Gharama za uendeshaji DSTV kulikoni

Big One

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
759
47
habar wa jf hv ndugu zangu dstv wanamatatizo gani gharama zinazidi kupanda sana au wao ndo wanazijua pesa sana kuliko sisi mm nadhani kampuni nyingine ijitokeze watashusha bei wenyewe wana jf hakuna mtu aneshughulikia gharama za uendeshaji ktk gvt yetu hii karibuni kwa michango yenu
 
Hana rival wa maana kwenye soko,baada ya kupigwa changa la macho na GTV.Wangetia akili tu hao DSTV.
 
Wanapandisha bei bila hata kujali kuwa hatuangalii masaa yote na huu mgao wa umeme wa masaa 16, hawana hata aibu wanachaji kwa siku badala ya kutumia mfumo wa LUKU... Hivi kama Tanesco wangechaji kama DSTV ingekuwaje. Sio lazima kusubiri kampuni nyingine ije ila na wao waone aibu kutuibia wateja wao hata wakati huu muda karibu wote hakuna umeme. Na hata umeme ukiwepo wanaangalia mahouse girl tu kwani tuko kazini mchana tukirudi jioni tumechoka. Wazungu wanatumia pay per view, hawa wezi wanachaji pay without view, ni kama capacity charge tunazolalamikia Tanesco. JAMANI DSTV ONENI AIBU MTUMIE MFUMO WA LUKU AU PAY PER VIEW SIO KUTUIBIA HELA ZETU AUTOMATIC. ZIKIBAKI SIKU MBILI MNATUMA MSG TULIPIE BILA KUZINGATIA KUWA WATEJA HATUJAANGALIA CHANNEL ZENU HATUNA UMEME
 
Wale wameweka malipo yao kwa dola, kwa hivyo dola ikianguka na wao wanakula shushu. Tena rate yao ni komesha wanafanya forecast ya kuanguka rate ya mwaka ujao ndiyo wanakucharge leo.
 
mambo iko huku STARTIMES living for today building tomorrow, just 9000 per month nadhani Mpira tu ndo tunaukosaaaaa
 
Kwani umelazimishwa kuendelea na dstv? Wewe mwenyewe unasema muda mwingi haupo nyumbani na kama upo home mgao wa umeme ni balaa! Achana nao! Lipia star times kama unataka mechi nenda baa ukaangalie!
Watanzania tunapenda kushadadia mambo hata kama uwezo wetu hauruhusu. Na hata kama uwezo unaruhusu si lazima ukawa na dstv usiyokuwa na manufaa nayo. Ni bora hiyo pesa unayolipa bila kuitumia ukai save na kuinvest katika mambo mengine!
Watanzania bwana! Tunalalamika weeee, no action! Tubadilike jamani
 
Naipenda Tanzania.
Inajali wageni kushnda wazawa.
Nataman ningekuwa mgeni.
 
mimi hakuna kitu kinaniboa kana kile kibahasha chao! kinaanza kupeperuka siku 3 kabla ya hawakata sinema zao... my last born hua ananivizia asubuhi utasikia baba baba... dstv wamekituma kile kile kibahasha chao cartoon itakuwaje??kudadeki utazani wanamlipa kwa kunikumbusha kulipa bill zao...
 
Niliwahi kudokezwa kuwa unaweza ukaipata coverage ya Abudhabi TV (Abu Dhabi TV wins English Premiership football rights « Campaign Magazine Middle East ) hapa nchini, wao malipo yao wao ni kama USD 100 tu kwa mwaka, kuna yeyote mwenye taarifa zao?

Mkuu mimi nakaa Kisukuru B. Nina bahati naipata TVZ na kwa hiyo naona Premier League bure. Ni TV chache sana ambazo zinaweza kunasa TVZ, sijui kwa nini. Tunatumia antennae ya kawaida. Kisukuru yote hamna anayenasa TVZ. Quality ndiyo siyo nzuri sana.

Nasikia charge ya hao Abu Dhabi ni sawa na bure ukilinganisha na dstv
 
mimi hakuna kitu kinaniboa kana kile kibahasha chao! kinaanza kupeperuka siku 3 kabla ya hawakata sinema zao... my last born hua ananivizia asubuhi utasikia baba baba... dstv wamekituma kile kile kibahasha chao cartoon itakuwaje??kudadeki utazani wanamlipa kwa kunikumbusha kulipa bill zao...

hahahahaha umenikumbusha mbali sana..... chunguza vizuri unaweza ukakuta kijana kaaanza ujasiriamali mapema kwa kuwa indoor agency wa dstv... anakula percent na c unajua siku hizizmabepari wanapenda cheap labour.. wanaweza kuwa washachonga nae dili
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom