Gharama za sherehe ya harusi

Gharama za sherehe ya harusi

gharama zisizoepukika kutoka mfukoni mwako na ili bibi arusi akuheshimu niiiiiiiiii;
Gharama za mahari
Mavazi ya bibi harusi
Mavazi yako mwenyewe
Gharama za honey moon
Pesa ya kuanzia maisha baada ya ndoa

naomba niongeze nyama mkuu,mavazi ni pamoja na pete 3.gharama ya saloon si chini ya laki,nguo za wazazi wake.
 
mkuu mimi hapa mama yangu akiongelea hayo mambo tunapishana kwa sababu tu mimi naamini ndoa na sitaki harusi.... kwa hiyo nimeshaamua na hapa nilipo najaribu kumshawishi huyu mpenzi wangu kuwa aachane na maswala ya harusi tufunge ndoa.. na namshukuru Mungu tupo karibu kuelewana japo anahisi kama kuna jambo namficha... ninakajukumu cha kuendelea kumshawishi mpaka tuelewane tu... mwenzangu akinielwa anakazi na yeye yakuelezea wazazi wake pia waelewe... now days bwana wazazi ndiyo wamekuwa watu wa kwanza kushurutisha harusi mara send off sababu kubwa atakuambia kuwa amechangia harusi nyingi na yeye anatakiwa achangiwe ambapo to me ni hoja jepesi tu hiii ... any way msimamo wangu siubadilishi sababu sitendi dhambi ila nafanya lile la msingi

Hongera sana misschaga ni wanawake wachache sana wenye upeo kama wako.

Keep it up!
 
Last edited by a moderator:
wengi tunaandaa mambo ya nje nivae shela harusi kubwa ... tunaandaa kufurahisha jamii huku tukisahahu kujifanyia evaluation in detail je kweli moyo wangu upo tayari kuishi na huyu binti na je nitamvumilia mangapi kwa mda gani? na je yeye kajiandaa kiasi gani kukubaliana na mapungufu yangu? na je ni kweli kuna chemistry between you too au mnaoneana huruma au mnafanya tu bila kujua kwa nini mnafanya? lingine mmemtanguliza Mungu kiasi gani katika kusimamia ndoa yenu au Mungu anapewa nafasi ndogo ndiyo maana hata kwenye kadi mnawaambia watu mkutane ukumbini huku tendo muhimu la ibada hamataki jamii ishiriki ,, na pia ninyi mpo pale kama misanamu tu huku mkiwa na mawazo sijui ukumbini kumepelea nini? sijui mtu wa keki kafika ? sijui kamati imekaaje?


muhimu ni kuandaa mioyo zaidi kuliko sherehe za masaa mawili wakati ndoa ni maisha ..........
hapa umesema la maaana ila ukiona mtu anatangaza nia ni kwamba karidhika na mwenzake
 
hapa umesema la maaana ila ukiona mtu anatangaza nia ni kwamba karidhika na mwenzake
kama karidhika na mwenzake mafigisu figisu baada ya ndoa yanatokaga wapi? kwa baadhi
 
kama karidhika na mwenzake mafigisu figisu baada ya ndoa yanatokaga wapi? kwa baadhi

ni kawaida huwezi kupredict future mambo yanabadilika na jinsi kila mmoja alivyo mvumilivu inatofautiana hata glass zinagongana kabatini sembuse watu?

hongera kwa kuandaa sherehe simple complication hazina msingi

kwanza mi hua najiuliza hata nikicomplecte harusi itavunja rekodi ngapi hata hapa mtaani tu
 
mkuu mimi hapa mama yangu akiongelea hayo mambo tunapishana kwa sababu tu mimi naamini ndoa na sitaki harusi.... kwa hiyo nimeshaamua na hapa nilipo najaribu kumshawishi huyu mpenzi wangu kuwa aachane na maswala ya harusi tufunge ndoa.. na namshukuru Mungu tupo karibu kuelewana japo anahisi kama kuna jambo namficha... ninakajukumu cha kuendelea kumshawishi mpaka tuelewane tu... mwenzangu akinielwa anakazi na yeye yakuelezea wazazi wake pia waelewe... now days bwana wazazi ndiyo wamekuwa watu wa kwanza kushurutisha harusi mara send off sababu kubwa atakuambia kuwa amechangia harusi nyingi na yeye anatakiwa achangiwe ambapo to me ni hoja jepesi tu hiii ... any way msimamo wangu siubadilishi sababu sitendi dhambi ila nafanya lile la msingi
Unaona tatizo hilo?yani kwanza uanze kuwaelewesha wazazi wako,pili umueleweshe wenzio halafu nayeye akawaeleweshe wazazi wake duh!japo naona inakuwa rahisi kwa upande wa kiume kukubali.
 
Kama ukishindwa kuwa na maamuzi thabiti ktk maisha yako baadae utapata shida kuendesha familia.Mwanamke siku zote analilia kuolewa na wazazi wa binti wanalilia mtoto wao kuolewa so unatakiwa uwe na msimamo binafsi watakaoufuata wao na haikatazwi ushauri ila uwe wa kuboresha mawazo yako si kuyaacha.

Wewe ndo mwanaume ukianza kusema oooh vp mwanamke atakubali hili mara lile! Kumbuka wanawake ni mapambo muda wote wanataka kung'aa hata kama ni msibani au wakati wa hali ngumu.

Mwanamke asiyeplan mbele anawaza alipo si atakapokuwa so ukisema umuulize juu ya harusi gani anayaka! Kwanza atachukua mifano ya hatusi za rafiki zake zilizofanyika au alizowahi kuhudhuria then atataka kati ya zote ya kwake iwe bora.

Be care unapochukua ushauri kwa mchumba hasa binti anayejua unamtaka kwa udi na uvumba na hasa akijua unampenda sana hata akitaka chupi tu atakuomba 100,000 wakati shida ni chupi.

Mytake:A brave man in the world is he who stands on his own.
 
Mwenzangu sio mtu wa kupenda masherehe makubwa makubwa kwa hiyo tulikibaliana vizuri tuu wala hakukuwa na shida.
Hatukutaka kuanza kukimbizana na watu michango ya harusi mpaka iwe kero, au tumalize harusi tuanze maisha na madeni kwa sababu ya sherehe ya masaa machache tuu. Hasa ukizingatia kuwa uwezo wetu kiuchumi ulikuwa ni.mdogo pia. Tulifanya kitu simple sana.
Bajeti ilikuwa kwa watu 60; ambao walikuwa ni ndugu zetu wa karibu ma close friends wachache.
Pesa kubwa ilienda kwenye chakula na vinywaji; ukumbi tulipewa bila kuulipia as i said hoteli ya nemax royal iliyopo kinondoni(kwa sababu vinywaji na msosi tulichukua hapo hapo).
Hakuna cha maids wa bibi harusi zaidi ya matron wa bi harusi na mpambe wangu.
Gharama nyingine ndogo ndogo zilikuwa ni keki,picha,shampeni. Ukumbi walitupangia tuu viti na meza vizuri na high table(no mapambo complicated).
MC akawa dada yangu, na tulitumia Public addressing system ya ukumbi tuka connect our laptop bro akawa DJ.
Mimi binafsi nilipenda sana jinsi ilivyokuwa kiukweli,it was nice and no stress!!! Na,hata waliohudhuria walisema nimefanya,kitu kizuri sana.
Bajeti(kadri ninavyokumbuka)
1.chakula
20,000 @ plate X 60=1200000
2.vinywaji(bei ilikuwa ni moja, Tshs 2,000 kwa bia au soda)
Kwa bia 4 @ 2000X 40=320000(kwa watu wetu tuliowaalika coz ni wa karibu,tunawajua personally,i tulijua wanywaji hawatazidi 40)
Kwa soda 3@ X 2000 X 20=120000
Picha za mnato=140,000
Keki= 250000
Usafiri wa wakwe(tulichukua noah ya mshikaji tukampa 40,000 na kuijaza mafuta)
Gari ya maharusi tulitumia ya kwangu.
Kupambwa bi harusi + kupamba gari ya maharusi 150,000
Champane @ 15,000 X 3=45,000
TOTAL 2,265,000. CHOCKSTIC
Unaweza kumpata mwelewa tatizo likawa kwa wazazi na ndugu,ukingalia tayari tushatofautana dini.
 
Back
Top Bottom