ambazo umeme ni wa kuchangia labla kwa mwezi lazima utoe 20,000 haijalishi matumizi basi io ni fixed cost.
 
Back
Top Bottom